Sakata la Million 300 Lawaka moto Voda, Kigoma all star wajieleza!

Red one

Member
Apr 22, 2011
99
26
Katika kile kinachoendelea kwasasa kwenye sakata la mgombea Urais 2015, kampuni ya simu za mikononi ya husika katika maandalizi hayo yenye Lengo la kumsimamisha mgombea Binafsi ama Mgombea huyo akagombee kupitia ADC na ndiyo maana ADC imewekwa Rangi za Chadema maana mgombea huyo atatokea Chadema na kujiingiza kwenye kambi hizo.

Ilikuwa ni siku mbili kabla ya Tukio la Kigoma all star kwenda kufanyika ndipo wanamitandao hawo walipoenda Arusha kukutana jinsi ya kuendeleza mikakati hiyo baada ya kigoma, walikutana kwenye hotel ya Mount Meru hotel watu ni mmoja anayehusishwa na sakata la Urais 2015 kutokea Upinzani na Mwingine ni yule mnyonyaji wa wasanii Tanzania na msimamizi wa kituo kimoja cha Redio kwasasa kina mpaka Runinga.

Mtandao huo wenye lengo la kudhoofisha Upinzani kwakutumia wanamziki hawo wanaowika kwasasa kwa kigezo cha Kigoma all star na kutaka kuzunguka nchi nzima kwaajili ya kujijenga kupitia vijana, inaelezwa kwasasa mabosi wa Voda wameanza kukinzana kuhusu faida watakayoipata kupitia project hiyo.

Vile vile uchunguzi wa mambo unaendelea kuchunguza kwa kupata Data za picha pamoja na vikao vinavyofanyika mara kwa mara na vile vilivyofanyika kwa lengo la kuanzisha ADC. Mchakato huwo ukikamilika hivi karibuni tutamwaga data hapa kwa majina na sehemu walizokutana, japokuwa mtandao huu upo mpaka kwenye mamlaka ya nchi kwaajili ya kuhakikisha upinzani haufiki 2015.

Tutajitahidi kuweka na majina ya watu wa mamlaka wa nchi wanaohusika. Ni taarifa tu, Ushahidi baadae.

Update:naomba niweke taarifa sawa, makampuni yanayohusika na sakata hili yapo matatu kwasasa ni hilo moja ndiyo ushahidi upo hayo mengine tutayaleta uchunguzi ukikamilika.
 
Dah kama kweli bora iwe hvyo,liwalo na liwe,maana mgombea binafsi afadhali itakuwa,
 
Red One, hii ni mpya inawezekana, maana ZZK kashajiapisha LAZMA agombee urais so connection na ADC? ukipata hizo data hebu tuweke...
 
Ukweli utadhihirika tu hata kama siyo leo. Vyama vya upinzani vina mapindikizi yanayohakikisha kwamba vyama hivyo havifanikiwi kufikia malengo yao.
 
Mungu amesikia kilio cha muda mrefu cha kumtaka mungu atuondolee watu wafanyao mambo katika giza.Mungu atatuweka huru na kweli itatuweka huru.ole wenu wanafiki cha moto mtakiona
 
kama ni mgombea binafsi hili wala sina mashaka nalo ila la kuleta chuki kwenye vyama vya upinzani hapo sijafurahishwa na mbinu hiyo, ni bora watumie mikakati miingine kuliko njama za kizamani na kwanza mgombea binafsi ni ngumu kuchukua nchi kwa mazingira ya kwetu, waafrica wengi wanapenda chama.

Elimu bado haijawaingia na ndio maana sasa hivi watu wanaependa chadema tafikiri woote waliomo ni malaika ila kumbe ni binadam kama wao, vile vile mtu akisikia ccm tu mtu anasikia kinyaa tafikiri woote wameoza, so wengi wanaangalia vyama ingawa kama katiba ya mgombea binafsi ikipita itakuwa ina nguvu sana kwenye kugombea udiwani, na ubunge ila uraisi ni kujipanga kwanza. Wasitumie maji taka kwa kuwachafua wengine, wawe na njia mbadala.
 
Usiseme upinzani maana hata ADC ni upinzani, sema CHADEMA ndo wanataka idhoofike na isifike 2015! Lakini hawawezi maana mtandao wa chadema upo hadi ikulu!
 
Kwa hili Nakaribia kukubaliana nalo. Namkumbuka Spika mmoja wa bunge wa zamani aliwahi kusema kuwa watu wana wivu wa kike, pale alipohusishwa na kampuni moja ya simu. kwa sasa hivi nadhani ni mtu mkubwa sana kwenye chama kikubwa sana hapa nchini.
 
Doubt any, get many

lets go........................................................
 
hii kitu ni kweli na mimi kitengo changu cha intelejensia kiko nusu ya kazi na vyama vinavyochunguzwa ni ADC NA CHAUMMA.pamoja na kauli ya waziri mwandamizi wa ccm kuwa chadema haina muda mrefu.
 
kama ni kweli basi mbinu hii itakua ni kudhoofisha upinzani, wakifika kwenye uchaguzi itakua ni kugawana kura tuu na mwisho ni kushindwa na mafisadi wataendele kula nchi, kweli usilolijua litakusumbua!!! tunasubiri ushahidi.
 
kama ni kweli basi mbinu hii itakua ni kudhoofisha upinzani, wakifika kwenye uchaguzi itakua ni kugawana kura tuu na mwisho ni kushindwa na mafisadi wataendele kula nchi, kweli usilolijua litakusumbua!!! tunasubiri ushahidi.


umenena vema hilo ndilo lengo na anaye tumiwa anajulikana hakuna ubishi.
 
Mkuu mtoa mada endelea kutupa hizo updates ili na sisi tuendelee kujipanga kuyakabili haya manyang'au
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom