Salaam kutoka Zanzibar - Hotuba kamili - Msikie SEIF SHARIF HAMAD-Si mchezo

Mkuu,
Bila kukuwekeni wasiwasi, FMES yuko sawa kabisa! huyu Sief - HAFAI!.. hafai hata kwa kulumangia kwa sababu huyu mtu ni pandikizi tu..CUF ni chama bora zaidi bila mtu huyu..
Kila siku anapozidisha matatizo kati ya bara na Visiwani ndivyo anavyowapa CCM support na nguvu ya kuzua sababu za kuendelea kushika madaraka kwa nguvu, wakidai kwamba kuna watu kama Sief wanaotaka kutugawanya...Vyama vya Upinzani havijengi uadui kati yao na chama tawala au kiongozi aliyeko madarakani, siasa haiwezi kwenda hivyo hata kidogo....What if Kikwete angekuwa CUF haya maneno bado yangemtoka..

Trust me, maneno ya Kikwete hayagawi watu zaidi ya hayo ya Seif kwa sababu Kikwete amezungumza kisiasa kwa kuvitumia vyama..Siasa ni mchezoi mchafu lakini una wigo lake hautoki nje ya hapo..na hii ni ruksa kisiasa lakini mjinga huyu kaingia na gear ya kuzungumzia mtu yaani Kikwete mwenyewe! imekuwa swala la personal kati yao wakati hakuna mahala Kikwete amemtaja Sief kwa jina wala ujinga wa nani mzee wa siasa kati yao.

Historia ya Zanzibar haihitaji Sief kuizungumzia zaidi ya Wazanzibar wenyewe kuifahamu kutokana na maisha yao ya kila siku..Wazanzibar walipigania haki hizi toka Sief akiwa CCM, kama waziri Kiongozi na waziri wa Elimu.. kujiunga kwake CUF haku jabadilisha matakwa ya wananchi na kama kweli anaijua vizuri Zanzibar namwomba yeye atueleze aliweza kufanikisha kitu gani akiwa kiongozi na mwanachama wa CCM.. maanake hapo ndipo tunaweza kumpima ubora wake..

Nakumbuka swali hili aliwahi kuulizwa na akashindwa kulijibu sasa narudia tena atwambie au nyie mnaomjua vizuri Sief na ubora wake twambieni mazuri alowahi kuyafanya kwa Wazanzibar akiwa Waziri kiongozi au waziri wa Elimu?...
Hakufanya la maana zaidi ya kupandikiza chuki tu kati ya Wapemba na Waunguja. na kati ya Wazanzibari na ndugu zao wa-Bara.Ni mkosoaji mkubwa (mlalamikaji)kuhusu Muungano lakini hakuna lolote analoeleza kuhusu kuboresha Muungano huo.
 
- Hapana kama ungekwua mchukia uabguzi ningekusikia maana nilimsikia Sumaye peke yake akilalamika lakini sio wengine kwa sababu ya kuamini kuficha ficha, no inatakiwa yatolewe nje kama ninavyofanya ili yashughulikiwe.

Mkuu FM ES, HUNIJUI, ndio maana huwezi jua wakati Salim anabaguliwa nilipinga ama la. Lakini kwa kusema ukweli nilipinga vibaya mno. Na hili la kubaguliwa Salim halikuanza leo. Wakati yuko AU (OAU) kama Katibu Mkuu alirudi kwa Mwalimu kumuuliza achukue fomu. Hapo ndio hili lilianza, na mwanzilishi ni Mama fulani mtu mzito aliyeko CCM (namuhifadhi jina, bali mme wake kawahi kuwa bosi Nyaraka za Taifa), alifikia kumwambia Nyerere kuwa unataka tutawaliwe na Mwarabu?. Mwalimu kuona mambo yamekuwa makubwa akamwambia Salim usichukue fomu. Hivyo halikuanza wakati wa mchakato wa uchaguzi wa 2005, bali zamani kidogo.

- Kwa sababu ndio siasa za Seif, hayo maneno ya juu hayawezi kukubalika na sisi wananchi, maana ni matusi sana na hivyo ni vyema akaeleshwa mapema kwamba akielta siasa zake za kibaguzi tunajua sababu na hatuwezi kumpa nafasi.

Maneno ya Seif (kwa uelewa wako kuona kakosea) hayawezi kufanya wazanzibar wote wasio weusi uwabague. Dhambi ya mtu mmoja haifanyi wengine wote waibebe.

- siwezi kujibu hoiaj za hicni namna hii mkuu maana kama wewe hatumii maneno kama shetani sisi tunatumia wka nia njema, Seif aache siasa za Pemba na kutuletea taifa, abaki nazo huko huko Pemba lakini hawezi kumtukana rais wa Jamhuri kwa visingizizio vya sias zake za kibaguzi, majibvu ni kwamba we know him na siasa zake na hatuwezi kumruhusu, Karume alipokuwa akilazimisha wananchi waarabu na wesui kuaona hakuwa mbaguzi ila alikuwa anajaribu ku-deal na ukweli kama mimi sasa,

Nashukuru, ndio uelewa wangu ndio maana natoa hoja za chini, wewe mwenye hoja nzito Mola akuzidishie.
Hivi unataka kusema CCM hawatoi kauli za ajabu. Kikwete alipokuwa Pemba juzi juzi aliwaambia nini kuhusu wapinzani kupata nchi. Na hata Pinda Alhamisi hii iliyopita naye kazungumza hilohilo kuwa wapinzani hawawezi kushika madaraka akiwa Bungeni. Unataka wapinzani wajibu nini?, kama viongozi wanaweza toa kauli ambazo zinaashiria kuwa hawawezi toa nchi hata pale wanaposhindwa. Karume alifanya kosa kubwa sana kulazimisha watu waoane, hiyo ni kuvunja haki za binadamu. Kuoana ni kupendana na si kulazimishana. SASA NIMEKUONA TENA JINSI UNAVYOUNGA MKONO UVUNJAJI WA SHERIA HASA HAKI ZA BINADAMU.

- Hawawezi kuiba kura Unguja kwa sababu hakuna wa kumpigia kura Seif kule Unguja, huwa wanaiaba kura za Pemba tu, ubaguzi upo na ni lazima uemwe wazi, hapa ndicho kinachomsumbua Seif, na hatutampa nafasi kuleta siasa zake za ki-Pemba kwenye Muungano.

Hivi kama unakubaliana nami CUF ilishinda uchaguzi wa 1995, hao watu walitoka wapi?. Na kama unasema CUF hawapati kura Unguja, ulizia kwa nini waliyagawa tena majimbo baada ya uchaguzi wa 1995. Unajua CUF walichukua mpaka jimbo iliyopo Ikulu (Ngome ya CCM), unalijua hilo?. Na mpaka sasa CUF wana mwakilishi Unguja. Kuhusu uizi Pemba huwa wanatumia vikosi vya usalama. Wakati karibia na uchaguzi wanajeshi, askari, zimamoto, KMKM, uwt kibao huhamishiwa zenji, hapo ndio huiba kura toka kambini. Lakini vituo vya raia kwa Pemba wanaiba kiasi kidogo manake jamaa wako ngangari kama walivyokuwa ngangari CHADEMA kwenye jimbo la Mheshimiwa Ndesamburo (Ndesapesa), unajua yaliyojiri kwa hili jimbo?.

Unajitahidi, lakini bado kidogo ingawa pia kuna hoja nzito unazitoa, lakini la ubaguzi wa Seif na hali halisi ya huko linakupa taabu sana ingawa ninajua kwua una background nzuri sana ya CUF

Sijatoa hoja yoyote nzito nje, siwezi kukubali kuwa Seif mbaguzi kwa kushinda Pemba, na CCM wanaoshinda Unguja tu nao sio wabaguzi. Tena CUF huwa wana wawakilishi na Unguja, nani wabaguzi hapo. Hili suala CCM mnatumia “Divide and Rule” kama wakoloni ni baya sana. Fanyeni maendeleo ya haki kote Unguja na Pemba mtaliondoa jinamizi linalowasumbua, sio kuiba kura.

Mfumwa ni wajibu wako kumuweka sawa mpotofu huyu. ANA MACHO HAONI AMEGUBIKWA NA CHUKI BINAFSI, ana masikio lakini anachuja cha kusikia na mwisho ana akili na amepewa elimu ya kupambanua anaendekeza hisia. Ameshindwa kutowa hoja za uhakika kwa anachokitetea UBAGUZI.
Yeye yuko mbele kukemea maovu na ufisadi lakini kwa hili limegusa UARABU na pengine element nyengine. Pengine ungemjuvya kuwa Seif juu ya rangi yake si mwarabu na hilo si geni kwa kule Zenj.
 
Mfumwa, hawa viongozi wetu hawajali kabisa dhamana kubwa tuliyowakabidhi kutuongoza. Huwa wanakurupuka na kutoa kauli bila kujali athari yake katika usalama na umuoja wa Watanzania. Kamwe huwezi kusikia kauli aliyoitoa Kikwete ikitolewa na Obama kuwaambia Republicans au kiongozi yeyote yule wa nchi za magharibi. Maana wanajua wakivurunda basi wataondolewa madarakani kwa kura, lakini Viongozi wa CCM na serikali sasa hivi wamekuwa na kiburi cha hali ya juu na wanajua pamoja na kuvurunda katika uongozi wao wakati wa uchaguzi ujao watawanyanyasa viongozi wa wapinzania, wanachama wao na wapenzi kwa kutumia vyombo vya dola watahujumu na kuiba kura na hatimaye kuiba ushindi.

Juzi juzi tumesikia Makamba akiwafananisha Wapinzani na Paka, lakini sijasikia hata kiongozi mmoja wa CCM kumwambia Makamba kwamba amekosea hivyo awaombe samahani viongozi wa wapinzani na wanachama wao, lakini wao wamesimama kidete kutaka Maalim Seif amuombe samahani Kikwete.

Dalili za uchaguzi wa 2010 si nzuri inaelekea kutakuwa na umwagaji damu mwingine ambao mwisho wake haujulikani utakuwa na athari gani katika usalama na umoja wa nchi yetu. Maafa yoyote yakitokea wakulaumiwa ni Kikwete na viongozi wa juu wa serikali na CCM. Pamoja na kuwa wana uwezo wa kufikia makubaliano ya kweli na CUF lakini hawakutoa uzito unaostahili katika kufikia makubaliano hayo na sasa kuna kila dalili kwamba vyombo vya dola vitatumika tena kuwaua raia wasiokuwa na hatia yoyote. Mwenyezi Mungu apishilie mbali.

Mungu ibariki Tanzania.

Mkuu BUBU ni HATARI SANA kwa KIONGOZI au VIONGOZI hasa wa ngazi za juu Kupoteza BUSARA na HEKIMA wakati wameshikilia dhamana ya uongozi ambayo wakati wote huendana na Maisha ya wale mnao au unaowaongoza. Labda niwasaidie kidogo kwa misemo hii ya Wahenga wanaposema: MDOMO ULIMPONZA KICHWA! Hizo kauli zao za ovyoovyo mara nyingi MADHARA yake huwakuta wengine! Na WAPIGANAPO FAHALI WAWILI ZIUMIAZO NYIKA hivyo wakati wao wanapigania MADARAKA,mishahara minono,marupurupu,magari ya kifahari nk Maumivu na mateso yanakwenda kwa Washabikiwao. Tafadhalini acheni Siasa na Sera za kinazi za Simba na Yanga. MADARAKA YANAKWENDA PAMOJA NA RISPONSIBILITY!!!!!!!! YES??..............YES.
 
Back
Top Bottom