Sambwee Shitambara aachwa solemba na wananchi

Zitto kujadiliwa humu kunatokana na kufamika kwake kwa mengi mazuri na mabaya. Zitto alipoibua kashfa ya Buzwagi akatimuliwa bungeni sote tulimsifu, si jf tv au magazeti. Lakini alipoanza kupoteza ramani sote tukamgeuka. Kwa hiyo, haonewi anapewa haki yake. Je, alituambia kuwa,
Tununue downs, zitto ana mawasiliano ya karibu na Naibu mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Zitto Swahiba wake ni Rostam. Ushahidi uliwekwa uk wa mbele wa magazeti. Je, tusimjadili kwa hili? Yeye aje ajibu hayo, mambo au aombe radhi. Haonewi mtu hapa.
 
Sambwee ipo ufwile fwa. ilile huliwe iyo. nganga uiga wewe watitwalile hechadema! pole sana. Tili ni njele zyetu ngashee yi sukulu nati timanyile sana hata azidi iwe. Halafu uleshi amahelu. vasi waizengile ichadema! enya itunga!

uenda ukawa umeandika jambi zuri sana ila ndo sikupati
 
Jamani hizi habari za Zitto sasa zinatosha lakini kwa kuwa ipo hapa JF, ngoja tuchangie kidogo;

Kwanza napongeza mchango wa Zitto kwa Chadema ila sio kweli kwamba yeye peke yake ndio kakiweka hapo Kilipo ila ni kwa ushirikiano wa Viongozi wote na Wanachama wote pia.

Pili Zitto bado ni kiongozi wa Chadema ila tulio wengi kwa siku za hivi karibuni hatumwamini sio kwa kuwa aligombea uenyekiti lahasha ni kwa mienendo yake ya hivi karibuni, ila kwa kitendo cha jana kusimama na kumtetea mbunge mwenzake Wenje nime msifu na ninampongeza popote alipo alionyesha kukomaa na kukua na pia kupigania maslahi ya Chama Bungeni, kwa Hilo nakupongeza Mh Zitto, ila ushauri wangu narudia kama ni kweli ulijikwaa sehemu tafadhali rudi kwenye mstari kaka tutaanza kukuamini tena, wengi huwa tunakosea ila unaposemwa na kugundua unajirudi. hakuna mtu asiyekosea mkuu ila si busara kuzarau ushauri hasa pale wanao kushauri wanakushauri kwa kutaka ufanikiwe zaidi, Ubinafsi haufai.
 
Wazee mbona muna hasira? Mbona hatukusikia haya mlipo mpokea Prof. Safari? Akihamia poa, akihama noma? Acheni hizo!

Prof. Safari aliondoka cuf akakaa muda mrefu na kutathimini chama cha kwenda na akaona cdm ndo mahala pake wala hakwenda ccm. Hata huyo shitambala kama hakuwa mamluki si angeenda upinzani kama yeye ni mpiganaji !?
 
Zitto kujadiliwa humu kunatokana na kufamika kwake kwa mengi mazuri na mabaya. Zitto alipoibua kashfa ya Buzwagi akatimuliwa bungeni sote tulimsifu, si jf tv au magazeti. Lakini alipoanza kupoteza ramani sote tukamgeuka. Kwa hiyo, haonewi anapewa haki yake. Je, alituambia kuwa,
Tununue downs, zitto ana mawasiliano ya karibu na Naibu mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Zitto Swahiba wake ni Rostam. Ushahidi uliwekwa uk wa mbele wa magazeti. Je, tusimjadili kwa hili? Yeye aje ajibu hayo, mambo au aombe radhi. Haonewi mtu hapa.

Mwanajamii umefafanua vizuri sana, na kwa upande wangu naona umefunga mjadala kwakweli, hamna jiwe litakalo achwa bila kugeuzwa.... hata CCM (TANU) ilitupatia uhuru lakini leo inahojiwa kwa mambo ya msingi, HAMNA UONEVU!!
 
JAMANI LAZIMA TUSEME UKWELI, CHADEMA ILIKUWEPO KABLA YA ZITTO KABWE, WAMEPITA WATU WENGI MASHUHURI KAMA MHE AMAN KABUROU MBUNGE WA ZAMANI WA KIGOMA MJINI NA ALIKUWA KIONGOZI MKUBWA CHADEMA TAIFA LAKINI YUKO WAPI,

ZITTO NI MUHIMU SANA KWENYE CHAMA LAKINI LAZIMA NA YEYE ZITTO AKUBALI, CHAMA KITABAKI HATA KAMA YEYE ASIPOKUWEPO, UKWELI NI KWAMBA ZITTO ANAKITEGEMEA CHADEMA NA CHADEMA KINAMTEGEMEA ZITTO KWA SABABU NI MIONGONI MWA VIONGOZI.

NI UKWELI ZITTO ALIPATA UMAARUFU MKUBWA SANA KIPINDI CHA HOJA YA BUZWAGI LAKINI HAKUSOMA ALAMA ZA NYAKATI MAANA BAADA YA PALE AKATAKA NA UONGOZI MKUU WA CHAMA KISA TU NYOTA IMEMWAKIA,

USHAURI KWA ZITTO!!!!!! Wewe ni kiongozi mzuri na vijana wengi wako nyuma yako, lakini usiwe na haraka sana ya kupata madaraka makubwa, umri wako unakuruhusu kuja kuwa kiongozi mkubwa baadae lakini acha watu wakuone badala ya wewe kujionyesha kwa watu. Muangalie Nyerere kipindi kile alikuwa anawasikiliza wazee, wakamfanyia matambiko mengi pamoja na kumfingisha lakini nyerere hakuwadharau aliwasikiliza hatimaye wakamwamin na kumpa uongozi wa chama na hatimaye nchi.
 
Zitto kujadiliwa humu kunatokana na kufamika kwake kwa mengi mazuri na mabaya. Zitto alipoibua kashfa ya Buzwagi akatimuliwa bungeni sote tulimsifu, si jf tv au magazeti. Lakini alipoanza kupoteza ramani sote tukamgeuka. Kwa hiyo, haonewi anapewa haki yake. Je, alituambia kuwa,
Tununue downs, zitto ana mawasiliano ya karibu na Naibu mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Zitto Swahiba wake ni Rostam. Ushahidi uliwekwa uk wa mbele wa magazeti. Je, tusimjadili kwa hili? Yeye aje ajibu hayo, mambo au aombe radhi. Haonewi mtu hapa.
Amakweli wewe ni ndundu, inamaana unampangie marafiki? awe huru kuwa karibu na yeyote yule. siasa sio uadui?
 
Mimi nipindishe mjadala kidogo ingawa sitotoka nje sana! Watanzania wengi bado tuna "siasa za kujitenga na za uhasama"; nikiwa na maana ya kusifu kinapokuwa chetu hata kama hakina maana na kuponda/kupinga cha wenzetu hata kama kina maana. Na kwa uelewa wangu hizi ni siasa za kiCCM ambazo zisingelipaswa kupewa nafasi ndani ya vyama makini.

Nimesema hayo hapo juu nikikusudia shutuma anazoshushiwa Zitto (Zitto mnafiki, Zitto ananunuliwa, Zitto rafiki wa EL, RA, RK...Ni jana tu wengi walitaka kumtundika eti kwa sababu kawapongeza Makamba na Nape). Huwa ninajiuliza, hivi kwa sababu Zitto ni CDM hawezi kuwa na marafiki kutoka vyama vyengine? Kwa kuwa mtu ni mkristo awe KKKT au katoliki; mwislamu awe sunni au shia; ni dhambi kuwa na marafiki wa dini nyengine? Si mawazo wala maoni ya kujenga wala si kero za Tanzania. Tanzania ina kero nyingi, tujadili hizi tusijadili watu. Naomba niwe nimekosea ili wanaomshutumu Zitto wapate kusema "tulisema zamani", lakini binafsi nina imani naye wala urafiki wake na watu wa CCM, CUF, UDP au yeyote, maoni yake hata kama mara nyengine yanatofautiana na CDM, hayamfanyi awe si kiongozi mzuri, imara na muhimu kwa CDM. Kwangu mimi Zitto atabakia kuwa kongozi mzuri wa CDM na sitomhukumu mpaka athibitishe/athibitishwe kuwa kinyume na hivyo.

Nawasilisha na nasubiri kusulubiwa.
 
Sambwee ipo ufwile fwa. ilile huliwe iyo. nganga uiga wewe watitwalile hechadema! pole sana. Tili ni njele zyetu ngashee yi sukulu nati timanyile sana hata azidi iwe. Halafu uleshi amahelu. vasi waizengile ichadema! enya itunga!
Ndaga fijo naloli
 
Mimi nipindishe mjadala kidogo ingawa sitotoka nje sana! Watanzania wengi bado tuna "siasa za kujitenga na za uhasama"; nikiwa na maana ya kusifu kinapokuwa chetu hata kama hakina maana na kuponda/kupinga cha wenzetu hata kama kina maana. Na kwa uelewa wangu hizi ni siasa za kiCCM ambazo zisingelipaswa kupewa nafasi ndani ya vyama makini.

Nimesema hayo hapo juu nikikusudia shutuma anazoshushiwa Zitto (Zitto mnafiki, Zitto ananunuliwa, Zitto rafiki wa EL, RA, RK...Ni jana tu wengi walitaka kumtundika eti kwa sababu kawapongeza Makamba na Nape). Huwa ninajiuliza, hivi kwa sababu Zitto ni CDM hawezi kuwa na marafiki kutoka vyama vyengine? Kwa kuwa mtu ni mkristo awe KKKT au katoliki; mwislamu awe sunni au shia; ni dhambi kuwa na marafiki wa dini nyengine? Si mawazo wala maoni ya kujenga wala si kero za Tanzania. Tanzania ina kero nyingi, tujadili hizi tusijadili watu. Naomba niwe nimekosea ili wanaomshutumu Zitto wapate kusema "tulisema zamani", lakini binafsi nina imani naye wala urafiki wake na watu wa CCM, CUF, UDP au yeyote, maoni yake hata kama mara nyengine yanatofautiana na CDM, hayamfanyi awe si kiongozi mzuri, imara na muhimu kwa CDM. Kwangu mimi Zitto atabakia kuwa kongozi mzuri wa CDM na sitomhukumu mpaka athibitishe/athibitishwe kuwa kinyume na hivyo.

Nawasilisha na nasubiri kusulubiwa.
Mkuu hapo umenena maana tunatakiwa kubadilika na kuacha siasa za vijana wa CDM walio na chuki na Zitto sambamba na genge la Membe lililojaa huku wakiungana kumchafua Zitto
 
Bado mlio wengi mna me tazamo hasi, kosa lake ni kuwa na mawasiliano na Usalama wa taifa?wangapi wana ushahidi wa nini walichozungumza?tuna uhakika gani alikuwa anasaliti chama katika mazungumzo yao?akisema alikuwa ana habarishwa masuala muhimu juu ya usalama wake na chama chake?nani asiyejua taarifa nyingi nyeti alizokuwa anatoa SLAA source yake ni kuvuja toka huko usalama?au kosa ni Zitto tu kuzungumza na Usalama na ni sawa kwa Mbowe na Zitto?

Kuna mambo binafsi tunatka kuingilia kwa kumchagulia mtu marafiki, kosa ni yeye kuwa na urafiki na Rostam na wengine wanaotajwa ni wachafu?inawezekana anataka kuwashauri waache uchafu wao?inawezekana anataka kujifunza zaidi ili apate pa kuanzia?kwanini tunawahai kuhukumu?kuna picha ngapi zimetolewa Slaa akiwa na JK?ngapi Mbowe akiwa na vigogo wa CCM?au kosa ni Zittp akifanya hivyo?

Bado naendelea kuamini mchango wa Zitto ni mkubwa kuliko mdhaniavyo hii inathibitishwa na Ushindi wa Kafulila kule kigoma ni baada ya mchango mkubwa wa Zitto mbona wa Chadema hakushinda?Hakika nawathibitishia kuwa Zitto leo akitoka Chadema hakika chama kitameguka

Wana jf naomba kuwauliza kwanini zitto?kila napoona thread ya mtu aki comment postive kuhusu zitto watu wanakashifu na kumkosea heshima?

Naamini na nitaendelea kuamini hivi - heshima kubwa iliyo nayo cdm mbele ya watanzania kwa mchango mkubwa ni kwa ajili ya zitto, wangapi mlikuwa wanachama au mashabiki wa cdm kabla ya zitto kuwasha moto katika bunge la tisa?wangapi mlikuwa mnaikubali cdm kabla ya zitto kuonyesha msimamo thabiti mpaka kufukuzwa bungeni katika kashafa ya buzwagi? Hebu kuweni waungwana na mpeni heshima yake jamani

wengi mnamuona zitto mbaya toka alipotaka kugombea uenyekiti wa cdm , ila si ametumia haki yake ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa?mnamuona mbaya pale anapotofautiana mitazamo na baadhi yetu- ila mitazamo tofauti daima ni manufaa ya chama kama daima mnakubaliana hamuwezi kuwa na jipya
 
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, amesema aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mbeya, Sambwee Shitambala, amejimaliza kisiasa kwa hatua yake ya kuhamia kwenye kinachochungulia kaburi.
"Nimeshtushwa sana na uamuzi wa Shitambala kuhamia CCM najua ametumia haki yake ya kidemokrasia lakini hakuweza kusoma alama za nyakati …CCM aliyoikimbilia inaelekea kufa, amejimaliza na atakuja kujutia uamuzi aliochukua wakati CHADEMA sasa ndiyo chama kinachozidi kupanda chati," alisema Zitto.

My take: Maneno haya ya Zitto nayashikilia kwa mikono miwili nisije kuyasahau.
 
kwa kweli amejimaliza chadema tunachukua nchi 2015,yaani ameshindwa kusoma alama za nyakati kweli?
 
Shitambala ameingia kwenye orodha ya wanasiasa ambao Mheshimiwa FT Sumaye anawaita "wanasiasa maslahi" ambao wamechangia kuiua ccm. Huu ni ushahidi tosha wa kimazingira kuwa huyo bwana kwa kufuata maslahi hayahaya aliuza jimbo uchaguzi wa 2010. Kweli nimeamini Chadema ni chama makini, yaani naye angesubiri maandamo haya yafanyike, angeshushwa jukwaaani kwa kuwa he lost the trust from the Chadema supported from Mbeya

Amejimaliza mwenyewe
 
Sambwee ipo ufwile fwa. ilile huliwe iyo. nganga uiga wewe watitwalile huchadema! pole sana. Tili ni njele zyetu ngashee yi sukulu nati timanyile sana hata azidi iwe. Halafu uleshe amahelu. vasi waizengile ichadema! enya itunga!
An official translation. 'Sambwee hapo umekufa tu. Imekula kwako. Labda unafikiri wewe ndiwe uliyetupeleka Chadema! Pole sana. Tuna akili zetu. Kama ni shule hata sisi tumesoma pengine hata kukuzidi. Tuna uache matusi - Eti uliijenga Chadema - ona uchawi huu!!'
 
Shitambala acha kujitia aibu, eti unasimama kwenye mkutano na unadiriki kusema muswada wa katiba hauna tatizo lolote? Kelele zote toka bara hadi visiwani wote hao ni wendawazimu? Hata kama umeondoka CDM nakushauri simamia ukweli na acha njaa maana unaumbuka.:panda:
 
Back
Top Bottom