Sakata la pension: Waziri kivuli wa kazi wa CHADEMA kaingia mitini

thread critic

Member
Jul 17, 2012
71
14
hili sakata la amendments za pension tulitegemea kusikia maoni toka kwa waziri kivuli wa kazi wa CHADEMA waje na hoja mbadala lakini kimya

hajulikani ni nani na haieleweki kwa nini kaingia mitini

hii inaashiria nini?
 
hili sakata la amendments za pension tulitegemea kusikia maoni toka kwa waziri kivuli wa kazi wa CHADEMA waje na hoja mbadala lakini kimya

hajulikani ni nani na haieleweki kwa nini kaingia mitini

hii inaashiria nini?

Sasa unafikiri atasema nini wakati watu wamekaa tu NDIOO NDIOOO!! Na mi nadhani zile ndio wameaplify kitu pale sio bure. Yaani hadi utumbo kama huu waliitikia ndio kweli?
 
Nadhani waliosema Dioooo wameshinda,napenda kuchukua fursa hii kumpongeza mh wazari kwa kazi nzuri.
 
Wanaodhani CDM ni muarubaini wa matatizo ya waTanzania wanakosea sana.

Muarubaini wa matatizo ya watanzania ni watanzania wenyewe. Lakini wa kuwasemea? Jibu lipo pale ulipopigia mstari
 
hata cdm wakiingilia kati ,je wananchi wako tayari ku support?tuache unafiki!
 
Based on the fact, kwa hii ishu ya pensheni wabunge wa chadema walipigwa bao la kisigino. Mswada ulipitishwa bungeni April 13, na Beruberu akauweka mkono fasta. Mpaka leo wapo kimya! Au chadema na wao hawa shida na kura za wafanyakazi?
 
Wafanyakazi wa Tz ndio wapiga kura na wapiga debe wa ccm so wanavuna walichopanda. Maoni ya CDM yatasaidia nini wakati watu wameliwa tayari?? next time enyi watanzania fanyeni mabadiliko ya kweli kwa maslahi yenu. Ni nani hutumika kupanga mikakati ya ccm? nani husafirisha chumvi na kanga kwenda vijijini? Wafanyakazi wa tz wana sura mbili na hili litawagharimu sana safari hii. CDM wakipiga kelele wafanyakazi wanawachungulia madirishani na kusubiri kuona kitakachotokea badala ya kuwaunga mkono. Nafurahi kwa sababu sheria hii ihawahusu pia wale mabingwa wa mabomu na risasi za moto.
 
Wafanyakazi mnasubiri nani aje awalilie kilio chenu, mnaleta vyama vyenu nendeni mahakamani au muandamane mpigwe mabomu, sheria hii nzuri sana hawahusu wabunge , wala jk.mtabaki kusuburi chadema wawatetee wakati kura mnapigia ccm.kama hamko pamoja na ccm mbona Payee imeongezwa mkono kimya tu, ili nalo kaeni kimya.
 
mnawaonea bure tu,mswada ulipitishwa mlango wa nyuma,nyie c mmeona hata magamba wameushtukia wanataka kureviiew,chadema wapo makini hawawezi kupitisha huo ujinga wakuu!
 
Back
Top Bottom