Sambwee Shitambara aachwa solemba na wananchi

Mkutano ulioandaliwa na CCM kwa lengo la kumpokea mnafiki na msalititi aliyewasaliti wana-Mbeya vijijini na CDM, umeingia dosari baada ya wanachi wachache waliokuwa wamehudhuria ktk viwanja vya Kibondenyasi/Freepark-Uyole kumzomea na kusababisha vurugu zilizopelekea mkutano kufungwa kabla ya muda uliokusudiwa..
Mkutano huo ulio hudhuriw ana viongozi na vigogo waandamizi wa chama hicho Mzee wa Mtela-JOHN Malechella na Pof. Mark Mwandosya, uliingia dosari baada ya mbunge aliyeuuza ubunge huo na utu wake kwa kuwasaliti wana-Mbeya vijijini na kujipendekeza kwa CCM na kuwauzia ubunge wake alioshinda... kuwaambia wananchi wa Mbeya ambao wamechoshwa na usanii wa ombwe la watawala wa nchi hii, kuwa wasishiriki katika maandamano yaliyoandaliwa na CDM yatakayo fanyika jumamosi hii na kusimiwa na kamanda MBOWE Freeman, kwa madai kuwa wakafanyie maandamano hayo kwao Moshi....
mara uwanja ukatawaliwa na alama za vidole viwili (V) kuzomea na kum(wa)beza mwana-ccm huyo mpya asiye na dira... wala mwelekeo... big-up wapiganaji wa Mbeya****
Hata hivyo uamuzi huo wa kujiudhuru kwa aliyekuwa m/kiti CDM mkoa wa Mbeya na kuhamia ccm uli(me)pokelewa kwa shangwe na wana chama na wapenzi wa CDM-Mby: tofauti na matarajio yake na ahadi yake kwa m/kiti wa ccm-taifa ndg. JK kuwa angeondoka na wana-CDM zaidi ya 150, kaishia kuondoka yeye na chokoraa mmoja wa Ileje-Mby.:brick::behindsofa::pray2:
TUKUTANE JUMAMOSI KWENYE MAANDAMANO YA KI-HISTORIA;
 
akome kucheza na filosofia za watu .......na iwe fuyndisho kwa wengine.. ghongera sana watu wa mbeya...
 
Mkuu kama haya unayosema ni kweli basi wananchi wa mbeya wanastahili pongezi maana usanii wa CCm umezidi sasa
 
priceless chap! CDM kaharibu,CCM hauziki..keshalikoroga

Mkuu kitu kikiwa priceless maana yake ni kwamba kina thamani kubwa kuliko bei yoyote utakayofikiria. Sijui kama ulikusudia hivyo mkuu, Kama ndivyo mkuu nisamahe
 
Mbona kulikuwa na watu wengi sana? Pia wajumbe wa CCM kutoka wilaya mbalimbali walihudhuria.

Ujumbe wako hauko sahihi kabisa.
 
Namuonea huruma sana maana wale wote ambao walikuwa wapiga madebe ndio wametoka CCM sasa Makamba na Tabwe naye atafulia ile mbaya sana na anadhani kuwa wananchi wa siku hizi wapo vipi
 
Mbona kulikuwa na watu wengi sana? Pia wajumbe wa CCM kutoka wilaya mbalimbali walihudhuria.

Ujumbe wako hauko sahihi kabisa.

Watu wengi waliotulia kusikiliza utumbo kama ni kipimo cha kukubalika - zomea zomea ilikuwa ya nini?? Professor naye anazeeka vibaya!!!!
 
Nadhani CHADEMA tunapozungumzia Nguvu ya Umma kuamua kujikomboa kuondokana na Mafisadi akina Sitambala mpaka utawala wa nchi hi na rasilmani kurudi mikononi mwetu, wengi wa waporaji ndani ya CCM huenda hatuelewani nao vema na hata kudhani kana kwamb tunataniana tu hapa.

Jamani katika vita hivi wala mtu na au taasisi yoyote isipoteze muda wake hata kutembeza rushwa maana kama ni hela tutazichukua kwa sana tu na azma yetu ya kuleta mabadiliko ya aina yake iko pale pale!!!

Wewe Sitambala katambae mbele salama ila usubiri kujibu mashitaka mahakamani kama uliwahi kutuibia na au kusaidia kuibiwa Umma wa Tanzania.

Shitambara ameiona NGUVU ya UMMA aachwa akisikilizwa na wana CCM wenye mashingingi ,ikiwa kwenye mkutano Uyole alikuwa akisikilizwa na wanachi nadhani wana CCM wachache pemeni kukiwa na wanachadema na bendera zao wakizipeperusha huku wakisikiliza alivyosema tuu jumamosi musihudhurie kwenye maandamano yaliyoitishwa na Chadema akashangaa hicho kikundi kidogo kilichokuwa kikimsikiliza wakiondoka mmoja baada ya mmoja saa hizi kabaki na wale wenye mashangingi na FFU na vinq'ola vinaingia jamani wanachi sio wakuchezea kwa kweli
 
Back
Top Bottom