Sala ya pamoja Maisara-Zanzibar

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
IMG_0733-564x272.jpg

Na Salma Said,
WAUMINI wa dini ya kiislamu wameitaka serikali kuchukua hatua madhubuti ya kuhakikisha madanguro, baa na nyumba zenye kuendesha vitendo viovu vinaondoshwa kwa haraka kutokana na kuwa vinaharibu vijana wengi kimaadili katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba.
Hayo yameelezwa leo katika dua ya kuliombea taifa iliyosomwa katika viwanja vya Maisara mjini hapa ambapo Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ramadhan Abdullah Shaaban alimuwakilisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi. Katika hafla hiyo.
Katika riasala ya waislamu kwenye hafla hiyo, iliyosomwa na Sheikh Ali Basaleh, kutoka jijini Dar es Salaam ambaye alisema muda umefikwa kwa serikali kuhakikisha madanguro hayo yanafungwa na kutovifumbia macho vitendo vya uuzaji wa miili na kukithiri kwa baa ambazo hivi sasa vinaonekana kushmiri kwa kiasi kikubwa.
Sheikh Basaleh alisema endapo serikali haitochukua hatua za kulikemea tatizo hilo na kutoa tamko rasmi, la kulaani mambo hayo vitendo hivyo vitazidi kushamiri ambavyo vinaonekana kuiharibu jamii kwa kasi.
Aidha aliwataka waislamu kuacha tabia ya kukodisha nyumba zao ambapo vitendo hivyo vimekuwa vikifanyika kuhakikisha wanasitisha mikataba mara moja kwa waliowakodisha wanawake wenye kuuza miili yao ambapo hivi sasa ni sehemu nyingi zimekuwa zikendesha biashara hizo mjini na vijijini.
Sheikh huyo, pia aliiomba serikali kuhakikisha inapiga marufuku uingiaji wa watoto katika kumbi za starehe jambo ambalo linavunja maadili na kupatikana kwa vijana waovu katika jamii ambao ndio tegemeo la viongozi wa baadae.
Kwa upande wake Katibu wa Ofisi ya Mufti, Sheikh Fadhil Suleiman Soraga, alisema neema ya amani na utulivu iliyopo Zanzibar ni mtihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Muumba huyo anawatazama waja wake vipi wataitumia neema hiyo.
“Ndugu zangu waislamu, neema aliyotujalia Mwenyezi Mungu ni mtihani kwetu na ana tuangalia vipi tutaitumia neema hii kwa hivyo hatuna budi kuitazama kwa vizuri na kuidumisha kwa sababu iwapo hatutaidumisha itatoweka na tutaingia katika balaa kama inavyotokea nchi nyengine ambazo tunashuhudia machafuko yanavyoendelea”,alisema Soraga.
Alisema ni wanaadamu wachache wenye kupewa neema na Mwenyezi Mungu na halafu kukumbuka kumshukuru.Sheikh Soraga aliwataka waislamu waiheshimu na kuienzi amani iliyopo pamoja na kufanyakazi kwa bidii na mashirikiano katika kujenga na kustawisha nchi.
Awali Mtangazaji wa hafla hiyo Hassan Issa, alisema inapovunjika imani ndipo inapotoweka amani, kueleza kuwa dua hiyo ni kielelezo cha kurudisha imani ambayo itajenga imani miongoni mwa wananchi wa Zanzibar.Kisomo cha dua hiyo ya kuomba amani ya nchi baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana iliongozwa na Sheikh Mussa Saleh Abdulla.
Waumini kadhaa walihudhuria dua hiyo wake kwa waume na kwa upande wao walisema ni jambo zuri kufanyika sala na dua kama hizo lakini pia waumini wasisahau wajibu wao katika kulea familia kwa kuwa hivi sasa familia nyingi zimekubwa na matatizo huku baadh ya familia zikiwa zimesambaratika kutokana na wazee kusahau wajibu wao.
Dua hii inafuatiwa dua ya mwanzo ambayo iliandaliwa na jumuia za kiislamu na kuwakusanyisha waumini wa dini ya kiislamu katika viwanja hivyo kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu ambao inaelezwa umefanikiwa kwa kiasi fulani kutokana na kuwepo kwa maridhiano ya kisiasa yalioasisiwa na Rais Mstaafu Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.
#gallery-1 { MARGIN: auto}#gallery-1 .gallery-item { TEXT-ALIGN: center; MARGIN-TOP: 10px; WIDTH: 33%; FLOAT: left}#gallery-1 IMG { BORDER-BOTTOM: #cfcfcf 2px solid; BORDER-LEFT: #cfcfcf 2px solid; BORDER-TOP: #cfcfcf 2px solid; BORDER-RIGHT: #cfcfcf 2px solid}#gallery-1 .gallery-caption { MARGIN-LEFT: 0px}

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom