sakata la mwanamke aliyenyang'anywa mtoto na mhindi; ITV na CHANNEL 5 wafungwa mdomo

Tewe

JF-Expert Member
Jan 11, 2008
1,101
813
Akitangaza katika taarifa ya habari ya ITV saa mbili, Fatma almai nyangasa amesema ITV na Channel 5 wanaomba radhi kwa kumhoji hakimu aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo na kuriport matukio wakati kesi hiyo inaendelea; Swali je mhindi aliyenyang'anya mtoto kwa kutumia fedha kazipenyeza hadi mahakamani?
Baada ya kufanywa kuwa siri sasa je yule mdada atatendewa haki au ndio ameumia?

Karibuni wadau
 
kumhoji hakimu sio tatizo tatizo liko kwa hapa Tanzania ukitaka kumhoji hakimu
lazima upate kibali kutoka kwa msajili wa kanda mfano msajili kanda ya dar es salaam.
Huu utaratibu upo ila umepitwa na wakati. unawanyima waandishi uhuru
wa kupata habari za kimahakama na kuwajuza wananchi.
kama hakimu alichemka lazima ahojiwe na kuhojiwakwake
hakujaingilia uhuru wa mahakama au kuingilia mchakato wa kesi husika.
Tatizo la tanzania kila kitu ufuate taratibu hata kama ni mbovu ndio maana tuko nyuma kila kitu.
nawasihi wanaharakati mchunguze na mfuatilie hiyo kesi kwa undani ila kama hakimu alihusika achukuliwe hatua ila kama alikosea kisheria atalindwa judicial immunity ya mahakimu.
ITV MMEOMBA MSAMAHA KWA KOSA LIPI???????????
MBONA CNN,BBC WANATANGAZA LIVE KESI ZIKIENDELEA KWANINI TANZANIA TUNAFICHA???
SHERIA HIZI ZIMEPITWA NA WAKATI SASA TUPO KATIKA TEKNOLOJIA MPYA.
 
Mahakama siku hizi ni mdebwedo kwenda mbele si mmesikia ya mahalu
 
Kaka maigizo,MbOna Muhindi amemchua Mtoto,na dada akiendelea kupiga kelele hampati kabisa.Watanania na wajua Sheria Tumsaidie yule Dada
 
Haki ataipata MAHAKAMANI. Kwanza ni kosa la jinai kuongelea kesi iliyoko mahakamani, nje ya mahakama. ITV lazima waombe radhi, ingawa Mkuu wa kaya hatakiwi kuomba radhi kwa kuongelea kesi ya madaktari pamoja na ile ya waalimu nje ya mahakama.
 
naunga mkono swala la kumsaidia huyu dada ili apate mtoto wake kwani uchungu wa mwana aujuae ni mzazi,hakim aliyesimamia hiyo kesi abadilishwe kwani alipewa rushwa ili ampendelee huyo muhindiiiiii
 
Akitangaza katika taarifa ya habari ya ITV saa mbili, Fatma almai nyangasa amesema ITV na Channel 5 wanaomba radhi kwa kumhoji hakimu aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo na kuriport matukio wakati kesi hiyo inaendelea; Swali je mhindi aliyenyang'anya mtoto kwa kutumia fedha kazipenyeza hadi mahakamani?
Baada ya kufanywa kuwa siri sasa je yule mdada atatendewa haki au ndio ameumia?

Karibuni wadau

hii bhana bila hata kumung'unya maneno ni JEURI YA PESA. Mi narudia kusema kila siku hii nchi tunakoelekea sasa hivi, itafika mahali mwenye pesa atafanya lolote kwa mnyonge na mnyonge hatapata wa kumtetea. ki-uhalisia kabisa hakuna utawala wa sheria kwenye hii nchi. kilichobakia ni wanyonge kuingia barabarani kubadili utawala wa hii nchi. HII NCHI TUNAKOELEKEA NI KUBAYA HAIJAPATA KUTOKEA KAMA TUTAENDELEA NA SERIKALI YA CCM. kwa nini SHERIA ISILIMALIZE KWANZA SUALA LA HUYO BINTI KUNYANG'ANYWA MTOTO KABLA YA KUWANYAMAZISHA ITV????? WALE WAHINDI WAMEGHUSHI VYETI VYA HOSPITALI KUONYESHA ETI YULE BINTI ANA MATATIZO YA AKILI, MBONA MAHAKAMA HAIKUWATIA HATIANI KWA KUMDHALILISHA BINTI WA WATU???? HILI LI NCHI NI LA;
rushwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
rushwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
rushwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

MPAKA INAKERA, HAKYANANI HUKO MBELE YA SAFARI WANYONGE TUTACHINJWA HADHARANI HUKU MAHAKAMA IKITABASAMU BILA HATA KUFIKIRIA KAMA KUNA SHERIA YA KUTENDA HAKI. MAHAKAMA IMEGEUKA MACHINGA INAUZA HAKI ZA WANYONGE KWA WENYE PESA KWA BEI YA JALALANI KABISA.

MLAANIWE NYIE SERIKALI YA CCM.
 
Tanzania inapoelekea si kuzuri, Ukiwa na hela hata kama mjinga basi wewe ni sahihi, Tuache ulimbukeni sasa apo msamaha ni wa nini? kama hakimu anaelewa sheria vizuri ilibidi aonyeshe confidence kwa mwaandishi wa habari kua hairuhusiwi kuhoji kesi inayoendelea badala yake akajitoa kwenye kesi. HATA IVYO VITABU VYA SHERIA VIMEANDIKWA NA WATU PALE AMBAPO WATU TUNAONA SHERIA IMEPITWA NA WAKATI AU INAKANDAMIZA NI LAZIMA TUSEME HATUWEZI KAA KIMYA ETI KISA IMEANDIKWA KWENYE KITABU
 
Mbona kesi za kina costa mahalu zinatolewa hukumu! Je? Hizi kesi nyingine zinaishia wapi? Tz hamna mahakama itabidi kwenye katiba kipitishwe kipengele tuwe tunashtakiana icc sasa, hawa wa hapa ni mahakama ya kuficha maovu
 
Kama wahindi sasa wanaiweka mahakama kwenye kiganja kazi ipo! Bado kuiweka ikulu kwenye pochi! Hata kariakoo skuizi imekosa weusi, khaaaa! Inabidi tuanzishe m4c kuhusu wahindi tu,mana ni mabazazi sana hawa.
 
Back
Top Bottom