NgomaNzito
JF-Expert Member
- Jan 10, 2008
- 559
- 26
Wapendwa muda huu kuna maandamano pale mwanza kupinga ubadilishaji wa matumizi ya uwanja wa Nyamagana. Eti mgeni rasmi ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza (mpenda vyeo) sasa wakati anahutubia na waandamaji wakitegemea kuwa atatoa tamko rasmi badala yake akawaambia wananchi wajaze saini zao kwenye daftari lililotolewa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza la kupokea maoni yao.
Waandamanaji walipomzomea akaanza kuwatishia kuwaweka ndani
Ndiyo kusema mpaka leo hakuna city planners mpaka madiwani waplan.Maana hawa planners lazima wameshaandaa maeneo kulingana na matumizi.Au hilo eneo ndiyo limevumbuliwa sasa.This is unbelievable.Either I am not sure of Dar or Ar if they real have and effectively utilize city planners.
Jk amwondoe huyu Mkuu wa mkoa (a.k.a mpenda vyeo) amekuwa ni mchonganishi kati yake na viongozi mbalimbali jana kwenye sakata la uwanja anawatuhumu viongozi wa Wilaya ya Nyamagana eti wanatumia suala la kubinafsisha uwanja la kisiasa mwishowe viongozi wa CCM na wakashuka jukwaani wakamwacha akibwata hana jipya na hawezi kutoa tamko yaelekea hata yeye ni mmojawapo walovuta ten percent Bora Njolay angetoa tamko la msingi
Naona huyu apelekwe LINDI au RUKWa kama Njolay anastaafa
Nani Mkuu wa Mkoa wa mwanza sasa hivi?
......na hawa viongozi wanamuongoza nani? kwa nini hawataki kusikiliza matakwa ya wananchi?
Ogah
Kama unakumbuka Lowassa akiwa WM alikuwa kwenye ziara ya Wilaya ya Ukerewe Kijana mdogo wa shule ya msingi alimuuliza swali kwanini Mkuu wa Mkoa awe na vyeo vingi kama alivyo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (Engineer,Mbunge,Dr,Mkuu wa Mkoa,Mjumbe wa NEC,Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ya Mkoa yeye,aligombea pia CC akashindwa
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ni Dr James Alex Msekela kama sijakosea, unaweza ukapata Details zake kwenye web ya Bunge. Ni mbunge wa Tabora Kaskazini kama sija kosea.
Sasa tukirudi kwenye maada ya huo Uwanja, hivi haiwezekani kujenga majengo mazuri kuzunguka uwanja ili ziwe Office, Bank, Restaurant, maduka na makazi ya watu???? na katika mambo ya michezo yakaendelea?