Sakata la Wazee EAC: Litaisha lini?

Wengine wanaonekana vijana???!!! haielekei kama wote hawa walikuwa kazini miaka 30 iliyopita!

Mkuu hao wengine ni warithi wa marehemu baba zao ama babu zao waliokuwa wakifanya kazi EAC, ndo wandai badala ya hao waliokufa ama wengine ni wazee sana kufatilia madai yao!!

Ushi
 
Mwalimu gani? kama ni marehemu Julius, huyu babu mwacheni tu apumzike, kwani inaboa sasa hii tabia ya kila kitu mwalimu, mwalimu.....ukweli ni kwamba EAC ilivunjika mwaka 1977, yeye Mwalimu ibn Mtukufu, a.k.a messiah, a.k.a the saint akiwa rais, wakti anang'atuka ilikuwa ni takribani miaka nane toka hii kitu i-collapse!! swali, alikuwa wapi kuwalipa hawa waungwana mafao yao? Leo hii ni miaka 31 toka kuanguka kwa EAC...awamu zote nne za serikali nchini Tanzania zimepitia hili tatizo, lakini all of a sudden lawama zooooooooote kwa huyu kikwete na serikali yake ya kifisadi, wakti tunajua kuwa tatizo hili kalirithi toka kwa Mkapa, Mkapa toka kwa Mwinyi na Mwinyi toka kwa Nyerere.......

Badala ya kutoa lawama kwa serikali kwa staili hii ya chuki na kutafuta visababu, tuanze kutoa mawazo sahihi ya jinsi gani ya kutatua matatizo ya namna hii badala ya finger pointing wakti fwacts zipo wazi....pesa za hawa wazee zilishatoka na kuliwa kabla Kikwete hajawa POTURT!!!.

Hili tatizo si jipya, mnyonge mnyongeni lakini kuweni wa kweli.......njooni na mawazo na jinsi mbadala za kupata fweza za kuwalipa hawa wazee, badala ya makelele na ku-politik huu "mshipa" ulioachwa na Nyerere!

asubuhi njema....

Ndugu yangu YournameisMINE, unajua unachokisema au unasema unachokijua. Hivi unajua kwanini hawa wastaafu wanainuka kudai haki zao leo na si miaka mitatu baada ya kuvunjika kwa shirikisho. Hivi vitu haviji tu kutoka hamna mahali. Vina sababu zake. Kwa kukusaidia nenda tena kapitie madesa yako ya historia ya uchumi wa nchi hii.

Hivi unaweza kumdai mdeni wako aliefilisika na unajua kwamba amefilisika!!

Kwa kuongezea hapo, nilikuwa naamaanisha MWALIMU NYERERE!!!!. Haihitaji digrii kujua kuwa mwalimu alikuwa binadamu. Kuna wakati alifanya vitu sivyo ndivyo. Lakini kwa hili la wazee si la kumnyooshea kidole mwalimu hata kidogo. Ni uhuni tu wa hawa jamaa!!!.
 
Mwalimu gani? kama ni marehemu Julius, huyu babu mwacheni tu apumzike, kwani inaboa sasa hii tabia ya kila kitu mwalimu, mwalimu.....ukweli ni kwamba EAC ilivunjika mwaka 1977, yeye Mwalimu ibn Mtukufu, a.k.a messiah, a.k.a the saint akiwa rais, wakti anang'atuka ilikuwa ni takribani miaka nane toka hii kitu i-collapse!! swali, alikuwa wapi kuwalipa hawa waungwana mafao yao? Leo hii ni miaka 31 toka kuanguka kwa EAC...awamu zote nne za serikali nchini Tanzania zimepitia hili tatizo, lakini all of a sudden lawama zooooooooote kwa huyu kikwete na serikali yake ya kifisadi, wakti tunajua kuwa tatizo hili kalirithi toka kwa Mkapa, Mkapa toka kwa Mwinyi na Mwinyi toka kwa Nyerere.......

Badala ya kutoa lawama kwa serikali kwa staili hii ya chuki na kutafuta visababu, tuanze kutoa mawazo sahihi ya jinsi gani ya kutatua matatizo ya namna hii badala ya finger pointing wakti fwacts zipo wazi....pesa za hawa wazee zilishatoka na kuliwa kabla Kikwete hajawa POTURT!!!.

Hili tatizo si jipya, mnyonge mnyongeni lakini kuweni wa kweli.......njooni na mawazo na jinsi mbadala za kupata fweza za kuwalipa hawa wazee, badala ya makelele na ku-politik huu "mshipa" ulioachwa na Nyerere!

asubuhi njema....

.........much as I hate to admit it, you have a very big POINT there, mkuu!
 
Picha wazee walikuwa barabarani leo asubuhi !

2779d1225273240-wazee-wa-eac-wafunga-barabara-cos.024.jpg

2780d1225273240-wazee-wa-eac-wafunga-barabara-cos.023.jpg

Nimesaidia kuziweka zionekane. Ukishazi-upload una-copy link, halafu unatumia "insert Image" japo source ni JamiiForums.

.
 
Mie nafikiri uraisi ni taasisi na ukikaa pale uyapokee yote unayoyakuta yakiwemo mazuri na mabaya.

Visingizio vya eti 'ameyarithi' havitatupeleka popote; kama ambavyo anafungua miradi mipya iliyoanzishwa na watangulizi wake, tena kwa mbwembwe, vile vile ayabebe matatizo yalioachwa na awamu zilizopita yakiwemo ya wizi wa EPA na madeni ya wastaafu.

....and you have an even BIGGER POINT, mkuu! I LOVE JF!
 
Wengine wanaonekana vijana???!!! haielekei kama wote hawa walikuwa kazini miaka 30 iliyopita!

wazee wao nafikiri watakua hawajiwezi au walisha aga dunia kwaio watakua wanawakilisha

by the way sizani mtu asubuhi yote ile uende tu kufunga barabara bila sababu yoyote labda uwe na upungufu wa akili.

leo msg nafikiri imewafikia ipasavyo serikali
 
This is an embarrasment!Ninaungana na Gembe kwamba JK is a one term president!Hivi huyu mtu ana masikio kweli?Haoni watu wameshachoka kabisa?Na bado serikali isipotoa tamko lao kuhusiana na ada za wanafunzi nao wanagoma!Jana waaandishi wa habari leo wazee kesho nani?Is this country on the verge of collapsing and being termed as a failed state?
Sijui tunakoelekea kwa kweli!
 
i think we have an ceremonial president
 
wamekoma, hao wazee so ndo namba wani wapiga kampeni za ccm kwamba ndo chama chao cha zamani? sasa mbona selikali wanayoipenda imewasaliti, wakione cha moto kidogo. vijana tunaposema waachane na icho chama wao huwa wanafikiri tunawapoteza. ni funzo kwao kwa uchaguzi wa 2010. poleni kidogo tu lakini.
 
Zipo pia namna nyingine za kudai haki kuliko kusababisha usumbufu kwa watu wasiohusika na mzozo huo. Kuna jamaa wamechelewa flight na wengine tunafanya kazi za kubangaiza na binafsi nimechelewa kutuma bid. Manake nimekosa dili na nina bifu na wazee na serikali vile vile.

Mnapodai haki zenu watazameni na wengine kama kila mtu anajijali mwenyewe hatutafika. Huu ni uchoyo wa watu weusi kutazama kila mtu maslahi yake hatutafika na tutaendelea kuchapa miguu na kubuluzwa miaka yote. Politike kuweka mbele pia sio poa maisha ni zaidi ya siasa.

Wazee wamekuwa wastaarabu vya kutosha. Kama sikosei pesa zao zilitolewa tangu 1984 ni miaka 24 sasa tangu pesa zitolewe. Na wameanza kudai pesa zao kwa kutumia njia za kistaarabu bila kuwaathiri wasiohusika na kama binadamu inafika wakati wanaona ni bora watafute njia mbadala ndiyo watasikilizwa. Kikwete haoni kama kuna umuhimu wa kukutana na wazee hao, anadhani kwa kukaa kimya tatizo la wazee hao litakwisha kimya kimya. Kuna faida gani basi ya kuwa na kiongozi wa nchi ambaye hayuko tayari kutafuta uvumbuzi wa matatizo yanayowakbili wananchi wake!? Kama nchi imemshinda ni bora aachie ngazi kuliko kuendeleza usanii.
 
.

TATIZO LA EAC LILIANZA NA MCHONGA...HUO NDIO UKWELI.

You nail it bro,

I think it will be better if we could put like this. UFISADI uliaanza zamani sana hata kabla ya Mkapa sema watanzania wengi walikuwa hawajasoma na pia magazeti yalikuwa hayako huru sababu yalikuwa yamejaa jukwaa la wahariri lile kla zamani ambalo serilai inalitambua.

Jukwaa hili jipya ni kiboko,Absalom Kibanda unatisha mdogo wangu..Keep it up,Najua ulimpa sana heko Mkulu Jk kipindi cha 2005 kabala haujamfahamu.

Pesa za Wastaafu zililiwa kipindi cha mchongo na wizarani hazipo,ila busara inatakiwa itumike kwa rais kutoa pesa katika mfuko wa rais,una pesa nyingi sana ..

toka mwezi uliopita wastaafu na maandamano,Yes am tired with this issues,Rais wangu naomba uchukue hatua hata kama awewe ni bubu mtendaji?
 
Mimi sina mtazamo huo. Angekuwa ni mtu asiye na mikono michafu suluhu ya tatizo hili ingepatikana, na uwezo huo Raisi anao.

Yaani unataka kuniambia kwamba JK anapata kiburi kwa sababu eti tatizo amerithi? Ajitokeze hadharani basi ayaseme hayo kama hakupigwa risasi. Utakuwa ni ushenzi usio na kifani.

Hiki sio kisingizio anachoweza kukitumia.
Ngoja nikuulize, wewe ulimwelewaje Nyerere aliposema IKULU sio pa kukimbilia?
.

Hilo swali lako mkubwa limenifurahisha sana, tena sana!Ikulu siyo mahali pa kukaa na kula kuku kwa mrija, pale ndio makao makuu ya matatizo yote ya Watanzania! Kama mtu anakimbilia pale akidhani kwamba kwenda kula starehe, matokeo yake ndio hayo sasa!! Kila kukicha maandamano!
 
mimi kinachonisikitisha ni kwamba utasikia rais anataka kuongea na wazee wazee hao hao ndo watakwenda na kupiga makofi na nyimbo za kumsfia kwa sana. Pamoja na hilo inasikitisha sana kuon vingozi wetu wanashindwa kushughulikia suala hili la wazee wetu kwa ufanisi mpaka yanatokea haya yote. Kwakweli hata vyombo vya usalama nilidhani vingepaswa kuheshimu hawa wazee wetu , inasikitisha san kuona viongozi wetu wanakosa heshima na huruma
 
Jamani hawa wazee pesa zao zilitumika kupigana vita ya kagera na uingereza iliahidi kulipia pesa hizo mpaka leo hazijalipwa
 
Jamani hawa wazee pesa zao zilitumika kupigana vita ya kagera na uingereza iliahidi kulipia pesa hizo mpaka leo hazijalipwa

ina maana pesa ya wastaafu ililipwa kwa ajili ya vita??
 
Zipo pia namna nyingine za kudai haki kuliko kusababisha usumbufu kwa watu wasiohusika na mzozo huo. Kuna jamaa wamechelewa flight na wengine tunafanya kazi za kubangaiza na binafsi nimechelewa kutuma bid. Manake nimekosa dili na nina bifu na wazee na serikali vile vile.

Mnapodai haki zenu watazameni na wengine kama kila mtu anajijali mwenyewe hatutafika. Huu ni uchoyo wa watu weusi kutazama kila mtu maslahi yake hatutafika na tutaendelea kuchapa miguu na kubuluzwa miaka yote. Politike kuweka mbele pia sio poa maisha ni zaidi ya siasa.

ukiangalia vitu kama hivyo mabadiliko hayatatokea, ni kupunguza kero lakini cha msingi ni kafanikiwa katika malengo
 
wamekoma, hao wazee so ndo namba wani wapiga kampeni za ccm kwamba ndo chama chao cha zamani? sasa mbona selikali wanayoipenda imewasaliti, wakione cha moto kidogo. vijana tunaposema waachane na icho chama wao huwa wanafikiri tunawapoteza. ni funzo kwao kwa uchaguzi wa 2010. poleni kidogo tu lakini.

Mwana wa Mungu, sikuungi mkono katika hili.
Sio kweli kuwa wazee ndio wanaishikia wanaopenda ccm tu, bali hata vijana kwa ujumla mmekuwa wagumu mno wa kufikiri.

Takwimu zinaonyesha kuwa karibia asilimia 49% ya watanzania ni umri wa miaka 0-17, 33% ni umri wa miaka 18-44, wakati wazee wa umri wa 45-100 ni sawa na 18%.

Kwa taarifa zaidi vijana kati ya miaka 18-34 ni takribani 23%, wakati watu wa umri 35 na zaidi ni 28%, sasa hapa unaonaje.

Sasa kuwasingizia wazee wakati vijana mmekuwa wagumu wa kubadilika ni makosa, ona jinsi wazee wanavyoonyesha uweza wa kudai haki zao, mie nawaunga mkono. Bado kama vijana wangekuwa wakweli, hali isingekuwa hii tunayoiona leo.
 
tunaangalia vitu ktk lens tofauti! wewe umejaa ushabiki na jazba, unangalia vitu juu juu bila kuangalia tatizo limeanzia wapi ili kupata ufumbuzi ulo sahihi.....

kwa akili yako unadhani mie namtetea Kikwete?
la hasha, nilichokuwa nasema mimi, hii rhetoric hapa inafanya ionekane kana kwamba hili tatizo limemea ktk awamu hii, wakti si kweli......mshipa huu uliachwa na mchonga!! kama hutaki basi...ndio, anatakiwa atafute ufumbuzi kwa kuwa yeye ni rais,

Kwanza nakiri kwamba nimepatwa na jazba, lakini hio haibadilishi kitu, msimamo wangu hautabadilika jazba itakaposhuka. Chanzo cha jazba yangu ni jazba iliyojionesha kwenye post yako ya awali. :)

Naelewa unachosema, sioni tatizo kuuingiza uongozi wa Nyerere kwenye hili. Hata hivyo ulimtetea JK bila kujua unafanya hivyo. Halafu uchaguzi wa mtu uliyeamua kum-quote ndio ulileta balaa, maana Lighondi alikuwa akizungumzia kitu muhimu sana ambacho uongozi wa sasa kwa uzembe na ubinafsi umethubutu kupuuzia.

Maneno ya Lighondi hapa.

...lakini isiwe sababu ya kusema "oooooh kwa ajili ya hili, basi huyu bwana kweli ni one term president." Kila mtu anajua incompetency ya awamu hii, kama nilivyosema awali huko juu..mnyonge mnyongeni, lakini semeni basi na ukweli. TATIZO LA EAC LILIANZA KTK AWAMU YA KWANZA, MCHONGA AKIWA RAIS...huo ni ukweli!!!

Punguzeni jazba....

Nimekuelewa.

.
 
Back
Top Bottom