Samaki wa Magufuri wagawiwa bure

Jamani waziri ameamua samaki waliwe na wananchi, ninyi mnaleta maneno mengi.
Hivi angeamua kuchukua 10% yake toka kwa hao wavuvi haramu na akawacha waendelee zao ingekuwa faida ya nani?

Na wangeliwaje wakati kesi ilikuwa bado inashughulikiwa kujua uhalali wa hao wavuvi waliovamia maji yetu.

Mwacheni afanye kazi yake. Sidhani kama Magufuli anaweza kuwauwa wananchi wake kwa kuwapa chakula kibaya. Kama kilihifadhiwa vyema haina shida.

Mbona mnaletewa expired food/bidhaa toka nche ya nchi na zimejaa madukani kibao na hamsemi?? sembuse samaki wetu??? Ama kweli huwazi kumfurahisha binadamu.
hao samaki tayari washaingizia taifa hasara kama kawaida kutokana na uzembe wa serikali yetu.mambo hayo ya kugawa wangefanya toka mwanzo kama kweli walikuwa na nia yakutupa samaki wetu lakini wakaka kufanya kesi nzito wakati ushahidi wote wanao na wao ndio serikali ni kiais cha kufanya maamuzi tu ilikuwa.hao samaki wangetupa watanzania huku wao wanaendelea na kesi yao au wangeuzwa toka wakati huo hili taifa lipate hela.sasa wameenda kukaa na samaki mpaka nchi imeingia hasara leo ndio wanajifanya wanagawa.wizi mtupu kila kitu dili nchi hii.jaribu kuchunguza nani alilipwa hela za kuifadhi samaki?
 
Tuanze na ukwelisamaki hao ni mali ya serikali, halafu pili kuwa samaki waliokamatwa ni tani 296, je bei ya samaki hao ni shs ngapi kwa bei ya kulazimisha kuuza ( forced sale ) au bei ya soko ( market value ) sio chini ya milioni 100.Je sheria ya manunuzi inaruhusu mtu mmoja kuamua peke yake kuuza mali ya serikali? Au uamuzi uliofikiwa ulifikiwa na , lini na kwa kigezo gani.
 
Tuanze na ukweli kuwa samaki hao ni mali ya serikali, halafu pili kuwa samaki waliokamatwa ni tani 296, je bei ya samaki hao ni shs ngapi kwa bei ya kulazimisha kuuza ( forced sale ) au bei ya soko ( market value ). Kwa vyovyote sio chini ya milioni 100.Je sheria ya manunuzi inaruhusu mtu mmoja kuamua peke yake kuuza mali ya serikali? Au uamuzi uliofikiwa ulifikiwa na nani, lini na kwa kigezo gani.??????
 
Hao samaki mimi naona bora wakateketezwa kuliko kugawiwa bure, kwani licha ya kuhifadhiwa kwa muda wote huo toka machi hadi leo, nadhani hawatakuwa na ladha. Pia nahisi hizi ni kampeni kwa nini sasa na sio muda ule walipokamatwa?
 
Lakini kwa muda waliokaa kwenye barafu, kweli watakuwa bado wanafaa kwa matumizi ya binadamu, isije ikawa wateja wamekosekana ndo wakaamua kuwauza, baada ya miezi kadhaa magonjwa ya ajabu yanaibuka,

Samaki si walihifadhiwa kwenye barafu mjomba?,na walitaka kupigwa mnada watu wakashindwa kununua kutokana na ukubwa wa bei.
 
Kuna waliokuwa wanasema eti mimi natoa habari za udaku, sasa wanieleze nani katoa hii habari wa kwanza hapa JF na angalia vyombo vyote vya habari leo, habari hii inaongoza

Usimdharau usiyemjua
 
Mwenye majibu atusaidie:-

Samaki waliokamatwa na Magufuri walikwenda wapi?
Ile meli ilikwenda wapi?
Najua kesi ilishakwisha je hatudaiwi?
 
Inaonesha ni kiasi gani ulivyovamia siasa, rudi MMU ndo saizi yako
 
Mwenye majibu atusaidie:-

Samaki waliokamatwa na Magufuri walikwenda wapi?
Ile meli ilikwenda wapi?
Najua kesi ilishakwisha je hatudaiwi?

Meli ilizama Tafico pale serikali inadaiwa mabilioni kadhaa nadhani walishalipa, samaki waligawana.
 
Tuliwala wote. Aisee kuna watu wanafaidi sana. Ile minofu ya samaki sijawahi kula kabla ya kutuonjesha Magufuli. Akiwa Rais nadhani kile ndo kitakuwa kitoweo chetu na si hawa udufi
 
Jamani waziri ameamua samaki waliwe na wananchi, ninyi mnaleta maneno mengi.
Hivi angeamua kuchukua 10% yake toka kwa hao wavuvi haramu na akawacha waendelee zao ingekuwa faida ya nani?

Na wangeliwaje wakati kesi ilikuwa bado inashughulikiwa kujua uhalali wa hao wavuvi waliovamia maji yetu.

Mwacheni afanye kazi yake. Sidhani kama Magufuli anaweza kuwauwa wananchi wake kwa kuwapa chakula kibaya. Kama kilihifadhiwa vyema haina shida.

Mbona mnaletewa expired food/bidhaa toka nche ya nchi na zimejaa madukani kibao na hamsemi?? sembuse samaki wetu??? Ama kweli huwazi kumfurahisha binadamu.

kweli mnaomtetea mfa maji mwenzenu ubongo wenu una capacity ndogo samaki hawakukamatwa na magufuli walkamatwa na askari wa majini yeye alitoa maamuz tu
sema askari wangechukua rushwa
stone level wewe
 
Tuliwala wote. Aisee kuna watu wanafaidi sana. Ile minofu ya samaki sijawahi kula kabla ya kutuonjesha Magufuli. Akiwa Rais nadhani kile ndo kitakuwa kitoweo chetu na si hawa udufi

aya na hizo ndoto zako mchumia tumbo
 
Back
Top Bottom