sakaya wa cuf kweli ngangari.

in and out

Member
Jun 30, 2011
69
6
magdalena sakaya leo ameliambia bunge juu mkuu wa wilaya wanavyojichukulia mifugo ya wanainchi huko urambo-tabora, ameombwa amtaje kiongozi anayefanya hivyo au afute kauli yake lakini mbunge ameonyesha ungangari kwa kusimamia kauli yake, ametakiwa apeleke ushahidi mpaka jtatu mbele ya spika.
 
Nasema hivii,ofisi ya spika itajaa ushahidi wa wabunge hadi atakosa pa kukalisha makalio yake.........aanze kupunguza kwa kusoma mbele ya wabunge,maana atajaza MIKARATASIIII
magdalena sakaya leo ameliambia bunge juu mkuu wa wilaya wanavyojichukulia mifugo ya wanainchi huko urambo-tabora, ameombwa amtaje kiongozi anayefanya hivyo au afute kauli yake lakini mbunge ameonyesha ungangari kwa kusimamia kauli yake, ametakiwa apeleke ushahidi mpaka jtatu mbele ya spika.
 
kwa kweli spika anaboa sana, mimi nadhani nae angewaeleza tu walio mtuma kuwa kazi ya u spika imemshinda.
 
Huyu Sakaya anafaa cdm tatizo ni cuf ndio maana naona taabu kumsifia. Pipooooz......
 
Re: sakaya wa cuf kweli ngangari.
Umeona alivyo mchana Ngeleja na kumwambia kazi hawezi na ajiuzulu? Nimemkubali jimama. Kuna watu wakiongea unaona kabisa ana uchungu wa dhati na nchi na wananchi wake.
 
hapa muongozo a spika unahitajika! yaani kama sio wa chadema huwezi kumsifia hata kwa wema wake? hizi ni siasa za chama tawala tunazozilalamikia kila leo,kuwa wabunge wanaunga mkono hoja mbovu na kukataa hoja nzuri za upinzani. nadhani focus yetu wote ni maslahi ya wengi na isiwe vyama kihivyo!
Huyu Sakaya anafaa cdm tatizo ni cuf ndio maana naona taabu kumsifia. Pipooooz......
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Angesema mbunge wa ccm,vikao vngemuandama
Umeona alivyo mchana Ngeleja na kumwambia kazi hawezi na ajiuzulu? Nimemkubali jimama. Kuna watu wakiongea unaona kabisa ana uchungu wa dhati na nchi na wananchi wake.
 
Huyu Spika ana uthibitisho katika ofisi yake in that chronological
  1. Mh Lema V Pinda kuhusu Pinda kusema uongo bungeni
  2. Mh. David Kafulila V Godfrey Zambi kuhusu wabunge kuhongwa Handeni
  3. Mh. Peter Msingwa V Pinda Kwenda na mashangingi kadhaa na ndege mkoani Katavi
  4. Mh. Zitto Kabwe V Baraza la mawaziri kuhusu baraza la mawaziri kuwa lobbyed kubadilisha maamuzi ya tume kuhusu CHC
  5. Mh. Magdallen Sakaya V Waziri TAMISEMI kuhusu ma DC kutwaa mali za wananchi kwa nguvu.
Tunamtaka mama Makinda awaruhusu waheshimiwa hao wasome uthibitisho wao mbele ya bunge in that chronological. Tumechoka huyu Anne kuendelea kuyaatamia Makinda yake (read CCM)
 
Kama kila kitu kitakachotolfwa bungeni kitolewe ushahidi nchi inaelekea pabaya.wakati mwengine shutma husababisha mtu kujirekebisha.suali lakujiuliza hapa je ktk jamii hawapo viongozi kama hao.lazima viongozi wt wajifunze kukubali ukweli
 
Wanaolikoroga ni wale wanaoomba miongozo kana kwamba hawajui kinachoendelea huku kwa "mtogole". Ni hivi, baadhi ya viongozi wetu wamejifanya miungu watu kwenye maeneo ya kazi. Wapinzani na baadhi ya wanaccm wameliona hilo. Ni swala la kukubaliana kuwakabiri wajirekebishe na ama wawajibishwe. Vinginevyo mkiendelea kuomba ushahidi...
 
Nafikiri Spika wa Tanzania amekosa busara.

Na hilo ni tatizo kubwa sana katika uongozi especially kuongoza muhimili huu wa Doula.

Poleni sana kwa uchaguzi wenu kwake.
 
Back
Top Bottom