SAKATA LA UMEME ZANZIBAR: Lawama kwa Serikali, Tanesco ama ZECO?

Hapa siasa tu hakuna chochote cha maana, CCM zanzibar bila CCM bara haitakuwepo, bali tutakuwa na vyama vingi vidogo vitakavyoanzishwa na wakiojitoa CCM Zanzibar. Hili alina mjadala kwani mara nyingi tunaona jinsi wanavyopingana hata wao ila wanaunganishwa na CCM bara.

Ila kwa CUF naona wanaweza ( sina uhakika) kuendelea kuwa pamoja kama watajitenga na CUF bara, kwahiyo CCM zanzibar wasilete jeuri kwani CCM bara ndo mbabe wao kwa CUF otherwise watakuwa na hari mbaya sana.

CCM bara ndo iliwasaidia kmteka msabaha na ndo maana wakamweka makao makuu badala ya kumpa cheo kule zanzibar, CCM bara imekuwa ikiwasaidia mambo mengi sana kwa mfano wakati kamando alipotaka kubadilisha katiba na kujiongezea muda ni CCM bara ndo walikataa, otherwise karume asingekuwa madarakani leo hii.

CCM bara imewasaidi kutuliza watu wa CUF kwa mihafaka hewa, kila mara baada ya uchaguzi lakini wangekuwa peke yao hakuna mtu wa CUF ambaye angewasikiliza kamwe.
 
Kikwete azidi kuwatesa Wahafidhina amewapeleka salaaam anaenda kutafuta kipuri Japan ,habari zakuhaminika zinasema Unguja huenda watarudishiwa Umeme Jumamosi kumbuka tu leo ni Jumapili. Kipuri kitatumwa kwa njia ya DHL.
Wahafidhina wameshaanza kutoa makelele na kusema Muungano gani huu si bora tungelikuwa na yale majenereta yetu ,wanarapu ile mbaya eti wanasema bora Pemba haya mambu wameshayazoea ,kwa kuwa Pemba hakuna umeme macho yao yanaona zaidi usiku kuliko mchana.
Wameanza kuhisi kuwa isije kuwa Kikwete analipiza kisasi kwa kupandishwa mkenge kule Butiama.
 
332rodi.jpg
 
Kuna tetesi Kikwete ameanza kujibu mapigo ya wahafidhina waliodai warudishiwe ASP kama CUF itajumuishwa kwenye Serikali ya Mapinduzi .Uvumi huo ambao unaonyesha kuwa maneno waliyoyatoa wahafidhina wa serikali ya mapinduzi dhidi ya wenzao wa CCM bara yamewagusa wengi ambao wanaita kuwa huo ni udhalilishaji wa hali ya juu ambao ulifanywa mbele ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano na Mwenyekiti wa CCM Mh.Kikwete ,kama alivyosikika Warioba akijibu jeuri za wahafidhina hao wa Serikali ya mapinduzi kuwa angeliwapa ruhusa hapo hapo Butiama wachukue ASP yao na wawaachie wao na CCM ili wakakumbane na dharuba za CUF huko visiwani ,akimaanisha kuwa bila ya nguvu za CCM Bara kutumika wahafidhina hao wangelikwisha kusahauliwa na kuwa wauza mbatata za urojo na pweza pale forodhani.
Inasemeka Unguja hakuna umeme leo ni siku ya tatu ,tayari maji hayapatikaniki mjini kwani shida hiyo iliondolewa kwa kuchimba visima vinavyotumia waterpump ambazo hutumia umeme ,pia mawasiliano yamekuwa duni kwani mobile simu zinahitajiwa kila baada ya matumizi.
Wahafidhina sasa wameanza kutumia toilet paper na wengine wameonekana wakijisogeza karibu ya pwanipwani ili kukidhi mahitaji yao dharura na wengine kelekea mashamba.
Nguvu za kuilazimisha na kuisemesha bara hawanazo kwani kuna kitu kimeanza kujulikana kama machafuko ya Butiama ,mbinu zilizotumika Kikwete hakuambiwa tokea mwanzo na jinsi walivyomzidi kete kwa mazungumzo Kikwete aliona ni rahisi na alidanganywa kwamba hakuna tatizo,lakini muda si mrefu aling'amua wakati maji yameshamwagika na hasira zake ndio zitakazo wakosesha raha hili genge la wahafidhina wa serikali ya mapinduzi. Wanasema ameanza kuwakatia umeme japo siku nne na mengine yatafuata baadae.

Mwiba maneno yako ni kweli kabisa na kama ukitazama ile DVD ya kule Butiama utashangaa jinsi gani wale CCM ZNZ wlaivyo mbully MUUNGWANA to the extent akiishia kupitisha vimemo ili CCM BARA wawajibu wahafidhina.

Kilichonishangaza ni kwa nini JK ahakutumia uwezo wake na nguvu zake ya kidola kumpa dress down krume na maswahiba zake toka Unguja walikuwa mamegang up agaisnt me

kingine cha kushangaza ni jinsi CCM bara walivyooamua kumchunia MUUNGWANA lakini i can understand kwa nini maana mijitisho iliyokuwa ikitolewa na wahafidhina inatisha bwana..unajua walikuwa wako tayari kuuvuinja Muungano na pale nikajua kuwa Muungwana uwezo wa Leadership hana hata kidogo..yuko half way ngwe yake ya kwanza lakini inaonekana tayari keshakuwa LAME DUCK President

halafu eti Membe anataka kuwa rais atawaweza wahafidhina na jeuri ile?
 
Kibunango,

Hili la Umeme wa Upepo lisiishie Zanzibar tuu, hata Bara kunahitajika kanza mikakati ya kutengeneza umeme wa upepo na jua.

Kwa Bara mikoa ya Dodoma, Singida na Shinyanga inafaa sana kwa kuwa umeme wa upepo. Nimewahi kupita katika mikoa hiyo na kukutana na windmill kwa ajili ya kusukuma maji, na inafanya kazi karibu mwaka mzima. Tatizo la wind power ni gharama kubwa katika ujenzi wake(aidha katika kutafuta sehemu muafaka kwa kuweka hizo wind power), aidha ukiondoa kelele ni nzuri kwa mazingira yetu.

Inaekela nyinyi bado mko nyuma hivi hamjaona zile wind farms zinazopelekwa Iringa?

wenzenu tayari washajipanga na tayari mwezi ujao wafungaji wanakuja toka Ujerumani
 
kusudi haiambiwi pole na huruma hailei mwana........kama JK haijui misemo hii nitaamini kama kweli yeye si mzaramu kama anavyojipachika!

acha yamfike, anawalegezea sana, wamemtolea jeuri utasema mtoto mdogo na yeye ameshindwa hata kuwakemea!
 
siamini kabisa. wenzetu wa cuf kila kitu ni siasa tena za kipropaganda

kosa la kiufundi hugeuzwa la kisiasa.

basi Karume asiumwe katishwa maji yasikatie au umeme usizimike wanaonyeshwa jeuri.

mtabaki hivyo hivyo mafisi fupa hamling'ati ng'o na mwiba huo utawachomeni kubaya

Mkubwa chukua 5 hiyo. Maana sasa hivi hata mitambo ikikorofishwa watu wanalimuvuzisha kwenye Siasa na kulaumiwa Mkuu wa Kaya.
 
Kuna habari kwamba huenda mambo mpaka wiki ijayo ,wataalamu kutoka Norway hawakuridhika na picha na hivyo wameona kwanza waone ndio wajue kifaa cha kuagizwa,watakuja na kutazama kifaa halafu waagize .kile kilichopigwa picha kina matatizo ya size hivyo kama ndicho kinacholeta tatizo na kitafiti watakifunga ila ikiwa size inameta basi watakirudisha kwenda kukichonga au kuleta kipya.
Tukirudi kwenye mazungumzo baada ya habari ,habari kutoka Ikulu Zanzibar zinasema sasa wahafidhina maji wanaita mee.Wakati kutoka tetesi kutoka Ikulu za bara zinasema Muungwana amewataka waseme wamekoma na hawatasubutu tena kutoa ufezuli ,wahafizina hao ambao walikuwa wameongozana kwenda kuoga baharini nyuma ya ikulu yao wamesikika wakiimba nyimbo za kusifu mapinduzi.
 
Z`bar gizani siku 21

2008-05-26 08:59:32
Na Joseph Mwendapole

Wataalamu wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) na wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), jana walikwama kutatua tatizo la ukosefu wa umeme visiwani hapa kutokana na kukosa vitendea kazi.

Kutokana na hali hiyo, mashirika hayo yamewaagiza wataalamu wake kufuata vifaa jijini Arusha wakati wakisubiri wataalamu wengine kutoka nchini Norway.

Akizungumza Visiwani hapa jana, Mhandisi wa Matengenezo kutoka TANESCO, Bw.. Josephat Gandie, alisema zoezi la matengenezo limesimama hadi vifaa vitakapowasili.

``Hata hivyo tunazingatia pia ushauri wa Rais Amani Abeid Karume, aliyetuambia tufanye matengenezo kwa ushirikiano wa ZECO, TANESCO na Wanorway,`` alisema.

Alisema wakati wakiwasubiri wataalamu kutoka Norway, vifaa vimewakwamisha kazi hiyo kutokana na kutopatikana Zanzibar na kwamba tayari TANESCO wakishirikiana na ZECO, wameviagiza Arusha. Bw. Gandie, alisema wataalam kutoka nchini Norway, wanatarajiwa kuwasili leo au kesho tayari kwa kuanza matengenezo.

Ofisa Uhusiano wa ZECO, Bw. Salum Abdallah alisema kuwa kifaa kilichoharibika kinaitwa Submarine Cable na kitatengenezwa kwa wiki tatu nchini Norway.

``Tulipeleka picha kwa kampuni ya Neksans Ltd ya nchini humo ambayo wamesema kuwa, kifaa hicho kitaweza kukamilika baada ya wiki tatu kwa kuwa ni oda maalum tumekubaliana nao lakini tunaendelea na jitihada mbalimbali kuhakikisha umeme unarejea,`` alisema.
-----------------------------
Nilisema wiki ijayo kumbe siku ishirini na moja ,jamani kuna tatizo kifaa kinaitwa submarine cable kitaagizwa arusha mafundi wanatoka Norway ,Yaani Muungwana unajuwa kuwatia adabu wahafizina ,hii ndio kasi na ari mpya submarine cable kuitwa kipuri ambacho kinapatikana Arusha vijjini ,mwandishi amezidi kuwawacha hoi wahafizina sasa hawajui wasuke au wanyoe .
Hapa kuna mtu tu ambae anawatia adabu wahafizina yaani hiyo habari ya kifaa na mafundi ni mambo mbali mbali na hayalingani ,mnataka kutwambia kuwa kifaa hicho kipo lakini hakuna anaejua kukifunga.
Kama kuna wachambuzi wa kusoma kwa kina waisome hii habari ya mwandishi ndipo mtajua kama hii kitu ni well planed ,na jamaa wanababaishwa .Karume anasema mafundi washirikiane si bora kwanza angeitisha kura ya maoni kama mafundi wanakubali kushirikiana.
 
Mwiba maneno yako ni kweli kabisa na kama ukitazama ile DVD ya kule Butiama utashangaa jinsi gani wale CCM ZNZ wlaivyo mbully MUUNGWANA to the extent akiishia kupitisha vimemo ili CCM BARA wawajibu wahafidhina.

Game Theory, nimetafuta sana hiyo DVD sijaipata. Tafadhali sana naomba unisaidie namna ya kuipata.
 
Hii habari ya kuagiza kipuri, mara mafundi toka Norway, mara kipuri toka Arusha, mara kipuri siku 21 kukitengeneza - ni ubababishaji mtupu. Naanza kuona mantiki ya hoja zako Mwiba.
Kwa nini wanajikanganya kiasi hicho?
 
Hii habari ya kuagiza kipuri, mara mafundi toka Norway, mara kipuri toka Arusha, mara kipuri siku 21 kukitengeneza - ni ubababishaji mtupu. Naanza kuona mantiki ya hoja zako Mwiba. Kwa nini wanajikanganya kiasi hicho?
Acha upofu.....ni ushauri tu
 
Acha upofu.....ni ushauri tu
Ndugu sio ushauri ,siri imeshafichuka ,sasa watu wa upande wa Muungwana wamesema wahafidhina ni watukutu hawasii na wala hawafuati yale wanayoyataka wao tu,sasa kunakuja twisted mamboz ,eti watu wa Muungwana hawa Tanesco waliwaambiwa watu wa wahafidhina kuwa wazime swith (main switch ) jamaa wakasema washeni hivyo hivyo ,watu waKikwete wakasema kumbe nyinyi wapemba ni wakaidi sana basi kazi kwenu walisahau kama umeme unaenda Unguja wakauwasha kwa kasi mpya maswichi ya wahafidhina yote yakachawanyika tatizo kule hawana elimu ya kutosha wameagiza submarine cable wakati vitu vinavyohitajika ni socket na switch gear ,hivyo ambavyo vinapatika Arusha.
Ili kuwakomoa wahafidhina jamaa wamekwenda kwa kutumia njia ya barabara kwenda kufuatilia vipuri hivyo wakati wangeliweza kukodi ndege ndogo tu na kuchukua muda wa masaa matatu ukizingatia tatizo linahusu kisiwa kizima cha Unguja.
Sasa baadhi ya wataalamu wamesema kazi hii inaweza kuchukua muda mrefu kuliko inavyofikiriwa hasa ikizingatiwa ikiwa hitilafu imesababisha na nyaya zinazopita chini ya bahari kuathirika.
Ila kuna wapenda amani wanaosema ikiwa umeme wa kukodi tabu yake ni hii bora wasife masikini kuna waliozidi kwa kusema Muungwana anaonyesha nguvu zake na wahafidhina wakome kujidai na kusema kuwa warudishiwe ASP yao ,shuguli zote za mabenki na serikali kwa ujumla ni za kusua sua.
 
Hao mabulls wenyewe wanasemaje kuusiana na kutokuwa na umeme siku zote hizo, wanamkakati gani wakati hicho kifaa kinasubiriwa, ina maana hawakuwa hata na spare walisubiri kife ndowaagize?
 
Ndugu sio ushauri ,siri imeshafichuka ,sasa watu wa upande wa Muungwana wamesema wahafidhina ni watukutu hawasii na wala hawafuati yale wanayoyataka wao tu,sasa kunakuja twisted mamboz ,eti watu wa Muungwana hawa Tanesco waliwaambiwa watu wa wahafidhina kuwa wazime swith (main switch ) jamaa wakasema washeni hivyo hivyo ,watu waKikwete wakasema kumbe nyinyi wapemba ni wakaidi sana basi kazi kwenu walisahau kama umeme unaenda Unguja wakauwasha kwa kasi mpya maswichi ya wahafidhina yote yakachawanyika tatizo kule hawana elimu ya kutosha wameagiza submarine cable wakati vitu vinavyohitajika ni socket na switch gear ,hivyo ambavyo vinapatika Arusha.
Hapo unguja wanaishi ccm pekee?
 
Watalaamu wa kutengeneza kifaa cha umeme Zanzibar waondoka

2008-05-27 10:16:31
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar

Wakala wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ambao walikuwa mjini hapa kufanya matengenezo ya kifaa cha umeme kilicholipuka, wameondoka baada ya kazi hiyo kusitishwa.

Imeelezwa kuwa, wataalamu hao wameondoka hadi wataalam wanaosubiriwa kutoka Norway watakapowasili mjini hapa ambapo watashirikiana kufanya matengenezo hayo.

Mhandisi kutoka Tanesco, Bw. Josephat Gandye alithibitisha hayo jana kuwa wataalam hao wameondoka Zanzibar kwa kuwa kazi hiyo imesimama kwa muda.

`Tumelazimika kuondoka kwa vile kazi ya matengenezo imesimama hadi hapo wataalam toka Norway watakapokuja ndipo tutakapoungana nao,``alisema.

Akielezea chanzo cha kulipuka kwa waya huo alisema kuwa hakijajulikana lakini alisema umeme ulipokatika Tanzania Bara na kurejea ulikuwa hauna nguvu.

Wakati huo huo, ofisa uhusiano wa Shirika la Umeme la Zanzibar (ZECO), Bw. Salum Abdallah amesema hadi jana hawakuwa na uhakika iwapo wataalam hao kutoka Norway watawasili lini mjini hapa.

``Tunaendelea kuwasiliana nao, isipokuwa siwezi kusema watafika lini ingawa tuna matumaini kuwa watafika leo au kesho,`` alisema.

Hata hivyo, alisema kukosekana kwa huduma hiyo kumeleta athari kubwa kwa vile wezi wamecharuka kuiba nyaya za umeme.

Aliyataja maeneo yaliyokumbwa na matatizo hayo kuwa ni kiwanda cha maziwa cha Maruhubi, Mwembe Makundi ambapo zaidi ya mita 400 za nyaya zimeibiwa.

Aidha alisisitiza umuhimu wa wananchi kulinda njia za umeme kwa vile athari zitakuwa kubwa.

Baadhi ya wananchi wameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuangalia uwezekano wa kuomba msaada wa jenereta kutoka Tanzania Bara kwani upo umeme wa kutosha.

Hata hivyo, Bw. Burhan Msoma wa Kikwajuni alisema Zanzibar ina fedha za kutosha kununulia jenereta ili zitumike kuondoa tatizo la umeme na maji.

Wakati huo huo, Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) imelazimika kuanzisha kituo cha kugawa maji kwa wananchi katika eneo la Msikiti Mabluu, mjini Unguja.

Mkurugenzi wa ZAWA, Bw. Ahmed Salim alisema hatua hiyo imechukuliwa ili kuwapunguzia usumbufu wakazi wa visiwani.
Aliongeza kuwa mamlaka yake ina mpango wa kununua jenereta.

SOURCE: Nipashe
 
Wakulu sasa hii kali.Sasa umeme utarejeshwa lini Unguja?Mwiba naona uko online sasa haya mambo yako ni kweli lakini au???Hii haijawahi kutokea!!!
 
Mwiba maneno yako ni kweli kabisa na kama ukitazama ile DVD ya kule Butiama utashangaa jinsi gani wale CCM ZNZ wlaivyo mbully MUUNGWANA to the extent akiishia kupitisha vimemo ili CCM BARA wawajibu wahafidhina.

Kilichonishangaza ni kwa nini JK ahakutumia uwezo wake na nguvu zake ya kidola kumpa dress down krume na maswahiba zake toka Unguja walikuwa mamegang up agaisnt me

kingine cha kushangaza ni jinsi CCM bara walivyooamua kumchunia MUUNGWANA lakini i can understand kwa nini maana mijitisho iliyokuwa ikitolewa na wahafidhina inatisha bwana..unajua walikuwa wako tayari kuuvuinja Muungano na pale nikajua kuwa Muungwana uwezo wa Leadership hana hata kidogo..yuko half way ngwe yake ya kwanza lakini inaonekana tayari keshakuwa LAME DUCK President

halafu eti Membe anataka kuwa rais atawaweza wahafidhina na jeuri ile?

mkuu hebu tuwekeeni na cc tuone hiyo DVD.halafu pale ktk kikosi cha wahaFIDHINA amekosekana Brg Gen MWAKANJUKI,na kama angekuwepo basi duh pangekwua patamu hapo.
 
Back
Top Bottom