Sakata la wizi wa masanduku ya kura Kisarawe, Chadema yashinda uchaguzi wa Marudio

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
2,973
3,901
Wiki chacha zilizopita nilianzisha uzi hapa JF wa kuahirishwa kwa uchaguzi wa kijiji cha Mwanzo Mgumu, kata ya Msimbu wilayani kisarawe Mkoa wa Pwani ( Nyumbani kwa Baba Riz 1) kutokana na 'mabaunsa' wasiofahamika kuvamia chumba cha kuhesabia kura na kutokomea na masanduku yote yaliyohesabiwa kura na yasiyohesabiwa kura. Vile vile nikasema kuwa wakati huo Chadema walikuwa na zaidi ya kura 100 zilizohesabiwa huku CCM ikiwa na kura zaidi ya 20.

Nikasema kuwa Uongozi wa wilaya haukuweza kumchukulia hatua mtu yo yote pamoja na wananchi kuwataja wahusika siku chache baada ya tukio hilo. Nikawapa Changamoto waandishi wa habari watupe undani wa habari ile na kuziweka magazetini.

Habari ile ilileta ubishi mkubwa sana hapa JF wengine wakisema Aweda anafanya proganda za Chadema dhidi ya CCM.
Hata hivyo, leo naomba kuleta taarifa rasmi kwamba Chadema wameshinda uchaguzi huo uliorudiwa na kufanikiwa kuitwaa serikali ya kijiji kwa mara ya kwanza ktk wilaya ya Kisarawe (mkoa wa pwani, Ngome ya Baba Riz 1, to the best of my knowledge).

Huu ni ushidni wa nguvu ya umma kwa sababu serikali ilifanya juhudi kubwa kuwatisha wananchi ili wabadilishe maamuzi yao kumchagua mtu wasiyemtaka, lakini wananchi waligoma kufanya hivyo, uongozi wa wilaya ukafyata mkia na kukubaliana na matakwa ya wananchi bila ridhaa yao.

Uchaguzi ulifanyika tarehe 10 mwezi huu
Kura zilizopatikana baada ya nguvu kubwa kutumika kuwashawishi na kuwalazimisha wananchi wabadilike bila mafanikio ni kama ifuatavyo;

Chadema - Saidi Selemani Mulugendi 148

CCM - Jabiri Nasoro Kibiriti 141

zilizoharibika 13.

Waliokuwa wanasema kuwa nafanya propaganda dhidi ya CCM sasa kubalini kwamba nilikuwa na sema kweli.

Naona CD ya ccm ya Ukabila imepotea, ya Ukanda imepoteza wateja na sasa ya udini nayo imeanza kuchuja (Mwanzo mgumu Msimbu wakristo 5%).. Je, ni CD gani sasa itazinduliwa na ccm? ya Chama cha vurugu? Kazi kwao. Mimi sipo.
 
Ngome baba ya baba riz kushney.....! Aweda hongera kwa kutuletea kilichofuata naukumbuka sana ule uzi wa kwanza, pamoja na hila zao awam hii lazma wafyate mkia, ingekuwa poa ungetuwekea na idad ya kura kabisa.
 
Ipe uhai taarifa yako, mfano jina la mshindi, kura alopata nk. Jamii ya .com inahitaji taarifa zenye uzito timilifu.
 
Wiki chacha zilizopita nilianzisha uzi hapa JF wa kuahirishwa kwa uchaguzi wa kijiji cha Mwanzo Mgumu, kata ya Msimbu wilayani kisarawe Mkoa wa Pwani ( Nyumbani kwa Baba Riz 1) kutokana na 'mabaunsa' wasiofahamika kuvamia chumba cha kuhesabia kura na kutokamea masanduku yote yaliyohesabiwa kura na yasiyohesabiwa kura. Vile vile nikasema kuwa wakati huo Chadema walikuwa na zaidi ya kura 100 zilizohesabiwa huku CCM ikiwa na kura zaidi ya 20. Nikasema kuwa Uongozi wa wilaya haukuweza kumchukulia hatua mtu yo yote pamoja na wananchi kuwataja wahusika siku chache baada ya tukio hilo. Nikawapa Changamoto waandishi wa habari watupe undani wa habari ile na kuziweka magazetini.
Habari ile ile leta ubishi mkubwa sana wengine wakisema Aweda anafanya proganda za Chadema dhidi ya CCM.
Hata hivyo, leo naomba kuleta taarifa kwamba Chadema wameshinda kwa kura nyingi uchaguzi huo uliorudiwa na kufanikiwa kuitwaa serikali ya kijiji kwa mara ya kwanza ktk wilaya ya Kisarawe (pwani Ngome ya Baba Riz1) to the best of my knowledge. Huu ni ushidni wa nguvu ya umma kwa sababu serikali ilifanya juhudi kubwa kuwatisha wananchi ili wabadilishe maamuzi yao na wamchagua mtu wasiyemtaka, lakini wananchi waligoma kufanya hivyo, uongozi wa wilaya ukafyata mkia na kukubaliana na matakwa ya wananchi bila ridhaa yao.
Waliokuwa wanasema kuwa nafanya propaganda dhidi ya CCM sasa kubalini kwamba nilikuwa na sema kweli.
Ukiona watu wa Pwani wameamka ujue ukombozi tayari. Peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeez poweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeer.
 
Duh! Mpaka Pwani! Au Kisarawe nayo imehamishiwa Kaskazini! Magamba Kwishney!
 
Siku zote, mvumilivu hula mbivu, na Mwenyezi Mungu hujibu sala za waja wake. Viva Chadema, viva wanachadema wa pwani na wananchi wote wa pwani.
 
Mkuu, kwa kazi kubwa tunayoifanya ya kupambana na magamba, it is obvious kwamba hakuna uchaguzi tunaoshindwa! Swala linabaki tu kwamba wasimamizi wanaamua kumtangaza nani. Hiyo ndiyo changamoto iliyobaki. Otherwise ccm ilishakufa zamani. Hongera wana Kisarawe kwa kuhakikisha mnapata mnachokitaka!
 
Hapa sasa ngoja kabisa nitafute suti ya rangi za cdm niiweke tayari kwa 2015!!manake target yangu ya mwisho ilikuwa pwani.
 
Back
Top Bottom