Sumba-Wanga
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 5,349
- 1,224
Jana ilikuwa siku ya kwanza ya kazi baada ya mwaka mpya. Kama kawaida wakati wa tea time and hata lunch, colleague hawaachi kulete story za hapa na pale. Basi likaja swala moja ambalo lilileta ubishi na mzozo mkubwa, wanaume wakivuta kwao na wanawake nao wakisema lao. Kuna dada mmoja mwenye ndoa alilalamika kwamba wanaume wengi wanadhani kwamba jukumu lao ni kuoa mwanamke na kumweka ndani, na baada ya hapo ni kuhudumia family kwa mahitaji ya kula, na mavazi., FULL STOP. jukumu jingine la unyumba (ambalo wakina dada walidai kuwa ndio linalowatoa kwa wazazi wao kwenye vitanda na chakula kama kwa waume zao), linasaharika na kupewa umuhimu mdogo. Badala yake, wanaume wengi wanakuwa busy na vimada na mahawara, wanaacha kzai za ndani. Sasa kwa kuwa wanawake nao wanana mahitaji yao ya unyumba, na mume hapatikani, basi ndipo wanapoangukia mikononi mwa serengeti boys/mahawara.
Kwa kweli hadi mwisho hakukuwa na jibu la kueleweka: wanaume wanadia kwamba samaki ukishamvua kutoka majini hukuna haja tena ya kumpa chakula, na wanawake wanasema hawakufuata chakula na vitanda kwa maana hata walipotoka vipo. Wana JF, mnalionaje hilo?