Sakata la kuuzwa UDA: Kauli za Idd Simba, Masaburi, Kisena et al utata mtupu

kaburunye

JF-Expert Member
May 12, 2010
672
74
Gazeti la majira la leo linaripoti kuwa Idd Simba anadai ile pesa aliyoingiziwa kwenye akaunt yake na mnunuzi (Simon) haihusiani na mauzo ya UDA bali ni consultancy fees (yaani malipo ya ushauri wa kitalaam) alioutoa kwa SImon Group. SImon yeye anadai hajawahi kupata ushauri wa kitaalam kutoka Idd SImba bali pesa hiyo ni malipo ya ununuzi wa UDA. Yaani ni full utata....

Habari yenyewe hii hapa

Kashfa UDA - Idd Simba azungumzia kilichotokea

Iddi Simba ajibu tuhuma dhidi yake

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo, Bw. Idd Simba amejibu tuhuma zilizoelekezwa kwake, akisema mchakato wote ulikwenda kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi, akisema serikali ilijulishwa kila hatua.

Huku akitoa madai ya kughushiwa kwa saini ya Meneja wa UDA, Bw. Victor Milanzi kuonesha kuwa mnunuzi alielekezwa kuweka fedha katika akaunti binafsi, Bw. Simba alisema kuwa kutokana na mchakato wa uuzwaji wa UDA kufuata sheria na taratibu za nchi kadri zinavyojulikana, si sawa kusema kampuni hiyo imemilikisha hisa zake isivyo halali wala kuwa imetapeliwa fedha zake.

Akizungumza na Majira juu ya sakata hilo, hasa tuhuma kuwa alipokea sehemu ya malipo ya ununuzi na fedha hizo kwenye akaunti yake binafsi, Bw. Simba alisema kuwa fedha hizo hazihusiani na ununuzi na uuzwaji wa UDA, bali masuala mengine kati yake na Simon Group Ltd.

Bw. Simba ambaye amewahi kuwa kiongozi mwandamizi serikalini, alisema kuwa taarifa za mchakato wote wa uuzwaji wa UDA alikuwa akiziwasilisha serikalini, kwa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi na kwa Kampuni Hodhi ya Mashirika ya Umma (CHC).

Alisema kwa mujibu wa kanuni za UDA, madaraka ya uuzaji wa hisa ambazo hazijagawiwa yako mikononi mwa bodi ya wakurugenzi, ndiyo maana bodi iliendelea na mchakato wa kumuuzia Simon Group kwa mujibu wa sheria na mkataba wa mauzo ukafanyika, huku hisa hizo zikilipiwa, hivyo si kweli kwamba ziliuzwa kiholela.

"Mchakato wote ulikwenda kwa mujibu wa sheria na kanuni. Tulikuwa tunapata ushauri wa wanasheria katika mchakato mzima. Hao wanaodhani na kusema kwamba Simon Group imetapeliwa na kwamba haikumilikishwa hisa za UDA kihalali si sawa, kwani uuzwaji ulifanyika kwa mujibu wa kanuni na sheria tunavyozielewa.

"Kibaya kilichotokea ni kwamba baada ya Simon Group kuhalalishiwa ununuzi wa hisa hizo na kulipia malipo ya kwanza ya milioni 285, mwenyekiti (wa Simon Group), Bw. Robert Kisena akataka kuingia katika utendaji wa kampuni na uongozi wake, hata kabla ya AGM (mkutano wa wanahisa wa mwaka).

"Alipokatazwa kufanya hivyo na kushauriwa kwamba asubiri mpaka taratibu zikamilike, akaingia kwa nguvu kwenye majengo ya kampuni (UDA), kinyume kabisa cha taratibu. Hapo ndipo vurugu zilipotokea. Alipohojiwa hajakamilisha malipo ya pili kama ilivyotakiwa alidai kuna pesa alishalipa katika akaunti yangu mimi Idd Simba, kwa mujibu barua aliyoandikiwa na uongozi wa UDA," alisema Bw. Simba na kuongeza;

"Moja, barua ni ya kughushi, kwa sababu Meneja wa UDA, Milanzi hakuandika barua wala hakukuwa na maagizo yoyote ya yeye kulipia hisa zake kupitia akaunti binafsi. Hilo jambo lisingewezekana.

"Lakini ieleweke kwamba muda mrefu kabla ya tukio hilo na katika shughuli ambazo hazihusiani hata kidogo na UDA, zilizotokana na ushauri wa jumla wa kibiashara aliotaka kutoka kwangu, alikuwa anastahili kulipa fedha zangu binafsi. Nilitoa amri ya kulipia katika akaunti yangu, alifanya hivyo kwa awamu tofauti kadri nilivyotoa maagizo."

Akizungumza mbele ya mwanasheria wake, Bw. Simba alipoulizwa iwapo watu hawawezi kuhoji mgongano wa maslahi ulio wazi katika suala hilo, la Simon Group kununua hisa katika shirika (UDA) ambalo yeye ni mwenyekiti wa bodi, huku pia wakati huo huo yeye akitoa ushauri wa kibiashara kwa kampuni iliyotaka kununua UDA, alisema;

"Ndiyo wanaweza kuhoji...lakini sasa mimi si mtumishi wa umma, pale UDA mimi si mwajiriwa. Mimi nauza maneno, natoa ushauri. Ukija kutaka ushauri siwezi kukutalia. Lakini kwenye bodi tulikuwa serious sana. Tatizo ni kwamba mwanzoni sikutilia maanani sana tabia ya Robert Kisena, kwa sababu mimi nilikuwa na hamu sana mzawa achukue UDA, siyo kila kitu nchi hii anachukua mwekezaji mgeni," alisema Bw. Simba.

Alisema kwamba inasikitisha kuona mpaka sasa serikali haijachukua hatua yoyote kuinusuru UDA, akionesha matumaini yake kwa CHC itachukua hatua za haraka kurejesha hali ya kawaida katika shirika hilo muhimu la usafiri Dar es Salaam, pia kwa kamati iliyoundwa kuchunguza suala hilo.

Wakati Bw. Simba akisema kuwa fedha zilizowekwa katika akaunti yake binafsi hazina uhusiano wowote na uuzwaji wa UDA, Bw. Kisena amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema kuwa hawakuwahi kuwa na shughuli nyingine tofauti na hiyo ya ununuzi wa shirika hilo la umma.

Akinukuliwa katika moja ya magazeti ya kila siku jana, Bw. Kisena alisema kuwa walilipa fedha hizo katika akaunti ya Bw. Simba, kama sehemu ya malipo ya ununuzi wa UDA, kutokana na maelekezo ya uongozi wa UDA, akisema kuwa anazo nyaraka zinazoonesha hivyo.
 
Iddi Simba jaman tumekukosea nini wana wa nchi hii mpaka ututendee hivyo?

.....Wakati mwingine watu wanajuta kuwa Watanzania, sababu ndo Kama hizi!
 
na hii serikali yetu kwa kuchunguza tu wanawweza ila kutekeleza majibu ya uchunguzi ni zero.
 
Idd Simba ni tapeli, Magamba Robert Kisena kaingizwa chaka. Ndio maana anahaha kusingizia kuwa eti ni sehemu ya malipo ya UDA bali ni dili ambalo walielewana kuwa nipigie pande ninunue share za UDA nitakupa mshiko. Simba alifanya hivyo na kufanikiwa. Robert alipogundua deal ni batili ndo akaanza kuhaha. Hii ni Bongo
 
Hii ndio janja toto ya hawa wazee wa nchi,nae mkuu wa inji kabakia kibya kabisa ati uchunguzi ufanyike? Natamani Rais Paul Kagame wabadilishane na Jk kwa muda wa miezi kadhaa then afanye yale anayoyafanya Rwanda muone hawa jamaa wezi watakavyoshikishwa adabu
 
Kila siku ipitayo tunathibitisha kwamba viongozi tulionao hawana maadili binafsi na ya uongozi wanaopewa. Suala la Iddi Simba ni mfano wa ukosefu wa maadili walionao viongozi wetu. Moja ya sababu kubwa inayotufikisha hapa tulipo ni kwamba viongozi wa nchi hii hawapati nafasi hizo kwa njia asilia za kupata uongozi (natural ascendance to leadership) bali ni kwa kutumia undugu,urafiki,upenzi, Hongo za aina zote, urafiki wa kibiashara n.k. Hivi kweli kwa mtu wa uzoefu na uwezo kipesa kama Iddi Simba kuwa kati ya "waliofisadi" shirika ambalo tayari lilishajifia ineleweka? Ameshafisadi mangapi mpaka hapa tulipo? Hapa hatutapona mpaka watu wafunzwe adabu ya kuheshimu mali ya umma na njia iliyomwafaka ni kuiga China na uwazi walionao katika kutoa adhabu kwa makosa kama Rushwa, Uzembe na Biashara ya dawa za kulevya. Nchi inayomba kama meli iliyopigwa na dhuruba...Hapa tulipo tuko kwenye hali ya hatari...Naacha kuandika kwa hasira maana umeme hamna na mafuta nayo imekua bidhaa adimu ya kuipata kwa kidumu na kwa foleni.Grrrrrrrrrrrrrrmfffffffffffffffffffff 
 
Serikali inasubiri nini kuwakamata wote na kuwanyonga?ushaidi upo wazi so wanachunguza nini?

mjumbe punguza jazba kwani nini utawala wa sheria hauendi hivyo lazima wapatiwe nafasi ya kuhojiwa na kufikishwa mahakamani ndio wahukumiwe
 
Hii ni mitapeli inayo lelewa na si mwingine yule, bali Mh. Rais wetu Kikwete!! Mambo ya kuzungukazunguka mibuyu kwa chunguzi zisizo na tija ni kupoteza muda, uovu uko wazi, hawa ni majangiri ya mali za wananchi!!
 
Idd Simba (CCM) na Bob Makani (Chadema) Uhusiano wao Watoto wao Wameoana

Is this Conflict of Interest?
 
This is a direct theft which needs to be delt forthwith. It is shame up on us leaving everyone to grab even the little remain
 
Hii ndio janja toto ya hawa wazee wa nchi,nae mkuu wa inji kabakia kibya kabisa ati uchunguzi ufanyike? Natamani Rais Paul Kagame wabadilishane na Jk kwa muda wa miezi kadhaa then afanye yale anayoyafanya Rwanda muone hawa jamaa wezi watakavyoshikishwa adabu

Ataiharibu Rwanda!!
 
sasa wakioana ndo nini? out of topic, labda useme makani amefaidi matunda ya ufisadi uliopitia toka kwa mwanae alioupata toka kwa mkwewe. also not a big deal. mi nahisi hiyo hela aliyolipwa ilikuwa ni facilitation fee (kilainishi). Umeona statement ya simon group, wanadai wamelipa mpaka sasa amount ambavyo ina decimal points ndogondogo sana, kwa mtazamo wangu jamaa kastuka kile kilainishi chake kinaweza kupotea kwa hiyo kakiingiza kwenye malipo ili ionekane ni sehemu ya malipo na adhabu kwa mzee kwa kushindwa kulainisha dili. Kwakua mwaga mboga na ugali imeshaanza basi stay tuned utaniambia. Ukitaka kuamini angalia basis za kulipa hiyo amount, why that amount, 10%, 20% etc sio kweli, zile sio sio za manunuzi kabisaaaa. Napigania wazawa, ili uwaumize kwasababu ni wajinga??????????!!!!!!!!!
 
Iddi Simba jaman tumekukosea nini wana wa nchi hii mpaka ututendee hivyo?

.....Wakati mwingine watu wanajuta kuwa Watanzania, sababu ndo Kama hizi!

sasa wewe unataka mrundi akuonee huruma wakati watz wenzako ndio wanampasia ulaji?
 
Wamekutana wote matapeli huyu Robert Kisena maarufu kwa jina la Saimon Agency ni mdhulumaji mkubwa hata huo utajiri wake umetokana nakuwadhulumu wakulima wa pamba. malipo ni hapahapa duniani.
 
Hii ndio janja toto ya hawa wazee wa nchi,nae mkuu wa inji kabakia kibya kabisa ati uchunguzi ufanyike? Natamani Rais Paul Kagame wabadilishane na Jk kwa muda wa miezi kadhaa then afanye yale anayoyafanya Rwanda muone hawa jamaa wezi watakavyoshikishwa adabu
Ndugu yangu, Ni heri Jakaya Kikwete ambaye hajachukua na kuwa na Damu ya Mwanadamu mwilini Mwake, ila ni kuipa rasilimali ambazo atakufa na kuziacha na ametuacha sisi salama na umasikini wetu; Kuliko Huyo Rais Paul Kagame ambaye ana Damu za watu wengi ambao wani waaminifu na hawana hatia, kwasababu ya ulafi wa madaraka akaamua kuingia porini na kuua maadui zake; Heri Jakaya Kikwete simpendi lakini ameniacha huru nakufa na umasikini wangu
 
Back
Top Bottom