Sakata la umeme nchini sasa limeingia ktk sura nyingine - LUKU

Hhm

Member
Apr 28, 2010
69
14
Habari za asubuhi wana jamii wenzangu, hivi, mna habari kuwa kama tatizo halitatatuliwa Leo itakuwa ni siku ya nne tangu kukosekana kwa mauzo ya umeme nchi nzima...na sababu network hakuna.

Hii nimeshuhudia mwenyewe jana mara baada ya kuzunguka mji mzima na kukuta kundi la watu wakisubiri huduma ambayo haijulikani itapatikana au laa...hali watu wakiwa wenye hasira kali walilaani na kutoa maneno makali sana jambo ambalo hata mimi nilijikuta napandwa na hasira juu ya sirikali hii ambayo kimsingi inaonekana wazi imevurugika na kukosa mwelekeo. Ambapo sasa naweza kusema kuwa, pamoja na kuwa na mgao mkali wa umeme bado hata upatikanaji wa umeme huo mdogo ni wakusuasua.

Hivi unapokwenda kununua umeme halafu unaambiwa network hakuna, inakuja na kuondoka....jambo lakusikitisha sana, jana nikiwa katika kuhangaika kutafuta umeme nilikutana na shuuda mmoja aliyekuwa anatafuta umeme tangu majuzi na kushuhudia kuwa hawa mawakala wanaouza umeme wa luku wamekuwa wakidai rushwa ili mtu apewe favour Kila network inaporudi na wamekuwa wakitoa 5000/- .

Hii imenisikitisha sana sana.

Sijui siku ya leo itakuwaje Ndugu zangu ila habari ndo hiyo.
 
Hapa bongo panatisha sana ukifikiria lazima utalia..

Hongereni CCM na sirikali yenu juu ya nishati na maji..
 
Mimi nashindwa kumuelewa mleta hii topic, Umeme wenyewe hakuna sasa wewe unataka uuziwe unity ili uzipeleke wapi?
 
Habari za asubuhi wana jamii wenzangu, hivi.mna habari kuwa kama tatizo halitatatuliwa Leo itakuwa ni siku ya nne tangu kukosekana kwa mauzo ya umeme nchi nzima...na sababu network hakuna.

Hii nimeshuhudia mwenyewe jana mara baada ya kuzunguka.mji mzima na kukuta kundi la watu wakisubiri huduma ambayo haijulikani itapatikana au laa...hali watu wakiwa wenye hasira kali walilaani na kutoa maneno makali sana jambo ambalo hata mimi nilijikuta napandwa na hasira juu ya sirikali hii ambayo kimsingi inaonekana wazi imevurugika na kukosa.mwelekeo, ambapo sasa naweza kusema kuwa, pamoja na kuwa na mgao mkali wa umeme bado hata upatikanaji wa umeme huo mdogo ni wakusuasua.

Hivi unapokwenda kununua umeme halafu unaambiwa network hakuna, inakuja na kuondoka....jambo lakusikitisha sana, jana nikiwa katika kuhangaika kutafuta umeme nilikutana na shuuda mmoja aliyekuwa anatafuta umeme tangu majuzi na Lu.ishuhudia kuwa hawa mawakala wanaouza umeme wa luku wamekuwa wakidai rushwa ili mtu apewe favour Kila network inaporudi na wamekuwa wakitoa 5000/- . Hii imenisikitisha sana sana.

Sijui siku ya leo itakuwaje Ndigu zangu ila habari ndo hiyo.

Wewe unafikiri mmewacho, olea kwenye upatakanaji wa umeme fedha za DHARURA ZITALIWAJE??
 
Kwani ni lazima msubiri network ya tanesco wakati moto upo juu ya paa la nyumba yako? Unachoweza kufanya ni kuunganisha umeme wako kwenye switch direct. Wakikuuliza tanesco kwa nini umefanya hivyo, waambie kwa kuwa nchi hii kupitia taasisi zake hawatendi tena haki, nasi tumeamua kutoitenda kwa niaba yao. Pia wape pesa inayolingana na wastani wa umeme unaotumia kwa mwezi. Kosa ni lao tanesco na wala sii lako.
[Za mbayuwayu usisahau kutia zako].
.
 
Mkuu cheki na vishoka wakupe kitu live nchi ishauzwa hii kama noma na iwe noma
 
HIVI REJAO CCM WAMEKUPA NINI?PAMOJA NA MATATZ YOOOTE WE UPO NAO TUU AU WE NI RZ ONE UMEFICHA ID HEHEHEHE SIKU UKISHTUKA UTAKUWA UMECHELEWA NA HUNA PA KUHAMIA
Kwanini ujiumize kukimbilia matatizo?
Siku Upinzani wakijipanga, wakawa na sera za maana na zenye tija..nitawaunga mkono!
Mtu mwenye akili zako huwezi kusupport vyama vya kuhuni kama CDM!
 
Kwanini ujiumize kukimbilia matatizo?
Siku Upinzani wakijipanga, wakawa na sera za maana na zenye tija..nitawaunga mkono!
Mtu mwenye akili zako huwezi kusupport vyama vya kuhuni kama CDM!

Kwa hiyo CCM wana sera nzuri siyo?Una matatizo katika mfumo wako wa kufikiri.Wewe unaona nchi inatumbukia shimoni( kila siku afadhali jana)bado unakomaa,mijitu mingine bana au ndo nyie mnaofikiri kwa .................
 
Mi nipo kijijini bwana, umeme haunifai kitu. jiko la kuni, pasi ya mkaa, ximu ya betri size AA. CCM hoyeeeee!
 
mi jana nimelala giza,ila nimezoea maana hata umeme wenyewe ndo hivyo tena
Mimi sina umeme maana natakiwa ninunue nguzo tatu ili uingie kwangu jana nimelipia nimeambiwa by next three days utawaka, hivyo nitaingia rasmi kwenye changamoto ya wapi pa kununua umeme, naipenda sana Tanzania lakini basi tuu, nisiseme mengi nisije itwa mdini na mchochezi. Hivi inaingia akilini kununua nguzo moja kwa wastani wa Milioni moja na zaidi? ili niweze kupata huduma ya umeme na ikumbukwe kwamba nguzo hizo zitaendelea kuwa mali ya Tanesco.
 
Back
Top Bottom