Sakata la Wazee EAC: Litaisha lini?

God heal our beautiful land Tanzania. Give us courage and wisdom to seek you when it is tough and no one hears our cry especially those authorities that we have voted and put them in positions to lead us. God, grant the wishes and prayers of the old men and women who today had taken drastic measures which endangered their lives, as fragile as they are, just to demand to be heared. It is not easy God but with you am sure they got the strength and courage to go the extra mile, they have written letter, visited all the necessary channels - ministries, and all other places that could have assisted them, but to no avail, they have made demostrations, they have camped at the state house garden, no one heared, today, they decided to sleep on the road - where the impact of their cry will reach all areas - of our surrounding society. God we believe this is not the end, but their cry has been heared and they will be answered, give them extra strength and energy, for with their sacrifices we the coming generation will not have to go through the same process, as their journey and struggle will not go in vain. Protect them whereever they are. In you God we pray.
Bless our country and hear our cry.
We pray!
 
Tatizo Watanzania hatuna mshikamano thabiti, hadi kitu kiguse maslahi binafsi ya mtu ndo utasikia watu wanalalamika. Nadhani hatua waliochukua wazee hao ni sahihi kabisa maana itawafanya watu wote waone kuusika kwao kwa tatizo la wazee hawa.

inatakiwa hii waiendeleze wakati JK atakaporudi DSM wakafunge njia unapopita msafara wake wamlazimishe ashuke kusikiliza tatizo lao na kutoa majibu yanayoeleweka.

Yalishatolewa mapendekezo mengi hapa JF ya jinsi ya kushughulikiwa kirahisi kwa tatizo hilo nashangaa hivi hiyo wizara haina wawakilishi humu japo wakawasaidie mawazo?

I wish kama serikali hii ingekuwa wagumu hivyohivyo kwenye kusaini mikataba mibovu.

Zama hizi hazitapita bure, majibu yake lazima JK na CCM yake watakuja kuyajutia. wazee hawa hawa ndo wamekuwa ushawishi kwa watu kuichagua sisiem sintashangaa wazee hawa hawa sasa ndo wakaja kuwa ushawishi wa CCM kutupwa jehaman ya kisiasa. hama hizo tunazisubiri kwa hamu.

Mungu Iponye Tanzania na mikono hii hatari

Amin
 
Naona kuna thread mbili kuhusu hawa wazee,si vibaya zikawa merged! Mungu wabariki wazee na utubariki sisi tunaowakosea heshima wazee hawa ili tuweze kubadilika na kuwatendea haki na heshima wanayostahili!
 
Ilinilazimu kupanda bajaji leo, hata hivyo nilikuwa niko tayari kutembea kwa mguu kwa furaha kabisa niliposikia wazee wamefanya kweli.

Watanzania sasa wana mwamko na wanatambua haki zao. Wanazidai, ila tu bado hawajafahamu vizuri njia sahihi za kudai haki hizo. Kurusha mawe ni sehemu ya mchakato mzima, with time hali hii itabadilika.
 
nimejaribu kupata baadhi ya picha japo kwa kamera yangu sio nzuri ila itawapa picha wanajamii. jamani huku sio iraki ni posili walivyo kuwa wanawazitibu
i88_Image076.jpg

i89_east.jpg

i90_Video0130001.jpg
 
Zipo pia namna nyingine za kudai haki kuliko kusababisha usumbufu kwa watu wasiohusika na mzozo huo. Kuna jamaa wamechelewa flight na wengine tunafanya kazi za kubangaiza na binafsi nimechelewa kutuma bid. Manake nimekosa dili na nina bifu na wazee na serikali vile vile.

Mnapodai haki zenu watazameni na wengine kama kila mtu anajijali mwenyewe hatutafika. Huu ni uchoyo wa watu weusi kutazama kila mtu maslahi yake hatutafika na tutaendelea kuchapa miguu na kubuluzwa miaka yote. Politike kuweka mbele pia sio poa maisha ni zaidi ya siasa.
 
Kama kuna jambo linalonisikitisha siku zote basi ni hili la wazee wa EAC,hawa wazee hawastahili kufedheheshwa na kutopewa heshima namna hii.serikali yoyote makini ingeanza na hili kwanza kama priority kabla ya kudandia hayo mengine!

Jamani kuna anayeweza kuquantify madai ya hawa wazee ili tujue tunazungumzia fedha kiasi gani? je hiyo pesa iliyorudi toka kwenye EPA kwasababu ilikuwa haijapangiwa chochote kwanini isitumike kwenye kuwalipa hawa wazee wa EAC na pengine kulipa hayo mafao ya walimu? maana huko ndiko tunaweza kuona tangible things happening kuliko huko kwenye mfuko wa kilimo ambako ni geresha tupu!

Tafadhali mwenye kufahamu madai ya wazee ni kiasi gani na tujumlishe na bilioni 12 ya walimu tuone kama zile za EPA "zilizorudi'' kama zaweza tosha kumaliza haya majanga ya walimu na wazee!
 
Hali inasikitisha...

sijajua nia na madhumuni ya Serikali kufanyas hivi ni nini. Danadana zimekuwa nyingi sana katika Suala la EAC.

Utawala wa Awamu ya nne unatawaliwa na Migomo, maandamano na Usanii mwingi. Najaribu fikiria ni nani atakuwa Mgombea upande wa CCM mwaka 2010.
 
Ukiona wazee wa umri kama huu nao wameamua kulala barabarani ili kuishinikiza serikali iwalipe mafao yao basi ujue kwamba serikali haina nidhamu kwa wazee wa nchi nzima. Tanzania ya amani si ile tunayoiimba katika halaiki. Sasa imekuwa ni nchi inayoongozwa na viongozi waliokubuhu jeuri. Ifike wakati mkawapa heshima zao wazee hawa kuliko kuacha wakaharibu "image ya Tanzania katika siasa za kimataifa. Ni aibu sana kudhulum wazee kama hawa.

Kwakweli haiingii akilini hata kidogo kwa jinsi tunavyoona Baba na Babu zetu wanavyoteseka. Hivi viongozi wetu wanadhani wao hawatazeeka? Je, wao hawana wazazi kama hao? Je, wabunge wetu ambao tunawaita wawakilishi wa wananchi hawalioni hili? au wanadhani tuliwachagua waende kushughulikia posho zao tu? Maana kila kukicha tushuhudia jinsi wanavyohangaikia posho zao ili zipandishwe. Miezi michache iliyopita wamefanikiwa kujiongezea mgao wa mafuta ya mashangingi yao kutoka lita 500 kwa mwezi hadi lita 1,000 kwa mwezi. Je, kwa safari zipi walizonazo? Maana magari haya yote tunayaona hapa Dar kila siku.

Bado nakumbuka sana hotuba za mwalimu, ..........dhambi ya ubaguzi ukishaitenda ujue itakutafuna........., Je hawa viongozi wetu wataweza kuikwepa dhambi hii isiwatafune? Tusubiri tutaona.
 
Nimesikitishwa SANA na kitendo cha Serikali kutumia mabavu kuwaondoa wazee wetu. Wamekosa msaada, wamelia siku nyingi sana lakini kilio chao kilionekana kuwa cha samaki. Kwa busara zao waliamua wakae njia panda ambako mabalozi wanatokea (hapa walipatia) tena kwa amani, walitambua hata viongozi wengi wanatumia njia hii hivyo wakiwaona wanaweza kukumbuka kuwa kuna deni la wazee hawa.

Hivi wanataka kuwalipa wajukuu wao? Au ndio kutaka tuamini kuwa haki haipatikani bali kwa ncha ya upanga? Imenisikitisha SANA.

Masikini Tanzania...
 
Kwa serikali inayoongoza kwa kutumia akili hizi warning zingekuwa ni nzuri sana kwao, lkn kwa yetu hapa ni ubabe tuu na ndio kuzidi kuharibu mambo... Nimeipenda san ahii strategy, wazee, watz tusikate tamaa bado kidogo tuu tunafika, yes we can.
 
Nimesikitishwa SANA na kitendo cha Serikali kutumia mabavu kuwaondoa wazee wetu. Wamekosa msaada, wamelia siku nyingi sana lakini kilio chao kilionekana kuwa cha samaki. Kwa busara zao waliamua wakae njia panda ambako mabalozi wanatokea (hapa walipatia) tena kwa amani, walitambua hata viongozi wengi wanatumia njia hii hivyo wakiwaona wanaweza kukumbuka kuwa kuna deni la wazee hawa.

Hivi wanataka kuwalipa wajukuu wao? Au ndio kutaka tuamini kuwa haki haipatikani bali kwa ncha ya upanga? Imenisikitisha SANA.

Masikini Tanzania...

wamesha kwambia wanaostahili kulipwa ni wazee 18 tuu.... huu ni usanii wa hali ya juu... mbona vingine vinawezekana mashangingi mmejinunulia kwa bei kubwa tuu kuwapa chao hawa wazee inakuwa tabu?????
 
wazee mkitoka huko kama hamjalipwa uzi uwe huo huo, walimu amkeni mfanye vitu vyenu mgomo baridi hauwagusi kabisa hawa washenzi, watotto wao wanasoma nje ya nchi.... mnatuumizia watoto wetu sisi tunaolala hoi, tusijichanganye kuumizana wenyewe jama... kila kitu kifanyike kwa kuwalenga wao ili wapate ujumbe
 
God heal our beautiful land Tanzania. Give us courage and wisdom to seek you when it is tough and no one hears our cry especially those authorities that we have voted and put them in positions to lead us. God, grant the wishes and prayers of the old men and women who today had taken drastic measures which endangered their lives, as fragile as they are, just to demand to be heared. It is not easy God but with you am sure they got the strength and courage to go the extra mile, they have written letter, visited all the necessary channels - ministries, and all other places that could have assisted them, but to no avail, they have made demostrations, they have camped at the state house garden, no one heared, today, they decided to sleep on the road - where the impact of their cry will reach all areas - of our surrounding society. God we believe this is not the end, but their cry has been heared and they will be answered, give them extra strength and energy, for with their sacrifices we the coming generation will not have to go through the same process, as their journey and struggle will not go in vain. Protect them whereever they are. In you God we pray.
Bless our country and hear our cry.
We pray!

Amen!

.
 
Jamani wazee wanadai shilingi ngapi kwa ujumla wao? naombeni hiyo hesabu kutokana na madai ya wazee wenyewe siyo kama serikali inavyosema!
 
Back
Top Bottom