Salt Soil remediation

Kiresua

JF-Expert Member
May 13, 2009
1,184
259
Wana JF wenzangu,

Mkoani Morogoro kumekuwa na tatizo kubwa la chumvi kwenye udongo, hii imeathirii kwa kiasi kikubwa ujenzi wa nyumba mkoani humo! Nyumba nyingi zimeathirika na hasa ikizingwatiwa kuwa watz wengi ni common wanachi ambao kipato chao ni kidogo nikiwemo mimi!. Tembea meneo mengi ya Mkoa wa Morogoro nyumba nyingi zimeathirika kwa viwango tofauti.

Ujenzi mkoani humo uhitaji umakini wa hali ya juu ili kukabiliana na tatizo hili, (nyumba kulika na hatimaye kuanguka). Kilicho nisukuma kuanzisha uzu huu niwakazi wengi wa mkoani humo kujenga nyumba bila kuzingatia tatizo hili na hata wasomi wanakumbwa na tatizo hili, ingawa wengine wanatumia Mawe cement maalum nk.

Je kuna namna yeyote rahisi au ya gharama ya kukabiliana na shida hii?

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom