Salamu za Mshikamano kutoka kwa M. M. Mwanakijiji

Majuzi tumepokea salamu za mshikamano kwenye kongamano la wanafunzi lililoitishwa na CHADEMA kutoka kwa mtu anayejiita M.M. Mwanakijiji. Lakini hatukuambiwa kwamba huyu bwana ni nani na ametuma hizi salamu kama nani. Je, iweje chama cha siasa kiruhusu mtu ambaye wameshindwa kumtambulisha alete salamu za mshikamano. Kwenye hizo salamu za MM Mwanakijiji anawahamasisha wanafunzi waafanye uasi, wagome na mambo mengineyo. Sasa hivi hao wanafunzi ni mafala kiasi gani kwa kupokea ujumbe bubu, ambao aliyeuandika ni kunguru asiyejitambulisha?
Yaani kwa haya mawazo yako unayomwaga hapa hivi kweli ni kwa mtu aliyejipenyeza katika mkutanao wa siku ya vyuo vikuu, na isitoshe ni mdau mwenye elimu ya Chuo unatoa hizi pumba hapa? Tena huna aibu kusema siku ya vyuo vikuu, ukimaanisha na wewe ulikua mdau?

Hata kama aliwachochea kugoma, hakuna mbaya kwani dawa ya serikali dhalimu ni nini? Hata mimi nilichelewesha tu salamu zangu, nilitaka nizitume niwahamasishe vijana juu ya umuhimu wa kufanya yale ya BOLIVIA, INDONESIA nk.

Muda uliobaki ni mchache sana, tutafanikiwa tu.

Halafu siku nyingine ukipost hapa usome kabla hujapost ndugu yangu, kwa nini ujikosee heshima namna hiyo?

Mdau wa Chuo Kikuu? Hata common sense ni za muhimu sana.
 
Kwa wana Kongamano la Wanafunzi
Ukumbi wa DDC
17/11/2007
Utangulizi
Napenda kwanza kabisa kutoa shukrani zangu za dhati kuweza kutuma salamu za mshikamano kwenu wanafunzi wa Tanzania katika kuadhimisha siku hii ya Wanafunzi Duniani. Pamoja nanyi bila ya shaka wapo wanataaluma mbalimbali na wazungumzaji wengine mashuhuri ambao kwa hakika mawazo na mchango wao katika mjadala wa siku hii ni vitu vya kuonewa wivu, kutamaniwa na kwa hakika kufurahiwa. Kwenu ninyi nyote naomba nitume salamu hizi kwa niaba ya ndugu zenu, na watanzania wenzenu ambao wametanganishwa nanyi na muda, na geographia wakiwa wametawanyika sehemu mbalimbali duniani. Tuko pamoja nanyi katika wakati huu wa pekee katika historia ya nchi yetu. Umbali unaotutenganisha ni wa muda tu, na siku moja Inshallah, tutaonana na kushirikiana katika mapambano haya ya kifikra.

Wakati Huu ni wa Pekee
Wakati huu ni wa pekee kwani haijawahi kutokea katika historia ya nchi yetu ambapo mgongano mkubwa wa mawazo na kifikra unafanyika hadharani, kwa uhuru zaidi na kwa u wazi zaidi huku athari zake zikipiga hodi kuanzia vijijini hadi mijini na mlio wake kusikika kuanzia kwenye mashamba ya mikorosho huko Mtwara na vichuguu vya mawe kandokando mwa Ziwa Viktoria. Tuko kwenye kipindi cha mabadiliko makubwa ambapo kama mama mzazi mwenye utungu wa mwanae ndivyo hivyo tunavyotamani kuona nini kitazaliwa kutoka katika uchungu huu! Miezi ya kusubiri mwana imepita, na sasa tunakaa sawa kumkaribisha mtoto katika familia yetu!

Watanzania walipoichagua serikali ya awamu ya nne walifanya hivyo wakiwa wamejawa imani na matumaini kuwa hatimaye kidonda kimepata tiba na Taifa limepata uongozi. Leo hii katika kona mbalimbali za nchi yetu watu wanapita na kutikisa vichwa vyao kwa masikitiko kuwa waliyemdhania ndiye kumbe siye. Leo watu wameanza kukata tamaa na viongozi wao, leo watu wameanza kuangalia nyuma na kusema “kumbe ni wale wale”. Leo hii wanavyolindana huko madarakani, wakimega na kumegeana, waking’ata, huku wengine waking’atana, na wale wanaotafuna wakitafuna kama kwa zamu!

Leo hii kuna wanakijiji wamechomewa nyumba huko Kilosa na Jeshi lao la Magereza kinyume cha sheria; leo hii kuna wanafunzi 400 toka Arusha wanashindwa kuendelea na masomo ya elimu ya juu kwa sababu wenye dhamana ya mikopo wamejiweka kwenye viti vya enzi; na leo hii kuna wadogo zetu pale Azania wameshindwa kuendelea na masomo kwa kugoma sababu ya mazingira machafu yasiyomstahili mwanadamu, na leo hii wameingiza nchi katika mikataba ile mibovu ambayo wote sasa tunaifahamu na kuikariri utadhani aya za vitabu vitakatifu! Matumaini ya wananchi yameanza kuvunjwa na kupondwa na sasa baadhi ya watu wamefikia kuishi kwa ile falsafa ya kibepari kuwa kila mtu na lwake ila Mungu ni wetu sote!

Ndiyo maana basi kufanyika kwa kongamano hili kwa siku kama ya leo na kwa kuangalia mada yake kuu kuwa “Vijana: Nguvu ya Mabadiliko” basi kuna mambo machache ambayo binafsi naomba niyaseme kama mchango wangu wa mawazo.

Mambo matatu
Kwanza, wasomi wetu katika nafasi zao mbalimbali (iwe vyuoni au walio maofisini) wanajukumu kubwa la kuamsha dhamira za utumishi kwa nchi yetu. Binafsi ninaamini kuwa Taifa letu limeangushwa hadi hivi sasa kwa kiasi kikubwa na wasomi wake hasa miaka hii kumi na tano iliyopita. Miaka ya mwanzoni mwa uhuru na hasa ile ya sabini Taifa letu lilishiriki kwa kiwango kikubwa katika kuchambua dhana mbalimbali za kisiasa na kifalsafa kiasi cha kutoa wasomi mahiri wengi tu ambao mchango wao unatambulikana duniani. Wasomi wengi tunaowasikia leo hii ni matunda ya wakati huo. Wengine mnao hapa!

Leo hata hivyo baadhi ya wasomi wetu ambao walikuwa mahiri walipokuwa nje ya madaraka wamekuwa kama wamepigwa ganzi pale walipopata vyeo vya kisiasa na hasa walipoona bendera zinapepea kwenye magari yao na wanapigiwa saluti kila wanakopita. Sauti za “ndiyo mheshimiwa” na “ndiyo mzee” zimewalesha ugimbi wa madaraka! Leo hii tuliowadhania kuwa watakuwa chachu kwenye uongozi wamebakia kuwa kama alama za barabarani zilizofutika! Na wachache ambao wanaujasiri wa kwenda kinyume na mazoea mabovu wanaonekana ni majasiri kati yao! Ni lazima wasomi wetu waamshe dhamira ya utumishi ndani yao wenyewe na ndani ya wale wote wanaopata nafasi ya kusikia maoni yao na kuona matendo yao!

Pili, Ni jukumu la wasomi kuongoza mazoea ya kukataa sera mbovu, mazoea mabovu, na utendaji mbovu bila kuuonea haya au kuufumbia macho. Mwanzoni mwa wiki hii bila ya shaka mtakuwa mmesikia vijana wa Azania waliogoma kuingia madarasani kwa sababu vyoo na mazingira wanayosomea ni machafu. Mliopata kuona picha za video bila ya shaka mlijihisi kinyaa na kushangaa hali imefikiaje hapo. What transpired there it’s a metaphor of what is happening in certain quarters in our country! Tumezoea uchafu kiasi cha kwamba tunavaa suti na tai kwenda kwenye vyoo vichafu, tunatilia pafyumu hoteli migahawa michafu, na tunaendesha magari ya kisasa kwenye barabara mbovu! Vijana wa Azania wamefanya kitendo ambacho wengi wetu kwenye vyuo vikuu na taasisi nyingine hatuna ujasiri wa kufanya. Wamekataa kuuzoea uchafu!

Hawa vijana wameonesha kiini cha usomi nacho ni uwezo wa kukataa vitu vilivyozoeleka na uwezo wa kuhoji yanayokubalika kama kawaida. Kwa sababu tunapokataa tunajenga hoja ya kwanini majibu au vilivyopo havitoshi! Ni kukataa mazoea kulikosababisha mapinduzi ya Ufaransa, ni kukataa kulikosababisha mapinduzi ya Marekani, ni kukataa kulikosababisha uhuru wa India, ni kukataa kulikosababisha Martin Luther King Jr kuongoza matembezi ya Selma, Alabama. Ni kukataa kulikosababisha Mapinduzi ya Zanzibar na ni kukataa kulikosababisha Azimio la Arusha! Msingi wa kukataa huku ni imani kuwa mahali fulani kuna tunu zilizobora zaidi na mahali fulani kuna mawazo yenye mantiki zaidi! Leo hii wanapofukuza wanafunzi wa vyuo vikuu na wanafunzi wale wanapiga magoti kwa woga wakiyupa wasamehewe huku wanajua kabisa haki na sheria iko upande wao!

Katika hili niwatambue vijana wetu 29 waliokuwa wamekwama Ukraine na ambao serikali yao iliwatelekeza mchana kweupe. Vijana wale walikuwa na uwezo wa kukubali makosa na kuamua kuyamaliza chini chini. Walikuwa na uchaguzi wa kusema walikosea kujaza fomu na yakuwa walijiondokea kivyao vyao. Hadi wanarudishwa nyumbani hakuna hata mmoja wao aliyekubali makosa ya kutungiwa na aliyekuwa tayari kupiga magoti mbele ya watawala na kusema walisema uongo! Vijana wale wamerudishwa nyumbani kwa sababu hakukuwa na jinsi nyingine; lakini wamerudi wakiwa na heshima yao na dhamira zao zikiwa safi! Wakati watu walidhania suala la vijana hawa lilikuwa ni makosa yao leo mambo yale yale yanasikika Arusha, Dodoma, Dar na hata Urusi, China, India na Cuba ambapo wanafunzi wa Kitanzania wanapata matatizo yanayotokana na bodi mbovu isiyowajibika ya mikopo. Naomba niwapongeze vijana wale kwa moyo wao wa mfano na wale wote waliojitokeza kuwasaidia. Historia itawahukumu vizuri siku moja.

Tatu na mwisho, sisi sote tunao wito katika kuleta mabadiliko tunayoyatamania. Tumesema kuwa “Vijana: Nguvu ya Mabadiliko”. Naamini kabisa kuwa mabadiliko ya kweli katika nchi hii hayatatokea kwanza kwa kubadili Katiba, au kwa kubadili sheria au kwa kuunda tume teule na tume tukufu! Mabadiliko ya kweli hatatokea kwa kubadili mawaziri na kuongeza wajumbe kwenye kamati juu ya kamati. Na anayedhania kuwa mabadiliko ya kweli yatatokea kwa kuibembeleza serikali ajue amekosea sana. Ndugu zangu, mabadiliko ya kweli ni lazima yaanzie kwenye fikra! Hatutaweza kushinda kwenye sanduku la kura, kama tutashindwa kwenye uwanja wa fikra!

Ndiyo maana ninachokiona kinaendelea Tanzania hivi sasa siyo mgogoro wa kisheria, siyo mgogoro wa kikatiba, na siyo mgogoro wa vyama. Naamini kinachoendelea ni mgogoro wa kifikra, ni mapambano ya kifikra. Mwalimu Nyerere katika ile hotuba yake ya Mei Mosi Uwanja wa Sokoine kule Mbeya aliliona hilo. Na alitambua kuwa tusipokaa chini na kubadili mweleko wa fikra zetu tutajikuta tumepelekwa tusikotaka kwenda na tusijue tumefikaje huko. Leo hii watu kama kina Prof. Shivji anapozungumzia Azimio la Arusha kwa mfano kuna watu wanatetemeka kwa sababu wanakumbushwa enzi za “Mabepari walia kunyang’anywa mirija”. Hakuna kitu kinachowatishia wanyonyaji mambo leo kama mawazo ya msingi ya Azimio la Arusha na hapa sizungumzii utaifishwaji wa mali za umma. Leo hii hatuna mwelekeo wa kiitikadi ambao unaeleweka tunaendelea kuburuzwa tu kwa kufuata nguvu za soko! Mwalimu alitabiri kwa usahihi kabisa kuwa mambo waliyokuwa wameanza kuyafanya baada ya Azimio la Zanzibar “yatatengeza mamilionea wachache, lakini yatatengeneza masikini wengi”.

Hitimisho
Ndugu zangu wasomi! Mnao wito kwa Taifa letu, wito wa kuamsha fikra za wananchi kuukata ufisadi, kukataa kubebana, kukataa rushwa, kukataa viongozi wababe na kukataa sera za kibaguzi! Ni lazima sisi sote tuweze kuzishinda fikra mbovu na hoja za kitoto kwa kupendekeza fikra bora zaidi na hoja zenye nguvu zaidi! Kabla watawala wetu hawajaanguka kwenye sanduku la kura, ni lazima waanguke kwenye fikra za wananchi wao. Ndiyo ni lazima waanguke huko kwanza. Miezi michache iliyopita imeonesha mwanzo wa mabadiliko haya ya kifikra. Basi mtokapo hapa leo hii, cheche ya mwamko mpya wa mapenzi kwa nchi yenu iwashwe, na mwenge wa moto umulikao wa uzalendo uwake mioyoni mwenu ili siyo tu uangaze pale mlipo nyinyi bali uwaangazie hata ndugu zenu ambao hawajapata au hawatopata nafasi ya kutembelea taasisi zenu za elimu ya juu. Kama wanakijiji wa Buzwagi wameweza nanyi mnaweza; kama wanakijiji Dodoma wameweza nanyi mnaweza, kama wadogo zenu wa Azania wameweza nanyi mnaweza, wakati umefika na nyinyi muoneshe siyo tu mnaweza bali mnayo sababu, uwezo, na nia ya kuweza. Vinginevyo na nyinyi mtabakia kuwa irrelevant, na wananchi watasubiri kizazi kijacho cha wasomi; and my friends, that will be a tradegy for our country, please answer this historic call to duty! Nawatakia kongamano jema!

Ndugu yenu,
M. M. M.
 
Umetumia mfano wa mgomo wa Wanafunzi wa Azania hivi majuzi na kudai kwamba usomi wao ndiyo umewafanya "wakatae" uchafu wa mazingira iliyopo shuleni. Sasa mtu unaweza kujiuliza, jee huo uchafu umeletwa au kutupwa hapo shuleni na serikali au labda Al Qaeda? Ni nani au ni nini chanzo cha mazingira machafu shule ya Azania? Pili jee kila kitu kinataka pesa na direct involvement ya serikali kuu kama usafi wa vyoo na mabweni wanayotumia Wanafunzi wenyewe? Imekuwa tabia kulaumu serikali kwa kila mapungufu na maovu ambayo watu wanaweza kuyamudu kiurahisi kwa kutumia freely available resources and joint efforts.
 
Ukiangalia utaona kuna majibu ndani ya swali lako:

a. Katika mada yangu sikuilamu serikali (not directly anyway) kuhusu uchafu wa vyoo Azania, bali wale wanaowajibika kusimamia usafi maeneo hayo. Endapo walimu na utawala wa shule unavumilia uchafu kwa wanafunzi hilo ni suala la serikali. Tuliwahi kuwa na mabwana afya huko nyuma hivi sasa wako wapi? Kimsingi vitu vya jumuiya vinasimamiwa na jumuiya; binafsi nisingetoa mfano kama uchafu huo wa vyoo ungekuwa nyumbani kwa mwanafunzi au mwalimu.

b. Serikali inayo majukumu ya kutengeneza sera nzuri na zinazotekelekezeka. Kama ni wao wanaosimamia ujensi wa madarasa na kuajiri walimu, kwanini wasiwajibike katika ujenzi wa vyoo bora na safi? Kwa vile watawala wetu wanaona kuwa ni bora kuwa na madarasa mengi na wanafunzi wengi bila kuwa na vyoo vizuri na vyenye kutosha basi tunamatatizo.

Kuna mambo ambayo kwa hakika uongozi wa shule (ambapo kuna "wasomi") ungeyafanyia kazi. Kama ulifuatilia jibu la mkuu wa shule wa Azania ni kuwa suala la vyoo "limefikia ngazi ya Wizara ambako linashughulikiwa". Sasa kwanini tusitolee mfano Azania?
 
Kusema kweli sioni kama jibu lako linaridhisha. Wajibu wa usafi katika shule ni 95% wajibu wa wanafunzi wenyewe. Mavi chooni wajaze wenyewe halafu lawama waipelekee serikali? Kama vyoo vikiziba ingebidi wachimbe vyoo vipya vya mashimo kutumia majembe na zana nyinginezo za kawaida halafu waezeke kwa makuti. Kwa vyovyote huwezi kutegemea tip-top facilities wakati shule ni mali ya serikali na ada ni ndogo sana na ni sawa na bure. Dawa ni kufuta mtihani wa std 7 na kubinafsisha shule zote za serikali.
 
Crtical and logical Thinking nimuhimu.

Tatizo siyo uchafu unazalishwa na nani bali ni uwiano wa Idadi ya Vyoo na wanafunzi. Haihitaji kuuona mlango wa darasa la kwanza kufahamu kuwa uwiano usipokuwa sawa, sanitary facilities zitakuwa strained na hygiene itaenda chini. Je ni wajibu wa wanafunzi kujenga vyoo? Nani Kiranja mkuu wa Elimu kama siyo wizara ya Elimu? Mbona Waziri wa Elimu akitoa tamko" Magazeti yanaandika serikali imesema" lakini inapofikia kwenye Vitu wanavyoboronga wanataka kunawa mikono" Inachekesha sana hawa wanaongoza serikali (Chama Twawala) huvamia hata mambo yasiyo na maslahi direct kwa Watanzania kama " Mshindi wa BBA ni zao la makuzi ya Serikali iliyo chini ya sisiem" Inasikitisha kwa kweli.

" The mind is like stomach.It is not how much you put into it that counts, but how much it digests"
 
Halafu ukishafanya hivyo ndio inakuwaje..?
 
Kamanyola,
sentensi kama hii"Kama vyoo vikiziba ingebidi wachimbe vyoo vipya vya mashimo kutumia majembe na zana nyinginezo za kawaida halafu waezeke kwa makuti" siamini kama inatolewa na mtanzania wa karne ya 21. Watu wanakimbia, lakini wewe unataka turudi kwenye Ujima. Serikali imefanya mikataba mingi sana ambayo ni Bogus and Poor Tanzanians are paying the price.

Mimi naunga mkono hoja ya kukataa ufisadi,udikteta na mambo mengi ya kubaka UCHUMI wa Taifa. Hatuwezi kuendelea kuruhusu mama zetu(Wajawazito)kufa wakati wa kujifungua wakati Vascodagama anaendelea kuvumbua nchi za Ulaya karne ya 21"
Bravo Mkjj.
 
Ndio maana hawataki tuzungumzie ubovu wao na maamuzi yao ya kijima. Unaweza vipi kununua dege la bilioni 50 wakati unashindwa kutengeneza choo japo cha matofali ya kuchoma? na saruji mnayo vigae mnavyo n.k? Wanataka tuwasifie wanapofanya makuu lakini wanapoboronga madogo "wananawa mikono".
 
Majuzi tumepokea salamu za mshikamano kwenye kongamano la wanafunzi lililoitishwa na CHADEMA kutoka kwa mtu anayejiita M.M. Mwanakijiji. Lakini hatukuambiwa kwamba huyu bwana ni nani na ametuma hizi salamu kama nani. Je, iweje chama cha siasa kiruhusu mtu ambaye wameshindwa kumtambulisha alete salamu za mshikamano. Kwenye hizo salamu za MM Mwanakijiji anawahamasisha wanafunzi waafanye uasi, wagome na mambo mengineyo. Sasa hivi hao wanafunzi ni mafala kiasi gani kwa kupokea ujumbe bubu, ambao aliyeuandika ni kunguru asiyejitambulisha?
Shetani:

Usimfitinishe mwanakijiji. Mimi ndiye niliyemuomba aandike ujumbe wa ajili ya kuusambaza kwa wanavyuo siku ile. Kongamano halikuwa la wasomi wa CHADEMA tu, likuwa la wasomi wote bila kujali itikadi. Nilimwomba mwanakijiji aandike kwa kufahamu uwezo wake wa kiuandishi na mchango wake mkubwa katika mapambano ya fikra bila kujali itikadi.

Na ujumbe wake, pamoja na kuwa ulikuwa mrefu nilitamani sana usomwe siku ile ndio maana katika ratiba niliweka salam za mshikamano. Na ningetambulisha mwandishi wa ujumbe kabla ya kusomwa. Ni wazi, ningesema ujumbe unatoka kwa kijana mwenzenu wa kitanzania aliyoko ughaibuni ambaye nimemwomba atoe mchango wake katika mapambano hayo ya fikra ambayo yako juu ya itikadi. Kwa bahati mbaya, watu walichelewa kidogo kufika, tukachelewa kuanza hivyo salam za mshikamano toka kwa wageni wasio wanavyuo hazikuwasilishwa. Ilibidi ujumbe wake usambazwe tu kwa washiriki kupatiwa.

Ukweli ni kuwa katika kongamano hilo tulialika watu bila kujali itikadi. Ndio maana nilimwalika pia Makwaia wa Kuhenga ambaye ni kada mkubwa wa CCM kama mmoja wa wajadilifu(discussant) na alifika na kutoa mada yake. Nilimwalika pia Dr Azaveli Lwaitama(huyu si mwanachama wa chama chochote) alikuja alitoa mada na katika mada yake alikosoa mpaka upinzani. Ni mapambano ya fikra tu haya, mpaka fikra mbadala zitakaposhinda- na ushindi wa fikra mbadala hautakuwa kipeo cha kufikiri-yatandaanza mapambano mengine.

Ni vita kati ya ukweli na uwongo, ukweli ukishinda vitaanza vita vingine kati ya ukweli na kipeo cha juu cha ukweli. Endeleeni kuujadili ujumbe badala ya mjumbe. Chambelecho cha 'simple, ordinary and great minds'.

Natoweka.
J.J.
 
Mugo"The Great";103588 said:
Crtical and logical Thinking nimuhimu.

Tatizo siyo uchafu unazalishwa na nani bali ni uwiano wa Idadi ya Vyoo na wanafunzi. Haihitaji kuuona mlango wa darasa la kwanza kufahamu kuwa uwiano usipokuwa sawa, sanitary facilities zitakuwa strained na hygiene itaenda chini. Je ni wajibu wa wanafunzi kujenga vyoo? Nani Kiranja mkuu wa Elimu kama siyo wizara ya Elimu? Mbona Waziri wa Elimu akitoa tamko" Magazeti yanaandika serikali imesema" lakini inapofikia kwenye Vitu wanavyoboronga wanataka kunawa mikono" Inachekesha sana hawa wanaongoza serikali (Chama Twawala) huvamia hata mambo yasiyo na maslahi direct kwa Watanzania kama " Mshindi wa BBA ni zao la makuzi ya Serikali iliyo chini ya sisiem" Inasikitisha kwa kweli.

" The mind is like stomach.It is not how much you put into it that counts, but how much it digests"

Si unaona jinsi ulivyoishia kuikandia serikali tu licha ya kuanza hoja vyema kwa kugusia sababu za msingi. Nenda Uingereza, Marekani, Ufaransa na kwingineko utakutana na matatizo yakeyale ya uduni wa mazingira kwenye Public Schools likiwemo hilo la uwiano mkubwa kati ya wanafunzi na walimu. Tofauti inakuwa kwamba wenzetu angalau wana desturi bora maradufu kuhusu viwango vya usafi ya mazingira na ukarabati as miundombinu. Waswahili hata uwajengee vyoo vya kisasa vyenye sabuni na maji tele baada ya wiki chache tu wataishia kutupa vinyesi hadi kwenye dari halafu watasingizia halmashauri ya jiji au serikali.
 
personal nimesoma Azania kwa six years, maana kutoka form one mpaka six. Azania ni shule ambayo majority wanatoka kwenye low income family in Tanzania, hivyo imesababisha mikusanyo wa ada (school fee) kuwa mdogo sana. Majority ya wanafunzi hawalipi ada, mimi nilikuwa mmoja wao kwa miaka sita nadhani nimelipa 2 years. sasa basi, sidhani kama swala la vyoo ni haki ya serikali kuu kuoversite hilo.

Sisi Watanzania tumezoea big government, yaani serikali have to put his hand on everything. Swala hilo haliwezekani, what i think is Tanzania need High school fainancing reform, ile kasumba ya 100% ya fund za shule inabidi itoke adhina imeshapitwa na wakati. Each individual school need to operate from student tuitions, while government oversite the whole procidure, and also assist in funding if neccessary. This will help school to enforce tuition payments, and also school will be able to take immediately action when problem like vyoo hapened.

School is like any other organization, inabudget yake ambayo inabidi ifuate ili isirun short, sasa kwa system tuliyonayo sasa inapoteka emergency nilazima uombe pesa wizarani ili kucover tatizo. Ndio maana nilisema tatizo sio la serikali, tatizo ni mfumo mzima wa kusifund shule hizi.

Angalia nchi zilizoendelea jinsi zinavyongoza shule za msingi na high school, mfano US, state inafund partial na school tax inacontribute partial. Pesa yote ile inakwenda kwenye that particular school. Lakini Tanzania sio hivyo, pesa za ada zinakwenda kwanza adhina kisha adhina ndio wagawe kwa shule mbali mbali, matokeo yake ndio shule nyingine zinalemaa kabisa kukusanya ada, mfano Azania.
 
Mugo"The Great";103594 said:
Kamanyola,
sentensi kama hii"Kama vyoo vikiziba ingebidi wachimbe vyoo vipya vya mashimo kutumia majembe na zana nyinginezo za kawaida halafu waezeke kwa makuti" siamini kama inatolewa na mtanzania wa karne ya 21. Watu wanakimbia, lakini wewe unataka turudi kwenye Ujima. Serikali imefanya mikataba mingi sana ambayo ni Bogus and Poor Tanzanians are paying the price.

Mimi naunga mkono hoja ya kukataa ufisadi,udikteta na mambo mengi ya kubaka UCHUMI wa Taifa. Hatuwezi kuendelea kuruhusu mama zetu(Wajawazito)kufa wakati wa kujifungua wakati Vascodagama anaendelea kuvumbua nchi za Ulaya karne ya 21"
Bravo Mkjj.

Nani kasema inabidi ule kwa kutumia kisu na umma ili upate lishe inayotosheleza mwili wako? Ingawa tupo karne ya 21 ukweli ni kwamba kwa Watanzania walio wengi bado mila na desturi zao nyingi zimeelemea kwenye enzi za ujima, zikiwemo zile za usafi binafsi na usafi wa mazingira.

Sasa kuna tatizo gani kama Wanafunzi waliozoea vyoo vya mashimo (pit latrines) wangechimba wenyewe vyoo hivi ambavyo pia havihitaji huduma kubwa ya usafi kama vyoo vya kisasa (water closets) - haswa ukizingatia tatizo sugu la maji?
 
Kumbe tabia ya jitu zima lililomaliza form 4 mwaka '87 inaweza kunyooshwa na vitisho vya kufungiwa...Wow!!
 
Who is the government? Katibu Kata, Katibu Tarafa, mkuu wa wilaya.. ...Wote ni Serikali. Kinacho-lack ni uwajibikaji katika grass-roots level. Kama Headmaster si responsible, mabwana afya wako wapi?

Anyway the Bottom line is, mshikamano wa wasomi katika kuleta mabadiliko katika nchi ni muhimu. Wasomi wana exposure kubwa juu ya nini kinaendelea duniani na wengi wanatokea rural areas. Hivyo ni rahisi kufikisha Ujumbe kwa urahisi juu ya mifumo ya kisiasa, kiuchumi n.k. Suala hili lisichukuliwe kama up-rising kama baadhi ya watu wanavyotaka tuamini, bali liwe changamoto kwa wasomi katika kuwafanya watanzania wengi wawe well informed juu ya policies, strategies ili waweze kufanya maamuzi sahihi kwa wakati muafaka.
 
personal nimesoma Azania kwa six years, maana kutoka form one mpaka six. Azania ni shule ambayo majority wanatoka kwenye low income family in Tanzania, hivyo imesababisha mikusanyo wa ada (school fee) kuwa mdogo sana. Majority ya wanafunzi hawalipi ada, mimi nilikuwa mmoja wao kwa miaka sita nadhani nimelipa 2 years. sasa basi, sidhani kama swala la vyoo ni haki ya serikali kuu kuoversite hilo.

Sisi Watanzania tumezoea big government, yaani serikali have to put his hand on everything. Swala hilo haliwezekani, what i think is Tanzania need High school fainancing reform, ile kasumba ya 100% ya fund za shule inabidi itoke adhina imeshapitwa na wakati. Each individual school need to operate from student tuitions, while government oversite the whole procidure, and also assist in funding if neccessary. This will help school to enforce tuition payments, and also school will be able to take immediately action when problem like vyoo hapened.

School is like any other organization, inabudget yake ambayo inabidi ifuate ili isirun short, sasa kwa system tuliyonayo sasa inapoteka emergency nilazima uombe pesa wizarani ili kucover tatizo. Ndio maana nilisema tatizo sio la serikali, tatizo ni mfumo mzima wa kusifund shule hizi.

Angalia nchi zilizoendelea jinsi zinavyongoza shule za msingi na high school, mfano US, state inafund partial na school tax inacontribute partial. Pesa yote ile inakwenda kwenye that particular school. Lakini Tanzania sio hivyo, pesa za ada zinakwenda kwanza adhina kisha adhina ndio wagawe kwa shule mbali mbali, matokeo yake ndio shule nyingine zinalemaa kabisa kukusanya ada, mfano Azania.

Hakuna kitu kinachoweza kuelezea vya kutosha kwanini shule ya Azania iwe na vyoo vibovu, jiko bovu n.k Kujaribu kuondoa lawama toka uongozi wa shule au serikali ni kujaribu kukwepesha uwajibikaji. Kama wanafunzi wa shule hivyo wangefanya vizuri kwenye mtihani wa Taifa bila ya shaka kuna watu wangetaka wapewe sifa. Kuna uzembe shuleni period. Suala la vyoo siyo la Azania peke yake; Kuna shule nyingi, maofisi mengi ambayo viongozi wake wamekubali uchafu na kuuona uchafu kama ni kitu cha kawaida. Wanafunzi wa shule wanahitaji kuongozwa katika mambo haya yote, ni jukumu la walimu kuwaongoza wanafunzi katika mambo haya ya usafi.
 
Mugo"The Great";103795 said:
Who is the government? Katibu Kata, Katibu Tarafa, mkuu wa wilaya.. ...Wote ni Serikali. Kinacho-lack ni uwajibikaji katika grass-roots level. Kama Headmaster si responsible, mabwana afya wako wapi?

Anyway the Bottom line is, mshikamano wa wasomi katika kuleta mabadiliko katika nchi ni muhimu. Wasomi wana exposure kubwa juu ya nini kinaendelea duniani na wengi wanatokea rural areas. Hivyo ni rahisi kufikisha Ujumbe kwa urahisi juu ya mifumo ya kisiasa, kiuchumi n.k. Suala hili lisichukuliwe kama up-rising kama baadhi ya watu wanavyotaka tuamini, bali liwe changamoto kwa wasomi katika kuwafanya watanzania wengi wawe well informed juu ya policies, strategies ili waweze kufanya maamuzi sahihi kwa wakati muafaka.

Easier said than done, isn't it? Your (and MKJJ's) words and ideas may sound great on paper but the are in practice as worthless as Nyerere and his Ujamaa political ideology. Hao Wasomi wengi wao wana lengo moja tu: kuiacha nchi na kwenda Ughaibuni kwenye mazingira mazuri zaidi ya maisha. Kwa maneno mengine, usomi ni kama "means to an end". Kama kweli moo makini na mawazo na maneno yenu, basi na nyie mngefunga mizigo huko mlipo Ulaya na Marekani na kurudi nyumbani mkasote nao bega bega hao Wasomi na kuyafanya kwa vitendo hayo mnayohubiri.
 
Wee Likamanyola kazi yako kukosoa tu. Full of yourself and negative energy...Geeeez!! What kind of a person are you? You're not normal at all..something happened in your childhood that made you so bitter and you'll remain that way until your last day
 
No...Just an observation....
Or it could be The Ngabuian Psychoanalysis at work...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom