Magulumangu
JF-Expert Member
- Jan 7, 2010
- 3,047
- 452
Wale waloishi au kukaa maeneo ya Dodoma mnajua samaki wa kule jinsi walivyona shombo, wale wa kanda yetu ya ziwa Victoria mnajua Sato na Chengu zinavyochengua, kwa wale wa Pwani mnajua pweza mtabiri alivyokamata, na kule kwetu kilimanjaro na kwingineko mwajua walivyo samaki wenu, swali sasa, Leo nimekula samaki asie na shombo nikajiuliza huyu samaki wa wapi jamani? Hata kidogo hana shombo, hata ingekuwa shombo ya ng,ombe ningeelewa lakini hana hata kidogo, je umeshawahi kula samaki asie na shombo hata kidogo? Nijuzeni wakulu au wangu wa kichina nini?