Sakata la kuuzwa UDA: Kauli za Idd Simba, Masaburi, Kisena et al utata mtupu

Acheni kulalamika ndugu watanzania, elfu mbili na kumi na tano iko mlangoni jiandae kufanya kweli haya yote yatakoma.
 
Ndugu yangu, Ni heri Jakaya Kikwete ambaye hajachukua na kuwa na Damu ya Mwanadamu mwilini Mwake, ila ni kuipa rasilimali ambazo atakufa na kuziacha na ametuacha sisi salama na umasikini wetu; Kuliko Huyo Rais Paul Kagame ambaye ana Damu za watu wengi ambao wani waaminifu na hawana hatia, kwasababu ya ulafi wa madaraka akaamua kuingia porini na kuua maadui zake; Heri Jakaya Kikwete simpendi lakini ameniacha huru nakufa na umasikini wangu

Hapana mkuu kufa ni kufa tu mwishowe ni kuzikwa basi!
 
Hii nchi hawa walioko huko juu hawana hata chembe ya utu wala aibu, ni huyu huyu Simba na wenzake walituingiza mkenge wakafungua kampuni na kuipa jina la kijanjajanja-NICO (National Investment Company) wengi tulivyoona tukajua mkombozi ndio kaja, tukatumbukiza vihela vyetu mumo; kumbe maskini ya mungu tunaendelea kutajirisha matapeli! Iko siku watalipa tu hizi dhuluma wanazotutendea!kwani tuaambiwa dua la mdhulumiwa halidondoki chini!
 
Waaaait a minute - over Tshs 200 million consultancy fee? kwa kazi gani? au ni fee ya miaka 120? Ana-charge kiasi gani kwa saa huyu consultancy Simba? Yote tisa kumi ni pale aliposema alitaka UDA iende kwa mzawa! Hivi huyu Simba hajaelewa bado - kwamba watanzania tunapigania uhuru toka kwa mkoloni mweusi?

Mimi nadhani kukata mzizi wa fitna Simba ajibu maswali 'under oath' na huyu Simon Group Guy pamoja na Prof Juma Kapuya wajibu under oath. Baada ya hapo ndio uchunguzi uendelee halafu tuone nani atakwepa Keko!
 
Ndugu yangu, Ni heri Jakaya Kikwete ambaye hajachukua na kuwa na Damu ya Mwanadamu mwilini Mwake, ila ni kuipa rasilimali ambazo atakufa na kuziacha na ametuacha sisi salama na umasikini wetu; Kuliko Huyo Rais Paul Kagame ambaye ana Damu za watu wengi ambao wani waaminifu na hawana hatia, kwasababu ya ulafi wa madaraka akaamua kuingia porini na kuua maadui zake; Heri Jakaya Kikwete simpendi lakini ameniacha huru nakufa na umasikini wangu

Hata Rwanda kabla ya Kagame ilikuwa kama Tz ya sasa,una uhakika gani utakufa na umaskini wako ukiwa salama?panua fikra ndugu!
 
nchi ya ki3e#ge sana hii.. hao jamaa meya na huyo simon bado wako na wanabishana tu na vyombo vya habari
 
Yani Tanzania kila kitu dili wanao husika wote wapigwe nyundo
 
Ndugu yangu, Ni heri Jakaya Kikwete ambaye hajachukua na kuwa na Damu ya Mwanadamu mwilini Mwake, ila ni kuipa rasilimali ambazo atakufa na kuziacha na ametuacha sisi salama na umasikini wetu; Kuliko Huyo Rais Paul Kagame ambaye ana Damu za watu wengi ambao wani waaminifu na hawana hatia, kwasababu ya ulafi wa madaraka akaamua kuingia porini na kuua maadui zake; Heri Jakaya Kikwete simpendi lakini ameniacha huru nakufa na umasikini wangu

Kagame anafanya kazi bwana na nchi yake Inaendelea na Ndiyo maana tunamfagilia,hayo mambo mengine unayo mtuhumu yanatoafauti gani wezi wa mali ya umma,madini wakati watu wengine wanakufa kwa njaa na huduma duni za hospt na mambo mengi na wanakufa kila siku?

kagame safiiiiiiiiiiiiiiiii!
 
Bongo kweli tambarare yaani huyo Idd Simba ni mwenyekiti wa bodi ya UDA anatoa consultancy ya ununuzi wa UDA kwa Simon group, na huyo Simon group nusura awe mbunge wa CCM.

Yep, Idd Simba, mwenyekiti wa bodi ya UDA, anatoa ushauri kwa Simon Group juu ya ununuzi wa UDA. Kapuya, mwenye shares Simon Group, kateuliwa na meya wa jiji kuchunguza ufisadi UDA. Tanzania kila kitu kinawezekana.
 
ningelikua mimi ndio serikali, hao wote wangekua ndani ili waongee kinachoeleweka. Imekua ni kitu cha kawaida mtu kukutwa na tuhuma za ufisadi na kuanza kusafishwa au kujisafisha. Huwezi kuniambia mpaka leo hii bado kuna mambo ya uchunguzi wakati watuhumiwa wako huru. watarekebisha documents zote na mwisho wa siku tunazidi kuwa masikini.

Nachukia serikali inayolala usingizi wakati raia tunaumia....ifike mahali iwe historia ndugu zangu ili tuweze kuanza upya na kujenga Taifa letu! Viongozi wengi ni mdomo tu bila vitendo. Shame on you all na mkumbuke siku moja you will be punnished hata kama sio Duniani endeleeni na utawala wa kujisahau
 
tunachinjana wenyewe kwa wenyewe. huu ni sawa na uuaji kwani kwa kufanya hivyo maslahi na maisha ya watanzania wengi yako hatarini.
eee mwenyezi mungu wape moyo wa uoga wote wenye moyo wa namna hii!
kweli inaudhi, lakini TIME WILL TELL!
 
Maana yake ni kwamba Idd Simba tayari kashinda kesi, akishikilia huo msimamo, serikali haina la kumfanya!
 
Thread kama hii huwezi kuona members kama Omarilyas, Kasheshe, Seleman, Gamba la Nyoka, X-paster wala Zomba wakicomment!! Wakijitutumua sana ni FF, The Boss, Kibunango, FMES na Njiwa pekee ndo wanaweza kuja kubadili hali ya hewa kwenye sredi...
 
Na ndio maana we sio serikali. Lakini kumbuka kwamba anayeiweka serikali madarakani ni wewe kwa hiyo una mchango mkubwa sana kuleta mabadiliko. Kusema unaichukia serikali na sawa na kusema unachukia maamuzi yako na kujichukia mwenyewe.
Dawa ni moja tuu........
 
Ndiyo huyu Idd Simba alikuja na sera ya 'uzawa' eti biashara ndogo ndogo zifanywe na watanzania akitaka kutuaminisha kuwa ni mzalendo. Mwalimu Nyerere akamwita huyu ni kaburu tu. Kumbe alishaona mbali. Kazi kweli kweli!
 
Kuuza kampuni ya UDA ni kwa manufaa ya wajanja wachache kwa kile kilichofanya kuandaliwa mkakati wa ubinafshaji ulioshamiri enzi za awamu ya tatu ya utawala wa nchi ya Tanzania. Hakuna sababu yoyote inayoingia akilini kwani swali iweje mtu binafsi anaweza kuwa na magari ya abiria na kuendesha kwa mafanikio makubwa, lakini serikali ishindwe kuweka mkakati wa kuinua uchumi.

Mpango huo ni wa wengi kama ilivyo katika Shirika la ndege, ambapo shirika la wazalendo serikali imeshindwa kulisimamia lakini shirika lililoundwa na wafanyabiashara wachache la Prescion lifanye vizuri? Jibu liko kwa mikono ya serikali. Siri hiyo inajulikana japo watu wanalifumbia macho. Lakini viongozi wetu wafahamu wameapa uongo kuwa watatetea haki na maslahi ya wa-Tanzania. Ni hujuma tupu inayofanywa. Tabia ya kuleana haifai.

Nchi imeporwa na inaendelea kuporwa ni kauli ya mwanasiasa machachari aliyewahi kuwa Waziri wa mashauri ya ndani na baadaye kuongezewa madaraka na kushika unaibu Uawaziri Mkuu katika Tanzania. Huyu ni yule aliyetoka serikali hiyo na kujiunga na kambi ya upinzania, Bwaba Augustino Lyatonga Mrema.

Kipindi sakata la Richmond likipamba kasi, Mbunge wa Moshi Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Bwana Ndesamburo alitoa mfano wa kukomesha ufisadi ni kuiga mifano ya baadhi ya nchi za Mashariki ambapo watuhumiwa hupigwa risasi haradhani. Wakati mbunge huyo akitolea mfano wa kupigwa risasi, kamera ya televisheni ilimlenda sawia mmoja wa watuhumiwa aliyeonesha kustuka na kuogopa, na kuonesha hali hiyo isije ikaidhinishwa na Watunga sheria hao.

Hatua ichukuliwe kuwafilisi wahusika na tuhuma za ufisadi, bila hivyo nchi hii itaishia ombaomba tu kwa nchi za magharibi.
 
Back
Top Bottom