Salha Israel ashinda taji la Vodacom Miss Tanzania

jamii01

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,974
1,400
8318.jpg
Vodacom miss Tanzania Salha israel(katikati) akiwa na mshindi wa pili Tracy Sospeter(kulia) na mshindi wa tatu Alexia William mara baada ya kutangazwa usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa mlimani city jijini Dar es salaam.
BAADA ya kuwabwaga wenzake 29 na kuibuka na taji la Miss Tanzania 2011, katika kinyanganyiro kilichofanyika usiku wa kuamkia jana kwenye ukumbi wa Mlimani City, mrembo kutoka Kanda ya Ilala, Salha Israel (18), amejinyakulia zawadi zenye thamani ya Tsh. 80 M.

Salha amekuwa mrembo wa kihistoria Tanzania kwa kuzawadiwa zawadi zenye thamani kubwa ambayo ni gari mpya kabisa model ya kisasa ya mwaka huu aina ya Jeep Patriot yenye thamani ya shs. Milioni 72 na fedha taslimu sh. Milioni 8.

Hii ni zawadi kubwa kabisa kwa miaka 18 ya urembo ambayo imevunja rekodi ya mwaka 2003 ya Sylvia Bahame ambaye alizawadiwa gari aina ya Nissan Hardbody yenye thamani ya shs milioni 55 na fedha taslimu shs. 7 million.

Haikuwa rahisi kwa Salha ambaye pia ni Miss Ilala kushinda nafasi hiyo ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia (Miss World) yaliyopangwa kufanyika nchini London kutokana na ushindani uliokuwa wa karibu dhidi ya warembo wengine.

Salha ambaye anatokea kituo cha Miss Dar City Centre, alikuwa na wakati mgumu sana kutokana na kushindana kwa karibu zaidi na warembo wengine watatu kutoka kanda ya Ilala na kituo chao.


Ushindani ulikuwa mkubwa sana, nashukuru kwa kupata taji hili, siamini lakini, namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kupata taji hili,alisema Salha huku mabaunsa wakizuia kufanya naye mahojiano.

Tracy Sospeter aliyekuwa akiuwakilisha mkoa wa Shinyanga alishika nafasi ya pili na mrembo wa Kanda ya Ilala tena, Alexia Williams akiibuka katika nafasi ya tatu.

Jennifer Kakolaki wa Ilala tena aliibuka kuwa wa nne huku mkoa wa Lindi kupitia Lovennes Flavian ukiibuka kuwa wa tano.

Tracy alipewa kitita cha sh. Milioni 6.2 kwa mshindi wa pili,Alexia alipewa sh. 4 millioni kwa mshindi wa tatu. Jeniffer aliibuka na sh. Milioni 3 kwa mshindi wane huku Loveness akipewa sh. Milioni 2.4 kwa ushindi wa tano.

 
Ndugu zangu, naomba kutoa angalizo kuhusu haya mashindano ya Miss Tanzania. Ikumbukwe kuwa hayo mashindano yameendeshwa wakati wenzetu Wazanzibari wamekumbwa na msiba uliotamkwa kuwa wa kitaifa na viongozi wa nchi hii kutangaza siku tatu za maombolezo. Kwa kuwa waandaji wakiongozwa na Hashim Lundenga na timu yake ya Mafia na wadhamini wakiongozwa na Vodacom wamepuuzia haya yaliyojiri, naomba kutoa hoja kuwa Watanzania wayalaani haya mashindano na kuyasusia mpaka atakapopatikana mtu mwingine wa kuyaandaa. Aidha BASATA waone busara kumsimamisha Lundenga kuanzia sasa. Vilevile huyo mrembo aliyepatikana jana asitishwe kuhudhuria hayo mashindano ya Miss World kama mfano kwa wakaidi wanaopuuzia maswala nyeti ya kitaifa!! Naomba kuwasilisha!!
 
Back
Top Bottom