Salva Rweyemamu maneno haya ni yako?

hii ni hatari kwa mstakabari wa taifa letu, mzee wa miaka 60 anajifanya nae ni kijana wa miaka 25.
 
Baada ya kazi ipi? Yani kusafiri toka dar mpa hapa ndo kazi?
Kuna ulazima gani wa kusafiri na kundi la watu zaidi 50? Tatizo vijana mliotumwa kuitetea serikali katka mitandao ya kijamiii hamkupewa nature ya mwajiri wenu na kazi yenu!!
Tukisema njaa wanaona wametukanwa lakini ukweli utabaki pale pale kuwa siyo sahihi kiongozi wa nchi kuishi kama mapedeshee wanavyoishi hapa Bongo kazi yao ni kuwinda wanawake mstaa na kushinda club.
 
Rudia tena kuisoma hii thread usisome kama gazeti la udaku mkuu!
Kinachotajwa hapo ni Ikulu!

Mkuu, nimekupata vipi na ile habari ya Tido Muhando, kuwa boss wa El Jazzira ilishia wapi?

Kama ni kweli huu utakuwa ni ufisadi mwingine kaufanya JK na kundi lake..

Uchumi unazidi kushuka Tanzania shilingi kila kukicha inazidi kuanguka
 
kuna zile leadership attributes... sijui wenzetu hawa wanajua kama zipo?
 
Mkuu, nimekupata vipi na ile habari ya Tido Muhando, kuwa boss wa El Jazzira ilishia wapi?

Kama ni kweli huu utakuwa ni ufisadi mwingine kaufanya JK na kundi lake..

Uchumi unazidi kushuka Tanzania shilingi kila kukicha inazidi kuanguka
Ngoja niwasilia na huko nitajua ila kulikuwa na mpango wakuzima jamaa asipewe hilo shavu
 
2015 bora ifike...Atleast marais waliopita walikuwa hawana mambo kama haya..big up kwa mzee ben & hassan.
 
Kama mtu kamfanyia hivi hili ni jambo baya sana katika mitandao yetu ya kijamii.Usalama wa Taifa wako wapi?
 
Sijui huko mliko ni saa ngapi lakini mkiamka naomba umwambie Mzee kuwa huku hali mbaya, ajali jana imeua karibuni na 30 raia, arusha sukari ni kwa foleni tena ulipie bank. Atume pole japo kwa twitter..
Mpe pole ya starehe
 
Yule Salva wa kwenye Twitter ndiye huyu huyu wa Ikulu au ni fake ID mtu kaifanya? maana kama ni kweli ni hatari kubwa mno...huuh
 
Ikiwa hayo ni ya kweli basi JK uwezo wake wa kufikiri utakuwa umepungua sana, na kibaya zaidi wapambe wake nao watakuwa wamelevywa na starehe wakasahau kumshauri JK mambo yaliyo sahihi kabisa.

je kama hasikilizi shauri lenu mtafanya nini zaidi ya kuendeleza uvivu wake..
 
Yule Salva wa kwenye Twitter ndiye huyu huyu wa Ikulu au ni fake ID mtu kaifanya? maana kama ni kweli ni hatari kubwa mno...huuh
Kwa mawazo mgando niliyoyaona kule Twitter kama ni yeye Ikulu inabidi iombewe sana hali ibadilike, ikibidi hata kuwaombea vifo wafe ili Mungu atupe machaguo mengine.
 
Kwa mawazo mgando niliyoyaona kule Twitter kama ni yeye Ikulu inabidi iombewe sana hali ibadilike, ikibidi hata kuwaombea vifo wafe ili Mungu atupe machaguo mengine.

Mimi nahisi sio yeye; mtu anataka kumchafua ndio akatengeneza ile ID. Sitaki kuamini kama Ikulu yetu ina wasemaje wenye mawazo kama yale!
 
Yule Salva wa kwenye Twitter ndiye huyu huyu wa Ikulu au ni fake ID mtu kaifanya? maana kama ni kweli ni hatari kubwa mno...huuh
Ni yeye mkuu! Alivyo mshamba juzi kati watu wame haki account yake basi jana ameng'aka kama demu
 
Nimeamka leo asubuhi nikaingia kwenye ukurasa wangu wa tweeter, wakati naperuzi kidogo nikakuta tweet ya Salva Rweyemamu Ikiwa imeandikwa kama nilivyoonyesha hapo juu. Mi sijui sana kwanini maana haikuwa na maelezo zaidi labda mwenye kujua reason can tell me please nilikuwa sipo online jamani.................
 
Back
Top Bottom