Samia awaonya madereva bodaboda

chaikavu

JF-Expert Member
Apr 18, 2015
760
473
Suluhu-3Sept2015(1).jpg

Mgombea mwenza wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu.

Mgombea mwenza wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu, ameonya vijana waendesha bodaboda kuacha tabia ya kuwarubuni wanafunzi wa kike kwa chipsi na 'lifti' jambo linalowasababishia mimba zisizotarajiwa.

"Vijana ninyi na vipikipiki vyenu mnawaharibia maisha watoto wa kike kwa kuwapa mimba zisizotarajiwa," alisema Samia

Kutokana na tatizo hilo, Samia alisema akichaguliwa yeye na mgombea wa urais kupitia CCM, Dk. John Magufuli atahakikisha anakabiliana na hali hiyo kwa kujenga mabweni ya wasichana katika shule za kata.

Alisema bila mabweni wasichana wa kike wataendelea kupata mimba zisizotarajiwa na hivyo kuharibu maisha yao.

Kuhusu tatizo la maji katika jimbo la Kibakwe, Samia aliahidi kutatua kero hiyo kwa kuchimba visima virefu.

Akizungumza na wananchi, mgombea wa Jimbo la Kibakwe, George Simbachawene, alikiri kuna tatizo sugu la maji na kuahidi kwamba wampe kura ili aweze kumaliza tatizo hilo.

Kwa upande wake, mgombea wa Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde, alisema kuna tarafa nzima katika jimbo lake ambayo haina umeme.

Lisinde alitumia lugha ya kigogo kuomba kura kama ilivyotokea katika Jimbo la Iramba Magharibi kwa Mwigulu Nchemba wiki iliyopita alipotumia lugha ya kwao kuomba kura.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa, aliwataka wapigakura kubali njia kuu na kwamba mchepuko siyo dili.

Kimbisa alimkabidhi Samia zawadi ya mbuzi jike katika Jimbo la Mtera ambaye hata hivyo hakuichukua na badala yake aliikabidhi kwa mkuu wa wilaya akimtaka aitunze mapaka azae mapacha.

Samia alikiri kuwa Jimbo la Mtera linakabiliwa na hali ya ukame, lakini akawahakikishia wananchi kwamba serikali itapeleka chakula kwa ajili ya kukiuza kwa bei nafuu.

Chanzo: Nipashe

MY TAKE:
Ambao hatuna mashangingi tunadharauliwa kwa kuwa na uwezo wa vipikipiki.

Kama tungekuwa na mashangingi kama wao tusingekuwa tunaonekana tumebeba hivyo vibinti maana wao wanapiga tinted hatuvioni vibinti.


 
Kuna pande mbili hapo! Wadada wafundishwe uzazi wa mpango mashuleni itasaidia sana! Maan hali zao huko vijijini ndio chachu wao kupata vishawishi! Hali ni Duni kijana anajituma anampeleka shule na anampa hela matumizi....amenunua simu etc....nini kitafuata!? Boda boda nao wana hisia na malimbukeni pia! Wana hela za kuchezea
 
Back
Top Bottom