Samahani... watoto hawa wameniliza.. sasa najiuliza..

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987

Je tutawaachia taifa tulilonalo hivi? Je tunataka wakue katika mfumo huu huu ambao wengine umechukua maisha yao; je wanajua wanaimbia "Tanzania" kama wazo.. ? Nimeshindwa kujizuia.. lakini I think I needed it..
 
Last edited by a moderator:
pole sana mkuu,
unaweza kuniwekea picha yao niwaone maana sioni kitu mkuu
 
Halafu wakirudi darasani wanakaa chini kwenye mavumbi huku gavana wa benki kuu akitanua kwenye jumba lake lenye bwawa la kuogelea na viyoyoyozi na makorokoro mengine yaliyoagizwa toka majuu...
 
Kweli mkuu, laiti wangelijua hiyo Tanzania ilisha porwa na sio yetu wote. Hata binti yangu huniimbia wimbo huu kwa madaha makubwa lakini hajafikia uwezo wa kumueleza anielewe kwamba hii Tanzania ilishaporwa na inahitaji kukombolewa ili irudi kwenye hadhi yake kama wimbo huu ulivyo maanisha. Saa ya ukombozi ni sasa.
 
Mwanakijiji,

Tanzania ya JINSI HIYO (wanavyoimba)naweza nikasema kwa sasa kuwa ni 'MYTH"!....imeshakufa.

Namshukuru Mungu kwamba angalau niliiona Tanzania ya wakati huo, iliyokuwa imejaa uzalendo na hisia nyingi za upenzi wa nchi wa bila kulazimishwa!

Nakumbuka wimbo huu uliimbwa siku mwili wa Mwalimu ukiwa unaagwa pale uwanja wa Taifa kwenye kibanda, kweli watu wengi sana walitokwa na machozi, nadhani walikuwa wakipata maono kwamba huo ndio mwisho wa mshikamano wa kitaifa, na mwanzo wa ubinafsi!

Mungu Ibariki Tanzania!

Sasa hivi Tanzania lazima iwe ni za wazo ambalo tunataka iwe; Nadhani watu wengi wanasahau kuwa Tanzania ni nchi iliyoanzishwa tofauti sana na nchi nyingine zakiafrika.. ndio zao pekee la juhudi za Waafrika wenyewe kuwa nchi.
 
Tatizo lako wewe unaleta Umarekani kwenye mambo ya bongo.....nakumbuka kule YA ulielezeaga vizuri sana jinsi Marekani ilivyo "wazo" hadi watu wakakuuliza kama tayari umeshapata kile kitabu cha bluu....lol
 
Je tutawaachia taifa tulilonalo hivi? Je tunataka wakue katika mfumo huu huu ambao wengine umechukua maisha yao; je wanajua wanaimbia "Tanzania" kama wazo.. ? Nimeshindwa kujizuia.. lakini I think I needed it..

Hata mimi chozi limenilengalenga.Malaika hawa hawajui lolote.
 
Last edited by a moderator:

Je tutawaachia taifa tulilonalo hivi? Je tunataka wakue katika mfumo huu huu ambao wengine umechukua maisha yao; je wanajua wanaimbia "Tanzania" kama wazo.. ? Nimeshindwa kujizuia.. lakini I think I needed it..

Itapendeza siku moja ukajumuika nao ukalia mbele yao!!!!
 
Last edited by a moderator:
watoto hawa ni mashahidi wa jinsi wazazi wao wanavyoteseka majumbani kupata chakula na mavazi yao, kwa wavulana wengi wanaandaliwa kuwa makjambazi kwa mfumo mbovu usiokuwa na usawa unaoendelea sasa hivi, na kwa wasichana wanandaliwa kufanya biashara chafu kutokana na ugumu wa maisha ampapo kwa Tanzania mwenye nacho leo ndo atadumu kuwa nacho na wazazi masikini hawana cha kuwalisisha watoto wao wapendwa.

Tanzania Nchi yangu usikate tamaa, mabadiliko ni sasa.
 
Mwanakijiji... Umalia kweli au ni fiksi zako?

Halafu hii shule haina wanafunzi wakubwa? maana naona wote ni wadogo tu, like std 1.

Anyway... That is Tanzania... katika mikono ya wasaliti
 
nilitamani niwaone hao watoto nami nilie, hebu tuwekee picha hiyo, au ile ya watoto wa shule ya msingi wakiimba wimbo wa Taifa
wakiwa wamechafuka na miguuni hawana viatu.....
 
Bado tunaweza tukawaachia mwanzo mzuri hawa watoto wetu kama tu tutaamka na kushikamana katika kutetea maslahi yao .
Tukiungana pamoja twaweza weka msingi ambao wao watauendeleza na maneno ya huo wimbo yakawa yanatoka moyoni kil mara watakapokuwa wanauimba.
 
Kinacho uma zaidi hao watoto wengine wana njaa hawajala chochote asubuhi wkt wanatoka majumbani kibaya zaidi wengine hata kuoga hawajaoga kutokana na bajeti ya maji kuwa kali wanajipaka tu umande usoni na miguuni imetoka. Alafu kuna watu wanataka watuaminishe kuwa sasa hivi umaskini umetoweka na watu wanakula milo 3 kwa siku.
 
nilitamani niwaone hao watoto nami nilie, hebu tuwekee picha hiyo, au ile ya watoto wa shule ya msingi wakiimba wimbo wa Taifa
wakiwa wamechafuka na miguuni hawana viatu.....

awali nilikuwa na nina mwawazo kwamba klila kinachoandikwa JF ni keki kumbe ba pumba nazo zimo. Hata kama ni uhuru wa mawazo, mawazo mengine ni bora kuyafungia kwenye kabati.Sasa watoto wa shuke ya kuchafuta inatoa picha gani?
 
Je tutawaachia taifa tulilonalo hivi? Je tunataka wakue katika mfumo huu huu ambao wengine umechukua maisha yao; je wanajua wanaimbia "Tanzania" kama wazo.. ? Nimeshindwa kujizuia.. lakini I think I needed it..

Plzz Mzee MKJJ kama unaweza kuweka kwa format nyingine nitashukuru ili na mimi niweze kulia?
 
Last edited by a moderator:
awali nilikuwa na nina mwawazo kwamba klila kinachoandikwa JF ni keki kumbe ba pumba nazo zimo. Hata kama ni uhuru wa mawazo, mawazo mengine ni bora kuyafungia kwenye kabati.Sasa watoto wa shuke ya kuchafuta inatoa picha gani?
Kama na wewe umo kwenye line ya uchafu huwezi kuelewa kuelewa ujumbe alioleta MKJJ na mwenye shibe hamjui mwenye njaa akiona mtu anapiga miayo hufikiri kashiba sana hayo ndiyo mawazo yako yanavyotaka kutuambia.
 
Back
Top Bottom