Salender Bridge 3Hrs breakdown with Police ...ni Operation Zimamoto ama ??

Davie S.M

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
748
228
Jana saa sita Usiku,
Sina hili wala lile nipo na ki-Baby walker(gari) ya bwana mdogo narudi Kijitonyama Kati Kati ya Daraja ikazima nikajivuta hadi mwisho wa Daraja ikazima kabisaaa...sasa jasho lantoka sijui nini shida nikaweka shoto nikiwa na Hofu tele..Maana ni Sehemu Hatari pale,
Nampigia kijana anipe tabia ya gari yake ananiambia Gauge mbovu Possibly mafuta yameisha au imeoverHeat na Mimi nimekuwa nikilazimisha hadi nimeua Battery
Upande wa Pili kituo cha bus naona PickUp 2.5 imepaki nafikir nao wana shida zao...wapo. Na Askari kadhaa..ndio wananipatia Habari za wale Wahindi kuvamiwa na Kupigwa na Kuibiwa,hofu ikazidi.
Baada ya kukosa msaada wa Gari/BAckup kwa 'washkaj' maana simu ilizima na hata hakuna Gari lililo simama kwa Giza lile (hata mimi nisinge simama ),na Presha wa Maafande wanasema wataniacha nikaona doo hatari...sababu nishawah pata pancha mwaka jana pale nikatembea na rim hadi kituoni kwao nikakuta askari wawili na bunduki wanavuta sigara nje wananiambia nina "Bahati" ile sehemu hatari sana..nikashangaa wajibu wao nini ?

Liwalo na Nikaamua nitembee tu,wale askari hawakuwa na Gari/msaada wao ni uwepo wao kulinda kile Kigari...bahati nikapata taxi pale ubalozi wa Ufaransa..nikapata Mafuta pamoja na jumper cable akanisaidia sana.
Sasa nikagundua Leo Baada ya Kuona karibia kila Junction kuna police vijana wawili age 23-27 (wapya Nafikir) wakiwa na SMG zao wameshika Kwa 'mbwembwe'
My Take,
Hatuhitaji izi Operation Zimamoto,sio mpaka tukio Ulimboka Atekwe ndio tuanze kulindwa ni haki yetu tunatakiwa tuwe salama siku zote.Serikali Timizeni Wajibu wenu na sisi tutashiriki pamoja.


Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom