Salim Kikeke..............@ BBC

rajoh

Senior Member
Jun 2, 2011
174
142
Wadau, mimi ni mpenzi wa kipindi cha habari kinachorushwa na BBC kuanzia saa 3 kamili usiku kupitia Star TV. licha ya habari moto moto ambazo unazipata, pia kuna huyu mtangazaji anayeitwa Salim Kikeke.. Kifupi, jamaa ni jembe sana. Huwezi kuchoka ukiwa unamsikiliza au kumwangalia anavyotangaza.

Nimegundua licha ya technolojia waliyonayo BBC, lakini ubunifu unahusika kwa kiwango kikubwa sana, kumfanya mtazamaji au msikilizaji aweze kuendelea kufatilia matangazo. Kwa watangazaji wa hapa bongo, ni vipindi vichache sana ambavyo unaweza kuvutika kiasi hicho. Mfano, hata kama unaangalia taarifa ya habari kwenye kituo flan cha television au redio, ni vigumu kuitazama yote katika shauku ileile mpaka taarifa yote iishe.

Nadhani, watangazaji wetu wa bongo, wanapaswa kuwa wabunifu katika vipindi vyao ili viweze kuvutia na kuwa vya kimataifa pia. Nakiri kuwa vipo vipindi vichache vizuri lakini vingi bado havikidhi haja ya kimataifa.

Ni mtazamo tu binafsi!
 
Kisa na mkasa na salim kikeke huwezi kufananisha na habari nyepesi za Radio 1.
 
kile kipindi huwa kinaisha wakati mimi bado ninahamunacho,ndio maana siishi kukifuatilia.!
 
Wadau, mimi ni mpenzi wa kipindi cha habari kinachorushwa na BBC kuanzia saa 3 kamili usiku kupitia Star TV. licha ya habari moto moto ambazo unazipata, pia kuna huyu mtangazaji anayeitwa Salim Kikeke.. Kifupi, jamaa ni jembe sana. Huwezi kuchoka ukiwa unamsikiliza au kumwangalia anavyotangaza.

Nimegundua licha ya technolojia waliyonayo BBC, lakini ubunifu unahusika kwa kiwango kikubwa sana, kumfanya mtazamaji au msikilizaji aweze kuendelea kufatilia matangazo. Kwa watangazaji wa hapa bongo, ni vipindi vichache sana ambavyo unaweza kuvutika kiasi hicho. Mfano, hata kama unaangalia taarifa ya habari kwenye kituo flan cha television au redio, ni vigumu kuitazama yote katika shauku ileile mpaka taarifa yote iishe.

Nadhani, watangazaji wetu wa bongo, wanapaswa kuwa wabunifu katika vipindi vyao ili viweze kuvutia na kuwa vya kimataifa pia. Nakiri kuwa vipo vipindi vichache vizuri lakini vingi bado havikidhi haja ya kimataifa.

Ni mtazamo tu binafsi!

Hebu nijuze, wewe ni 'Me' au 'Ke'? Usiwe na jazba ya kina Ponda nijibu nijue maana huwezi kuwa na hamu ya kumuangalia mtu namna hiyo!
 
unataka 'Me" awe na hamu ya kumwangalia 'Ke" and viseversa? mimi ni 'Me" bana. Sidhan kama, wapenzi wengi wa Simba au Yanga ni 'Ke" kuliko 'Me' kwa kuzingati mtazamo wako hapo juu!
 
Vile vile, tunapowatambua wanaofanya vizuri, tusisahau na kuwachagiza na wale ambao bado wana boronga. Erick David Nampesya ni mtangazaji wa BBC ambayo angeweza kuwa mzuri pia kama angeacha kutumiwa kama chombo cha propaganda.
 
Jamaa naye si haba! Hivi Flora Nducha yuko wapi siku hizi?
 
Sasa jamani mtamfananisha KIKEKE na watangazaji wetu wanaotokea hapo DSJ? au wengine unaambiwa wanavipaji vya kuzaliwa hata shule ya habari hawajaenda.
 
Hilo la vipaji vya kuzaliwa huwa nashindwa kulielewa vizuri. Mimi nadhani vipaji ni sawa lakini shule muhimu!
 
Kwa wenzako shule sio sawa vipaji ndio vyenyewe, jaribu kuchunguza utajua kuwa baadhi ya watangazaji wetu wengine walikuwa wanafanya kazi kwenye promosheni wanazungukua na zile fuso za matangazo wakitoka hapo wanaingia Radio, huwa najiuliza mtu kama Zembwela alisomea wapi uandishi wa habari, jamaa yangu akaniambia Zembwela alikuwa anaalikwa na Musa katika kipindi chake radioni coz Zembwela anajua mambo mengi ya uswahilini na Musa alipoondoka EA R/T wakaona Zembwela ndio anafaa akala ajira, simple like that.......sasa tegemea umahiri kama wa KIKEKE.
 
Mbona hamsemi wa tbc1? Au wamekufa?

TBC1 marine Hassan naona kama vile amepoteza umaarufu baada ya kuacha kutangaza habari za kutoka kwenye matukio. Kuna jamaa mmoja alikuwa anatangaza michezo anaitwa Pendael, sijui yuko wapi siku hizi. Jerry mulo amepewa kipindi flan siku hizi hapo TBC1, hakikunivutia kivile....
 
Afu kuna jembe jingine linaitwa Lubunga Byaombe..... acha kabisa!

Ha ha ha ha ha ha.... kongoman hilo jembe.. Kiswahili kibovu lakini utamu unaupata. Jembe Charles Hillary kwenye kutangaza mpira... duh! kama vile uko uwanjani..
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom