Sakata la Jairo, kamati teule ya bunge si halali!

Hivi kwa nini huwa mnapenda kujadili bila kutaja vifungu vya Kanuni au Sheria vilivyokiukwa.
Au kwa sababu mna hakika kuna vilaza wataingia kichwakichwa kujadili bila kudai vifungu hivyo?

let me say danyel is jairo, anatafuta pa kutokea, tangu apewe likizo amekuwa msomaji mkubwa wa magazeti na mtandao wa jf.kaamua kjiunga jana baada ya kuona jf na wananchi wanamnyooshea kidole kila kona..baba jairo karibu ktk hii forum omba ushauri utaelekezwa usiingie kichwa kichwa.

learn to learn! usipende hoja nyepesi.

ufisadi is a very crucial and serious matter to discuss,hata tuwe na mipango mizuri kiasi gani kama ina mianya ya ufisadi na mafisadi wapo tusitegemee kupata ma matokeo mazuri ya mipango yetu.

Dont make everybody stupid.
Kuna ugumu gani katika kuona kuwa ufisadi upo, unashamiri, na unatetewa kwa nguvu zote na wachache waliopo madarakani.
Ni vizuri ukatuambia ni kwa mantiki ipi mtu mwizi,anarudishwa kazini kwa mbwembwe, wananchi wakija juu anarudishwa likizo haraka haraka.
Sasa kinatafutwa kifungu cha kuondolea aibu, halafu mtu mwenye akili timamu anakuja kusema kanuni zimekiukwa kujadili wizi na mwizi.
Ingekuwa mob justice DJ is long and gone to his Creator.

Kumbukumbu za bunge zinaonesha kuwa hoja ya Mh Sendeka kuhusu kuundwa kwa kamati teule ya bunge kuchunguza sakata la Jairo iliungwa mkono baada ya kutolewa lakini haikuafikiwa kwa mujibu wa kanuni za bunge!

Licha ya Naibu Spika kurejea kuisoma kanuni kabla ya kuamua,hakuwahoji wabunge ili hoja iafikiwe au la, kama kanuni inavyotaka mara baada ya hoja kutolewa na kuungwa mkono.inawezekana alipitiwa kutokana na jazba au ni usanii,lakini vyovyote iwavyo kamati teule iliyoundwa si halali kwakuwa haikuridhiwa na bunge.kwa maana hiyo serikali inaweza ikaikataa repoti ya kamati hiyo endapo itagundua mapungufu yanayoidhalilisha.

Licha ya upungufu huo wa kikanuni vile vile kamati teule pia inakwenda kwenye uchunguzi ikiwa inajua aliyewatuma (bunge) anataka nini, hivyo basi kwa kuwa wao pia ni sehemu ya bunge watakuwa kama mshtaki,muendesha mashata na jaji.
Tafakari!!!!!!

Jazba ya Naibu Spika Ndugai niliipenda, tena sana tu.
Ile ilionyesha frustration ya wananchi juu ya kuyumba kwa hali ya juu kwa serikali.
Mtuhumiwa tunaye mkononi na nguo za wizi, halafu mtu anakuja kumsafisha na anatukoga, zile shamrashamra za kumpokea Jairo ni kama anatuambia , mtanifanya nini?, kenge ninyi?
Nafikiri ingekuwa mtaani kwetu Jairo angekuwa historia.

Kumbukumbu za bunge zinaonesha kuwa hoja ya Mh Sendeka kuhusu kuundwa kwa kamati teule ya bunge kuchunguza sakata la Jairo iliungwa mkono baada ya kutolewa lakini haikuafikiwa kwa mujibu wa kanuni za bunge!

Licha ya Naibu Spika kurejea kuisoma kanuni kabla ya kuamua,hakuwahoji wabunge ili hoja iafikiwe au la, kama kanuni inavyotaka mara baada ya hoja kutolewa na kuungwa mkono.inawezekana alipitiwa kutokana na jazba au ni usanii,lakini vyovyote iwavyo kamati teule iliyoundwa si halali kwakuwa haikuridhiwa na bunge.kwa maana hiyo serikali inaweza ikaikataa repoti ya kamati hiyo endapo itagundua mapungufu yanayoidhalilisha.

Licha ya upungufu huo wa kikanuni vile vile kamati teule pia inakwenda kwenye uchunguzi ikiwa inajua aliyewatuma (bunge) anataka nini, hivyo basi kwa kuwa wao pia ni sehemu ya bunge watakuwa kama mshtaki,muendesha mashata na jaji.

Tafakari!!!!!!

Mkuu, main point hapo ni 'kuafikiwa' regardless imetolewa kwa mdomo ama maandishi, ndungai anasumbuliwa na siasa za mabavu, ukabila, jazba, na itikadi, hivyo nafasi ya busara kwake ni finyu mno. Kama wakiwa smart basi yawezekana ni kweli kamati ni batili kwa mujibu wa kanuni, ila kwa kuwa hakuna aliyehoji uhalali wake siku hiyo, tunarudi palepale kwamba ni 'halali' tu, kwa kusema haya na offload uzembe wote kwa ndungai. Mshemiwa, napenda kutoa hoja.

Ishu ya Jairo ni KIINI MACHO ili wananchi wasifikirie madudu ya gvt haswa mgao wa umeme unaosababishwa na mikataba feki hususani ya gesi asilia na umeme wa dharura. Kwa wenye masikio wanalifahamu hilo na kamwe hatuwezi kuwa POYOYO kama magamba

Haya bana! wataleta mizengwe hadi wakatae taarifa. Mhh, siasa...

Kimbunga umenena,na mm naungana na wewe nina mashaka na kamati kama ni utaratibu wa wizara kuwahonga wabunge na wabunge haohao wazichunguze hizo hongo aaaaaah ni kiini macho tu,ndipo ninapomkumbuka rapa wa FM academia dar-es-salaam hakuna mambo watu wanaishi kibongo bongo hakuna mambo,huyu pengine hata shule hakwenda,lakini amegundua watu wanafanya mambo kiujanja ujanja tu.mwizi anamchunguza mwizi we uliona wapi hiyo??????kama sio hapa bongo tu.

Yote ni maigizo tu kwani kuwahoji watu wengi kwa mara moja na ukategemea kupata jibu sahihi ni ishara ya usanii fulani bora ambapo hakuwahoji labda anasubiri mwongozo ili iuundwe kamati nyingine na nguvu ya mlala hoi wa Tz iendelee kusomesha warithi wa nchii kwa mtindo wa kupokezana.

Nashangaa mtoa mada sijui alikuwa amesinzia...! kama unakumbuka, bahada ya mh Ole Sendeka kutumia kanuni ya 117, Naibu spika Job ndugai aliwahoji na wabunge wakakubali, hoja ikapita.

Hata pale aliposimama mh Mkono kuomba utaratibu, naibu spika alimwambia "hoja ikishatolewa uamuzi haipaswi kuzungumzwa tena"

Au mheshimiwa Mkono amekutuma uje umsemee hapa JF kuwa yeye hakuunga mkono hoja?

Aaah ubaya wa jf jairo, mke wake, watoto hata wapambe wako humu kwa hiyo huwezi jua nania anaongea na anataka nini

Nashangaa mtoa mada sijui alikuwa amesinzia...! kama unakumbuka, bahada ya mh Ole Sendeka kutumia kanuni ya 117, Naibu spika Job ndugai aliwahoji na wabunge wakakubali, hoja ikapita.

Hata pale aliposimama mh Mkono kuomba utaratibu, naibu spika alimwambia "hoja ikishatolewa uamuzi haipaswi kuzungumzwa tena"
Au mheshimiwa Mkono amekutuma uje umsemee hapa JF kuwa yeye hakuunga mkono hoja?

naona hoja ya msingi hapa ni namna ambavyo kamati teule inakwenda kufanya kazi, ukizingatia wao ndiyo walalamikaji kwa madai ya kudhalilishwa, mtoa mada alilenga juu uhuru/independence (the committee need to be free from any kind of biasness) katika kumtendea haki jairo.

Kimbunga aliyekamatwa na ngozi ndo aliyeiba mbuzi

Mkuu nani kakamatwa na ngozi, Jairo? Miongoni mwa hadidu rejea za wajumbe wa kamati ni kuangalia mfumo wa ukusanyaji wa hayo mahela serikalini si kwa wizara moja tu!

Back
Top Bottom