Sakata la Mahujaji: Utendaji ATCL na Yaliyojiri Hadi Leo Hii

Shirika la Ndege nchini, ATC limelaumiwa kwa kufanya kitendo cha aibu ya mwaka kwa kuwasotesha kwa wiki nzima mahujaji zaidi ya 300 ambao wameshakamilisha taratibu zote za safari

Hii ni ishu ya kisheria, sio siasa kwa hiyo wahusika ni kwenda mahakamani na kudai fidia, mashirika ya ndege ya nje hutulipa dola 300 kwa kila siku utakayosubiri, kwa hiyo ATC wawajibike tu, wala hakuna sababu ya mjadala!
 
Hivi lile dege alilonunua Chez Nkapa (hadi tukaambiwa ikibidi kula nyasi tutakula, shurti dege linunuliwe) haliwezi kuwawahisha hao mahujaji huko Mecca na kuwaondolea hii adha? Maana kodi yao pia ilitumika kununua dege hilo. Mlio karibu na JK hebu mshaurini alitoe hilo dege lifanye angao jambo moja la kheri, pengine italiondolea nuksi inayotokana na malalamiko yaliyogubika ununuzi wake. Mawazo yangu tu.

"If I had served my God as diligently as I did my king, He would not have given me over in my grey hairs." Thomas Cardinal Wolsey (1473-1530), Archbishop of York, Lord Chancellor and Chief Aide to King Henry VIII.

KITHUKU,
YAANI SAHIHI YAKO NIMEIPENDA TU SANA! SASA HIZO MVI SII AMEKUWA MZEE? JE WAPEWE VIJANA BADALA YA WAZEE? HA HA HA HA?
 
Tumeshasubiri sana facts, vielelezo, maelezo, ushahidi, mashahidi, uchunguzi, vichunguzwa, katika mambo mengi pale Tanzania mpaka tumechoka lakini hakuna lolote linalofanyika.

Geeque,
Mmesubiri lini hizo facts wakati issue yenyewe umeelezwa leo?? Facts gani hizo? Ndio generalizations zenyewe hizi zisizo na mpango!

Hii ndio historia ya Tanzania na hii historia ndio inafanya kila mtu aje juu hapa kutokana na uzembe huu wa ATC.

Kama msomi, it is wrong and so unprofessional to make judgement based on past experiences, eti na historia imeonyesha. Yaani hata side ya ATC hamjasikia already mko na kwenye fastlane na "historia inaonyesha" ??? Halafu unauliza tutaondokanaje na umaskini, wakati matajiri wenyewe wa Elimu mna-act otherwise?!

Hivi hao ATC katika hizo siku saba walijaribu hata kuita Press Conference au kuwaambia hao mahujaji in private sababu kubwa za ucheleweshaji wa ndege na kwa nini hawakujiandaa kuwa na Plan B endapo tatizo lolote lingetokea.

Now these are the questions you need to ask...

Kwa utaratibu unaojulikana ni kuwa hawa mahujaji huwa wanalipia hizi safari in advance. Kutokana na uzembe uliokithiri katika Idara mbalimbali za Umma na Serikali kuu, Uzembe na Ugoigoi huu unaendelea kwa miaka mingi bila ya kupatiwa ufumbuzi wowote, Nadhani tuna haki kabisa ya kutumia msemo wa "Guilty Untill Proven Innocent" hasa kutokana na initial elements kuonyesha uzembe ni wa ATC.

I will be the first to shutumu ATC if proven negligence on their side, until then...

You have a great day now!
 
Geeque,
Mmesubiri lini hizo facts wakati issue yenyewe umeelezwa leo?? Facts gani hizo? Ndio generalizations zenyewe hizi zisizo na mpango!

Kama msomi, it is wrong and so unprofessional to make judgement based on past experiences, eti na historia imeonyesha. Yaani hata side ya ATC hamjasikia already mko na kwenye fastlane na "historia inaonyesha" ??? Halafu unauliza tutaondokanaje na umaskini, wakati matajiri wenyewe wa Elimu mna-act otherwise?!

Now these are the questions you need to ask...

I will be the first to shutumu ATC if proven negligence on their side, until then...

You have a great day now!

Kisura,
Kaazi kweli kweli!
 
I think you need to familiarize yourself with what really happens behind closed doors! Talk to the victims!! Tuachane na hivi vitu kuwafanya wazungu(nchi zilizoendelea) kuwa kila leo wanafanya vitu perfect, sometimes, things happen beyond their capabilities too, better yet, in short notice! "Cancellation to be precise" !!!

Nimesafiri sana na ATC as well as KQ,kwa kifupi shirika letu la ndege ni hawathamini wateja nimeexperience hivyo vitu na ATC mfano mmoja mwaka 1992 tumekalishwa kiti kimoja watu wa wiwili kisa yule kijana mwingine baba yake alikuwa pilot ATC, hizi za unakwenda Airport unaambiwa ndege imechelewa kufika kutoka sijui Entebbe au sijui Jo'burg njoo kesho alfajiri zilikuwa nyingi sana, nina uhakika hawa mahujaji waliambiwa vivyo hivyo kuwa njooni kesho muda fulani blah blah wakaona bora wasubirie hapo airport ikageuka wiki.
 
jana walikuwa wanaongelea kuwa serikali inatoa dola milioni 2 kuwakodia mahujaji ndege....nadhani ndege iliyokodiwa na serikali itakuwa imefika usiku uliopita....
 
mama lao sasa huo uchokozi dada. Uliza watu wa dar mmewasaidiaje wenzenu?
au we ulitaka wafanyeje?
 
mama lao sasa huo uchokozi dada. Uliza watu wa dar mmewasaidiaje wenzenu?
au we ulitaka wafanyeje?

huyo ana lake analolitafuta la kufungia mwaka au la kulia xmas

ila nnaona vijana wamekusudia kuumaliza mwaka kwa amani
 
Safari ya Mahujaji yaiva

2007-12-12 09:24:47
Na Eshy Mushi

Hatimaye, kundi la kwanza la Mahujaji zaidi ya 1,000 waliokuwa wamekwama kwa siku nane kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, jana lilifanikiwa kuondoka kwenda kuhiji Mecca, Saudi Arabia.

Kuondoka kwa Mahujaji hao kumetokana na serikali kulazimika kuingilia kati kutafuta ndege maalum ya kukodi baada ya Shirika la Ndege Nchini (ATC) kushindwa kuwasafirisha kwa wakati muafaka.

Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, jana jioni alifika uwanjani hapo na kuzungumza na Mahujaji hao kuhusu mpango wa serikali wa kuwatafutia ndege hiyo na pia kuwaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Ndege hiyo Al Zahar mali ya Shirika la Ndege la Saudi Arabia, iliwasili uwanjani hapo saa 1:50 usiku na kuchukua kundi la kwanza la Mahujaji 379 kwenda Mecca.

Akizungumzia suala hilo, Waziri Mkuu alisema alipata taarifa za kukwama kwa Mahujaji akiwa Dodoma kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 46 ya Uhuru.

``Rais alishtushwa mno na taarifa hizo na alihangaika usiku kucha akipiga simu kwa nchi mbalimbali za Falme za Kiarabu ili kupata ufumbuzi wa tatizo hilo,`` alisema Bw. Lowassa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Abbas Kandoro aliwaambia Mahujaji hao kwamba, ndege hiyo itapeleka kundi hilo la kwanza hadi Mecca na kuwarudia wengine na kwamba itafanya hivyo kwa kusaidiana na ndege mbili zote zilizotafutwa na serikali.

Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, pia alifika kuwaaga Mahujaji hao na kuwatakia safari njema.

Kadhalika, Waziri wa Miundombinu Bw. Andrew Chenge alikuwepo uwanjani hapo kuwaaga Mahujaji hao.

Mahujaji hao walipanga kusafiri Desemba 3, mwaka huu lakini walikwama na kuendelea kusota kwenye viwanja vya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa muda wote huo.

Kutokana na vikwazo hivyo, baadhi ya wanaharakati wa haki za Waislamu nchini ambao waliwatembelea Mahujaji hao jana, walitishia kuwa wataandaa maandamano kulaani kitendo hicho.

Mahujaji hao 1,150 ni wa kutoka Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Comoro na nchi mbambali zilizopo jirani na Tanzania.

Wakati wanaharakati hao wakitoa kauli hiyo, uwanja huo ulitawaliwa na vilio na simanzi kutoka kwa mahujaji hao hasa wanawake.

Sheikh Issa Ponda Issa, alisema kwamba Mahujaji hao walikuwa wasafiri Desemba 3, lakini kumekuwa na taarifa tofauti juu ya safari hiyo.

`Hili si jambo la bahati mbaya, bali la makusudi na limeratibiwa. Serikali isipopangua safu ya uongozi kwa kuwaondoa waliohusika kukwamisha safari hii, hatutawaelewa, alisema.

Kwa mujibu wa mahujaji hao, siku ya mwisho kupokelewa Mecca ni kesho na kwamba kama wasingesafiri jana usiku, uwezekano wa kwenda kutekeleza sala hiyo ambayo ni moja ya nguzo tano za Kiislamu, wasingeitimiza.

* SOURCE: Nipashe
 
Kwa mujibu wa taarifa nilizotumiwa hivi punde, hata baada ya kundi la kwanza la mahujaji kuingia ndani ya ndege tayari kwa safari kapteni alishindwa kurusha ndege kwa vile mahujaji waligoma kutua Madina. Kwa mujibu wa chanzo changu, ndege hiyo isingweza kutua Jeddah kwa vile haikuwa na "slot". Mahujaji walielezwa wangetua Madina na kusafiri kwa mabasi kwa mwendo wa saa sita kwenda Mecca. Kiutaratibu muda wa kutolewa vibali vya ndege kutua Jeddah huishia Ramadhan 15. Baada ya hapo hakuna njia nyingine iliyo rahisi ya kupata vibali hivyo. Inasemwa pia kuwa katika wakati huu ndege hutua Jeddah kila baada ya dakika 5 wakati nyingine zikizunguka angani kusubiri muda wake. Waziri wa Hajj na mwenzake wa Mambo ya Ndani ndiyo ambao Wizara zao zina jukumu la kuratibu shughuli za Hijja. Inasemwa pia, kuwa Sultan wa Saudi Arabia hana mamlaka ya kuingilia kazi za watendaji wake hao.
Njia pekee kwa sasa kwa Mahujaji waliopo pale Uwanja wa Ndege Dar kuweza kusafiri na kuwahi Hijja ni kukubali kutua Medina na bado kuna hati hati ya makundi yote kuweza kusafiri. Vinginenyo Hijja ya mwaka huu huenda ikawa ndoto kwa mahujaji hao. Wakati tukiendelea kufuatilia sakata hili, tunawapa pole mahujaji hao na kuwatakia mioyo ya ustahamilivu. Kwa habari zaidi katika picha, tembelea: http://mjengwa.blogspot.com
 
Asante Maggid.... Duh, poleni wenzetu Mola atawasikia..... Hivi jamani huu usanii wa Bongo mpaka kwenye mambo ya "Dini" na "Imani".......
Wallahi twafwa siye WaTZ!
 
Duh, hiyo kali. Naona wangeilimishwa waelewe hali halisi, maana hapo sasa wanashindana na ukuta. Kama hizo ndio taratibu zenyewe za kutua, hawawezi kulazimisha especially kwamba hiyo sio Tanzania ambapo taratibu hupindishwa kirahisi.
 
mtu wa pwani........

Kwa mujibu wa taarifa nilizotumiwa hivi punde, hata baada ya kundi la kwanza la mahujaji kuingia ndani ya ndege tayari kwa safari kapteni alishindwa kurusha ndege kwa vile mahujaji waligoma kutua Madina. Kwa mujibu wa chanzo changu, ndege hiyo isingweza kutua Jeddah kwa vile haikuwa na "slot". Mahujaji walielezwa wangetua Madina na kusafiri kwa mabasi kwa mwendo wa saa sita kwenda Mecca. Kiutaratibu muda wa kutolewa vibali vya ndege kutua Jeddah huishia Ramadhan 15. Baada ya hapo hakuna njia nyingine iliyo rahisi ya kupata vibali hivyo. Inasemwa pia kuwa katika wakati huu ndege hutua Jeddah kila baada ya dakika 5 wakati nyingine zikizunguka angani kusubiri muda wake. Waziri wa Hajj na mwenzake wa Mambo ya Ndani ndiyo ambao Wizara zao zina jukumu la kuratibu shughuli za Hijja. Inasemwa pia, kuwa Sultan wa Saudi Arabia hana mamlaka ya kuingilia kazi za watendaji wake hao.
Njia pekee kwa sasa kwa Mahujaji waliopo pale Uwanja wa Ndege Dar kuweza kusafiri na kuwahi Hijja ni kukubali kutua Medina na bado kuna hati hati ya makundi yote kuweza kusafiri. Vinginenyo Hijja ya mwaka huu huenda ikawa ndoto kwa mahujaji hao. Wakati tukiendelea kufuatilia sakata hili, tunawapa pole mahujaji hao na kuwatakia mioyo ya ustahamilivu. Kwa habari zaidi katika picha, tembelea: http://mjengwa.blogspot.com
 
Tunapozungumza ufisadi wao wanadhani tunazungumzia rushwa peke yake. Ufisadi ni pamoja na ubabaishaji, uzembe, kutokuwajibika n.k Sasa hadi hii leo hata Mataka ameenda kukutana na Mahujaji na kuwataka radhi?
 
mtu wa pwani........

Kwa mujibu wa taarifa nilizotumiwa hivi punde, hata baada ya kundi la kwanza la mahujaji kuingia ndani ya ndege tayari kwa safari kapteni alishindwa kurusha ndege kwa vile mahujaji waligoma kutua Madina. Kwa mujibu wa chanzo changu, ndege hiyo isingweza kutua Jeddah kwa vile haikuwa na "slot". Mahujaji walielezwa wangetua Madina na kusafiri kwa mabasi kwa mwendo wa saa sita kwenda Mecca. Kiutaratibu muda wa kutolewa vibali vya ndege kutua Jeddah huishia Ramadhan 15. Baada ya hapo hakuna njia nyingine iliyo rahisi ya kupata vibali hivyo. Inasemwa pia kuwa katika wakati huu ndege hutua Jeddah kila baada ya dakika 5 wakati nyingine zikizunguka angani kusubiri muda wake. Waziri wa Hajj na mwenzake wa Mambo ya Ndani ndiyo ambao Wizara zao zina jukumu la kuratibu shughuli za Hijja. Inasemwa pia, kuwa Sultan wa Saudi Arabia hana mamlaka ya kuingilia kazi za watendaji wake hao.
Njia pekee kwa sasa kwa Mahujaji waliopo pale Uwanja wa Ndege Dar kuweza kusafiri na kuwahi Hijja ni kukubali kutua Medina na bado kuna hati hati ya makundi yote kuweza kusafiri. Vinginenyo Hijja ya mwaka huu huenda ikawa ndoto kwa mahujaji hao. Wakati tukiendelea kufuatilia sakata hili, tunawapa pole mahujaji hao na kuwatakia mioyo ya ustahamilivu. Kwa habari zaidi katika picha, tembelea: http://mjengwa.blogspot.com

Hao vingozi wa msafara ndio wanataka kuharibu tu kwani jeddaha na madina kuna tofauti gani na muda wanao pia na wanarahisisha pia maana kwa vyovyote hata wakianza huko maccah lazima watafika madina ni miongoni mwa ibada pia..na usafiri kutoka madinah kwenda maccah mzuri japo ni masaa hayo sita
 
hiyo ndio bongo,kama raisi halitudanganya kuhusu umeme wa richmod itakuwa mataka na ndege ya kukodi,watanzania tu wavivu wa kufikiri yaani tumeshindwa kujua mbivu na mbichi zi wapi.hapo hakuna wa kuwajibishwa wala kuwajibika kwani ni kazi ya mungu.
 
Back
Top Bottom