Salaam za Mwalimu hizi hapa......

J.K.Rayhope

JF-Expert Member
Oct 26, 2011
316
31
Natuma salaam kwenu Watanzania wote na si Wadanganyika, sijawasahau, nawapenda sana. Ila nimeona niwaulize bayana, linalonikera moyoni. Hakika nilipo ni pazuri sana, ukifika wewe hutorudi. Niwaulize,

1.Kwa nini mnavaa nguo za ulaya wakati niliwajaengea viwanda?

Kiwanda cha zana za kilimo kiko wapi? n.k. Ona sasa bidha zenu hamtaki,mwataka za ng'ambo. Mnajua kodi mnayolipa ni kubwa sana kwa mataifa hayo?

2.Kwa nini nchi ina njaa wakati ardhi niliipigania hata ile Idd Amin aliyokuwa amejipimia kwamba ni yake, kwamba mlime ili msife njaa. Sasa, niliwaambia "Siasa ni Kilimo" leo mnafanya "siasa ni vurugu tupu"mtaendelea lini?

3.Naona kuna harufu ya kuuvunja Muungano,Hivi mnajua gharama yake mpaka tukaungana.Wanangu,wajukuu zangu,Vitukuu,Vilembwe,n.k ulindeni muungano.

Niko mbali sana,maisha ni mazuri,ya ikulu yana shida mno.Msipapende sana.
4.Kwanini kila Oct 14 mnasema mnanienzi,wakati sioni matendo?Ni wachache sana,wanaonienzi ,atakayekuja huku nitamwonesha,mmoja wao ni huyu niliyemtumia kuwaletea ujumbe.Nitawakumbusha mengi mliyokiuka miiko.Tupo pamoja ktk mapambano.

WENU MWALIMU.
 
Back
Top Bottom