Elections 2010 Salma: Ushindi wa Kikwete 2010 haukuwa na dosari

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,019
2,923
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Salma Kikwete, amesema ushindi wa Kikwete katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana hauna dosari kama baadhi ya vyama vya siasa vinavyotangaza.

Alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki alipokuwa akizungumza na wanachama wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Dodoma kwa nia ya kuwashukuru kwa kazi kubwa waliyoifanya wakati wa kampeni ya Uchaguzi Mkuu mwaka jana.

Mama Salma alisema baadhi ya vyama vimekuwa vikitawanya maneno ya uwongo na kuulazimisha ulimwengu uamini kuwa walishinda katika uchaguzi mwaka jana.

"Wanataka waiambie dunia kuwa wao ndio walioshinda, hivi walioshinda wana asilimia 20,"alihoji Mama Salma huku akishangiliwa na wanawake waliofurika kwenye ukumbi huo.

Alisema watu wanaoeneza uongo huo wanashangaza kwa kuwa tofauti ya kura kati ya CCM na vyama vingine ilikuwa kubwa sana.

Alibainisha kuwa uongo unaoenezwa na wapinzani umekuwa ukiwachochea wananchi kukichukia CCM wakati ukweli ni kuwa CCM ndiyo iliyoshinda uchaguzi huo.

Alisema wengi wanaoshiriki katika uzushi huo ni watoto wao kwani wamebebwa na wao migongoni lakini sasa wanawazunguka kuwachafua.

"Wasione simba kalowa wakafikiri ni paka akitoa makucha yake watakiona" alisema.

Aliitaka Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT), kutokuwa wanyonge kukemea mambo yanayofanywa na baadhi ya vyama vya siasa dhidi ya Chama cha Mapinduzi(CCM).

Alisema UWT ni moja kati ya Jumiya ya CCM hivyo ina haki ya kulaani kauli zinazotolewa na Vyama hivyo.

"Msiitegemee serikali peke yake kukemea haya hata nyie mnanafasi kubwa kwani serikali ni kila mtu,"alisema

Alieleza kuwa siasa za chuki zinazoendeshwa na baadhi ya vyama vya siasa hapa nchini dhidi ya CCM ni tabia ambayo haipaswi kuachwa bila kukemewa.

Alifafanua kuwa CCM haiwezi kupoteza muda kulumbana bali itatumia muda huo kujadili mikakati yake iliyojiwekea katika mkutano mkuu uliofanyika mwaka jana.

Aidha, alisema ili jumuiya hiyo iweze kuendelea kuwa imara inahitaji kuwa na damu mpya ambayo ni vijana wasomi.

Alisema nia si kuwaoondoa wanachama ambao ni wakongwe bali ni kuweka mchanganyiko ambao utawezesha kuwepo na kasi mpya.

CHANZO: NIPASHE
 
She's talking the obvious! Sikuweza kuwaza angeongea tofauti, wakati mwingine huyu mama akae kimya....Tutajua anabusara
 
we ulitegeme angesema wamechakachua, kwani yeye ni mwehu? Lakini cha msingi ni bora asingeliongelea hiyo issue, wenyewe wangeongelea habari zao za viduku tu.
 
CCM haiwezi kupoteza muda kulumbana bali itatumia muda huo kujadili mikakati yake iliyojiwekea katika mkutano mkuu uliofanyika mwaka jana.

"UWT ni moja kati ya Jumiya ya CCM hivyo ina haki ya kulaani kauli zinazotolewa na Vyama hivyo."

"Msiitegemee serikali peke yake kukemea haya hata nyie mnanafasi kubwa kwani serikali ni kila mtu,"

Naona hapa mama kajicontradict sana. Kama chama hakipotezi muda basi madhumuni ya hii hotuba ilikua nini? Kama chama hakilumbani anaomba UWT ijibu nini? Serikali ya CCM ina haja gani tena ya kukemea?Ingekua busara angeiga tabia za first lady wengine na kuto kujihusisha na busara bali kukazania zaidi kazi za jamii. Maana naona mama anazidi kuwa mwanasiasa na yeye kadri siku zinavyo kwenda.
 
Alibainisha kuwa uongo unaoenezwa na wapinzani umekuwa ukiwachochea wananchi kukichukia CCM wakati ukweli ni kuwa CCM ndiyo iliyoshinda uchaguzi huo.
Hii ni contradiction. Kama kweli wananchi wengi walimpigia kura Kikwete, itakuwaje leo maneno hayo ya uongo wa Chadema yawafanye wapenzi wa CCM waliompigia kura Kikwete kukichukia chama chao?
 
Hii ni contradiction. Kama kweli wananchi wengi walimpigia kura Kikwete, itakuwaje leo maneno hayo ya uongo wa Chadema yawafanye wapenzi wa CCM waliompigia kura Kikwete kukichukia chama chao?

Hapo mimi ndio nachoka kabisa.
 
Mama Salma alisema baadhi ya vyama vimekuwa vikitawanya maneno ya uwongo na kuulazimisha ulimwengu uamini kuwa walishinda katika uchaguzi mwaka jana.[/SIZE]"Msiitegemee serikali peke yake kukemea haya hata nyie mnanafasi kubwa kwani serikali ni kila mtu,"alisema
DUH! Hapo kwenye bold panatia mashaka. Huyu mama vipi huyu, yaani hajui hata serikali ni nini?? Serikali hajawahi na hatawahi kuwa kila mtu. Wanamwandalia hotuba naomba wamhimize awe anasoma alichoandikiwa tu vinginevyo atakuwa anaamwaga upupu unaomdhalilisha
 
UWT nadhani inapaswa kubadilishwa abbreviatons zake kama ilivo kwa bendera ya ccm (alama ya jembe na nyundo). kama wanamaanisha umoja wa wanawake wa ccm tanzania where does uwt comes/stands. naamini wanawake wote tz ya leo c wana ccm neither do they support it.
 
"UWT ni moja kati ya Jumiya ya CCM hivyo ina haki ya kulaani kauli zinazotolewa na Vyama hivyo."

"Msiitegemee serikali peke yake kukemea haya hata nyie mnanafasi kubwa kwani serikali ni kila mtu,"

Naona hapa mama kajicontradict sana. Kama chama hakipotezi muda basi madhumuni ya hii hotuba ilikua nini? Kama chama hakilumbani anaomba UWT ijibu nini? Serikali ya CCM ina haja gani tena ya kukemea?Ingekua busara angeiga tabia za first lady wengine na kuto kujihusisha na busara bali kukazania zaidi kazi za jamii. Maana naona mama anazidi kuwa mwanasiasa na yeye kadri siku zinavyo kwenda.

Elimu yake jamani mwacheni tu na hakutegemea kuukwaa ufalme ila atajua moto wakati umeish ufalme huo na CCM ni chama cha Upinzani .Waache tu hawa
 
Huyu mama anaongea asichokijua, na pia anakijua bali asema vile kwa kuwa Kikwete na yeye ni mtu mmoja katika nafsi mbili.
Aache Longolongo.

Mme wake katumia helkopta za Barrick kwenye kampeni na sasa analipa fadhila kwa wawekezaji wetu hawa kwa kutuulia ndugu zetu.
 
Hii ni contradiction. Kama kweli wananchi wengi walimpigia kura Kikwete, itakuwaje leo maneno hayo ya uongo wa Chadema yawafanye wapenzi wa CCM waliompigia kura Kikwete kukichukia chama chao?

Hapa ndo tunapopata wasiwasi, na ndipo uwezo wake finyu wa kufikiri unapojionesha wazi.... Ni bora angekaa kimya tu kuliko kuudhihirishia umma jinsi alivyo mbumbumbu!! Itawezekana vipi mtu ambaye alimchagua kwa kura yake leo aje kumchukia kwa kuambiwa tu, haiingii akilini kabisa!!
 
Mama gani asiye na huruma. Mimi najua wanawake ni watu wenye mioyo ya huruma naturally, sasa huyu asiyejua matatizo ya watz katoka wapi, nawashangaa hao waliokuwa wakimsikiliza na kumpigia makofi. Ndi hao wakipewa doti ya khanga wanapoteza network
 
Back
Top Bottom