Samaki wa Magufuli kuoza?

Msongoru

JF-Expert Member
Apr 16, 2008
306
24
Na Tumsifu Sanga

LICHA ya mahakama kuruhusu uuzaji wa samaki waliokuwa wamevuliwa kwa njia haramu zoezi hilo linaonekana kukwama kutokana na kukosekana kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Uvuvi chini.

Akizungumza na mwananchi ofosini kwake jana jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa kampuni ya Yono Action Mart, Yono Kevela alisema tayari mahakama imeshatoa idhini ya kuuza samaki hao lakini bado hawajapata kibali kutoka kwa mkurugenzi ambaye ndiye atakapanga bei ya kuuza.

“Mnada wa kwanza tulishindwa kuuza kutokana na malalamiko kutoka kwa wateja wakitaka tuwapunguzie hali ambayo ilisababisha kuvunjika kwa mnada na kusitisha zoezi zima la kuwauza wale samaki,”alisema

Ombi la wateja limesikilzwa na bei itapungua ndio maana nimekuambia siwezi kukuambia tunategemea kupata shilingi ngapi kwani hatutegemei kupata kiasi cha sh. 2 bilioni kama tulivyotegemea hapo awali.

Alisema kuwa kama kibali kitatoka mapema wmwishoni mwa wiki hii wanaweza kuanza kuwauza samaki hao wanasadikiwa kuwa tani mia mbili.

Yono alisema ili kuiondolea serikali hasara ya mamilioni inayolipa kwa ajili ya kuhifadhi samaki hao, ingependeza kama tungempata mteja wa jumla naye akawauza kwa wateja wadogo wadogo.

Aliongeza kuwa wateja wanaohitaji samaki ni wengi isipokuwa tatizo lilikuwa katika bei ya kuuza ndio iliyokwamisha zoezi zima la mnada kuendelea.
 
Wawape wafungwa wajinome.....maana wanataka wapate faida mara 15 wakati hawaja invest
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom