Malipesa
JF-Expert Member
- Aug 23, 2011
- 310
- 32
Wasomi mbalimbali wamesema sakata la mgogoro wa Madaktari na serikali linachochewa wanasiasa kutokana na misimamo ya wanasiasa hao walioitoa kwa nyakati tofauti huku wasomi hao wakinena kama ifuatavyo:
1. Uhai haupimwi na kitu chochote, Utaratibu wa Madaktari kugoma umepigwa marufuku katika nchi nyingi duniani-Dk.BENSON BANA
2. Ni tabia mbaya kuona kada moja inajiona ni bora kuliko nyingine-Dk. Bana
3. ANANILEA NKYA kusema kitendo cha Mawaziri wa Afya kushindwa kujiuzulu ni maajabu ni dhahiri suala hili limejaa siasa-SALIM SAID
4. Haki bila nidhamu, wajibu ni sawa na wazimu-Salim Said
5. Kuna njama za kuidhoofisha Serikali kupitia taaluma ya Udaktari-JOSEPH LUGHA
6. Kumpa Rais siku kwa ajili ya kutaka kufanikisha mambo yao ni kinyume na utamaduni wa Watanzania-BANA
Tutafakari
50% ya ulichosema kimesemwa na wasomi kimesemwa na Dr. Bana. Kwa maana nyingine unataka kuaminisha watz kuwa bana anawakilisha 50% ya wasomi hapa tz.
Unatakiwa kufahamu kwamba,
Dr. Bana ni muumini mzuri sana wa siasa na ni wa upande wa CCM. Ni mshabiki mzuri sana wa siasa za upande mmoja na kwa taarifa tu ni kwamba anajipendekeza kwa CCM kwa ajili ya kujiandaa kutwaa madaraka UDSM