Sakata la Polisi kukatwa posho elfu 50: Mnyika ishike pabaya wizara mpaka kieleweke

Original Pastor

JF-Expert Member
Nov 14, 2007
1,274
50
Wana JF lile sakata la Polisi kukatwa posho yao ya TSHS 50,000 Limeishia wapi? Mh, Mnyika wasaidie hawa watakutetea sana hawa Ingawa waliuwa watu wetu kule Arusha.

Wana JF walinda amani wetu wanakatwa posho bila sababu za msingi na zinaingia kwenye akaunti ya Waziri Sasa sijui Itakuwaje? Hawa tukiwatetea watatufaaa uchaguzi 2015 kupalilia shamba.

Washapiga na mikwara huku:
mkwara1.jpg

mkwara2.jpg

mkwara31.jpg

 
unalosema ni kweli,kwani tangu mwaka juzi posho yao ya chakula ilitakiwa iwe 150,000/= lkn zinakatwa na kuingizwa kwenye akaunti za vigogo wa wizara. hivi ss wanalipwa laki moja tu,sakata hili lilianza tangu kipindi cha IJP mahita ambapo posho ilikuwa inakatwa 25,000/= ambapo askari walikuwa wanalipwa 75,000/= badala ya 100,000/= ambapo ilisemekana hiyo 25,000/= inapelekwa kwenye ujenzi wa nyumba za polisi. Huo ni uongo kwani mwenye jukumu la kujenga hizo nyumba ni serikali kupitia wizara ya ujenzi!

Pia mnyika naomba uhoji pesa zinazotokana na malipo ya askari polisi wetu walioko ulinzi wa aman huko darfur zinapelekwa wapi kwani kwa mujibu wa taratibu,Umoja wa Mataifa unailipa nchi inayochangia askari wake kwenye ulinzi wa aman,ifahamike kuwa kila askari anayelinda aman nchi yyt,nchi inalipwa pesa na zinakuja nchini kwake. pesa hii ni tofauti na posho anazolipwa yy mwenyewe kujikimu huko aliko! kuna ufisadi mwingi wizara hii!
 
hizi nazo zimeenda kwa shimbo ama safari hii kwa MWEMA??
 
Mbona maelekezo yanatolewa na sacp (ruvuma) na sio igp / afisa utumishi wa wizara husika?
Please let someone responsible clear the dought. We need no blaa! Blaa! About seroius issues like this
 
Soma vizuri neno kwa neno,barua hii imetoka kwa kamada wa Mkoatu wa kwa,maagizo haya yametumwa kwao nao wametoa kwa wadogo watu wao.

Tusubiri wanaweza kutuletea taarifa zaidi.si wapo humu!!!!!!!!!!!!!!!!
 
hii kali tusubirie tuone nini kumbe hata polisi wamewachoka sasa sijui wataishije maana ndio walikuwa wanawatetea
 
Tena imekuja wakati mzuri maana IGP ameomba akutane na wabunge Dodoma siku ya Jumapili, August 14, 2011 awafunde kuhusu UTII WA SHERIA BILA KULAZIMISHWA.
 
Kwa hiyo kuna posho ambazo askari wamekuwa wakidhurumiwa!ipo siku dhuruma itawaponza CCM!!
 
Watanzania sasa wameamka kila kona maana barua kama hii toka ndani ya ofisi ya kamanda imeanikwa mtaani kila mpita njia anaiona sirikali ya Kikwete blabla tu.

Kudhibiti hali hii tena ipo kazi, vinginevyo serikali inalazimishwa na umma kujenga utandawazi.
 
ukitaka kujua polisi na JWTZ hawaipendi ccm,nenda mwanza,katika kituo cha kupigia kura mabatini ambapo ndipo ilipo kambi ya polisi,masha alipata kura 4,katika kituo cha kupigia kura lugalo dar kikwete alipata kura kumi!
 
Kwa huo mshahara wanaoutoa hautoshi kwa mapolisi, hebu fikiria, asilimia kubwa ya polisi ndani ya jeshi letu siku hizi ni vijana, wakiwa kama vijana nao pia lazima wanakuwa na mahitaji na matamanio mengine kama walivyo vijana wenzao wasio mapolisi, mbali na hao vijana wazee pia nao hawawezi kukaa kambini maisha yao yote, ni lazima watataka kujenga nyumba zao na kadhalika baada ya kustaafu, hivyo kutoa mshahara mdogo kwao ni sawa na kuwaambia kwamba nendeni mkaongeze kipato chenu kwa kuomba rushwa. Serikali inatakiwa ikumbuke na kuwajali hawa watu sababu ndio wanaotakiwa kulinda usalama na mali za wananchi. Mimi kwa maoni yangu nadhani hapa lazima kuna mtu atakuwa amegusa maslahi ya mwingine, na njia pekee iliyobaki kwa viongozi wetu katika kutatua matatizo ni kutoa vitisho. mimi nawaambia polisi msitishike, piganieni haki yenu kufa na kupona, msiridhike kuomba vijirushwa mbuzi huko mitaani, sababu tunasikia wengine mnaomba mpaka rushwa ya Tsh 100. PIGANIENI HAKI YENU!!
 
Hakuna aliyesalimika na uwizi na unyanganyi wa haki unaoendeshwa na mfumo uliopo,tuungane kuupinga ukoloni mweusi
 
Kwani Shimbo ndio CDF?

Au ndiyo yele yele Abdulrahaman Shimbo na Said Mwema.

UDINI MTUPU

Salaam alekhum Sheikh ubwabwa,Pole kwa saumu ila usijali coz ukimaliza mfungo kwenye ile sherehe yako ya kuazimisha siku 30 za kushinda njaa tutakuchinjia yule mwanakondoo wa maajabu mwenye baka leupe ubavuni.
 
Back
Top Bottom