Sakata La Gesi Mtwara: Tuache Unafiki na Woga, Tuchambue Mchele na Pumba

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,850
9,405
Taifa letu lipo katika wakati mgumu sana ambao unahitaji maamuzi sio tu MAGUMU lakini pia MAKINI; Lakini Ugumu na Umakini huu Kimaamuzi hatuna budi kuufanya kwa kushirikiana na wananchi wa Kusini badala ya kuwabeza, lakini hasa kuingiza siasa kuliko mantiki katika kulitazama suala zima. Vinginevyo suala la ‘Resource Curse’ ambalo kwa miaka mingi tumekuwa tunalisikia tu kwa wenzetu, sasa litatukuta muda sio mrefu na wahanga watakuwa ni kila mtanzania bila ya kujalisha cheo au uwezo wa fedha; Mengi yameshajadiliwa na wadau mbalimbali kuhusiana na mgogoro huu pamoja na mapendekezo juu ya nini kifanyike ili kuokoa taifa letu lisitumbukie katika janga la ‘resource curse’; Muhimu hapa ni kuwaweka wananchi wa Kusini at the ‘Centre’ katika suala zima la gesi asilia na economic development, sio kuwaweka at the ‘Periphery’. Pia ni muhimu serikali ikatambua kwamba wananchi wa kusini wanazidi kuelimishwa kwamba faida kwao itatokana zaidi na ubora wa ‘Natural Gas Policy’, ambayo kwa bahati mbaya, tayari tunaingia katika mikataba mikubwa huku ‘Natural Gas Policy’ ikiwa katika hatua ya ‘Draft Document’; Ni masuala kama haya ndio yanachangia sana kwa serikali ‘to shoot on its own foot, na mbaya zaidi, tiba zinazotatumiwa kutibu jeraha ni tiba ambazo zinazidi kuchimba kidonda kuliko kukikausha. Ni muhimu kwa viongozi wa Serikali sasa kuja na maamuzi magumu na makini ambayo yatalenga kurudisha imani ya wananchi wa mtwara kwa serikali yao; Huu sio wakati wa siasa za ubabe na arrogance, na pia vyama vyote vya siasa ni vyema vikaliondoa suala hili majukwaani na badala yake kutafuta mazingira ya kukaa meza ya pamoja na kulifanya suala hili kuwa ‘bipartisan’ kama kweli nia ni kurudisha hali ya amani na utulivu katika taifa letu;

Leo hii, Tanzania inakadiriwa kuwa na utajiri wa gesi asilia unao karibia 43 trillion cubic feet; Hifadhi hii inakadiriwa kuwa na thamani ya dollar za kimarekani karibia Billion 450, ambayo ni sawa na karibia Shillingi trilioni 730; US geological Survey inakadiria uwepo wa hifadhi kubwa zaidi na kwamba tafiti zinazoendelea zitabainisha uwepo wa gesi wa karibia 441 trillion Cubic feet; Nyingi ya gesi hii inakadiriwa kuwepo katika maeneo ya Pwani ya Afrika mashariki, huku Tanzania ikiwa ni sehemu kubwa ya eneo hilo; Ni kwa maana hii, inakadiriwa kwamba miaka kumi ijayo, Tanzania itakuwa ni moja ya mataifa yanayozalisha gesi asilia kwa wingi Duniani; Na ni kwa mantiki hii ndio maana kampuni mbalimbali za sekta ya gesi duniani kama vile British Gas imejipanga kuwekeza Tanzania Dollar billioni 15 (kumi na tano) sawa na shillingi trilioni 24 (ishirini) na nne kwenye sekta ya gesi nchini katika kipindi cha miaka kumi ijayo; Tufahamu kwamba Dollar Bilioni Kumi na Tani ni zaidi ya nusu ya pato la sasa la nchi (GDP) ya Tanzania!!!

Migogoro yote itokanayo na rasilimali aka ‘natural resource curse’, chanzo chake huwa ni tatizo la rent-seeking behavior na short terms gains on part of politicians and other public officials;Watanzania wanazidi kuchoka kuishi na ahadi za kisiasa majukwaani wakati wa kampeni za chaguzi kuu mbalimbali; Vinginevyo katika suala la rasilimali kama hizi (gesi), suala la faida kwa wananchi ni suala la common sense, kwani halihitaji rocket science kutambua kwamba ukosefu wa culture of transparency katika mikataba, hasa isiyoshirikisha wadau; Ndani ya dunia ya leo inayosukumwa na nguvu za utandawazi, wananchi hawahitaji kufundishwa na mtu yoyote kutambua kwamba the expected ‘revenues and investments’ from Gas, Oil, or Gold ni lazima zisaidie nchi to shift towards industrialization na kuzalisha ajira, huku pia mapato kupitia kodi yakienda kuboresha miundo mbinu, sekta za afya, elimu, na maji; Na katika haya, ni common sense kwamba wananchi wa kupewa kipaumbele ni wa vijijini, lakini hasa wale ambao wapo nyuma kimaendeleo kulinganisha na wananchi wa mikoa mingine;

Sasa inapotokea kwamba rasilimali husika inatokea maeneo yao lakini hakuna transparency katika mchakato mzima wa utilization ya rasilimali husika, migogoro lazima itajitokeza; Ni kwa mantiki hii, wananchi wa kupewa kipaumbele katika hili ni wananchi wa mikoa ya kusini ambao kwa zaidi ya miaka 50 wamekuwa hawapewi kipaumbele in terms of economic development ikilinganishwa na sehemu nyingine nyingi za nchi; Kwa maana hii, ingawa ni sahihi kusema kwamba Gesi ya Mtwara ni ya Watanzania wote, lakini pia ni sahihi kusema kwamba kwa simple logic tu ya ‘sustainability’ – kisiasa, kiuchumi, kijamii na kimazingira, faida ya gesi hii ni lazima iwe wazi kwanza pale inapotoka (source); Hivi ndivyo mataifa yaliyoendelea yalifanya; Kwa kuzingatia tu ‘simple economics’, mkoa wa Mtwara una mazingira yote muhimu yanayokidhi approach ya namna hii; kwa mfano, Mtwara tayari kuna Bandari, kuna nguvu kazi iliyo ‘idle’ ambayo kutokana na sera mbovu za serikali, nguvu kazi hiyo imegeuka kuwa wachuuzi nchi nzima, pia Mtwara ina eneo kubwa la Ardhi kwa ajili ya maendeleo ya Kilimo na Viwanda; Muhimu zaidi, Mtwara ni a better gateway kwa maendeleo ya uchumi ndani ya SADC Zone; Ni masuala kama haya ndio yanawia vigumu watu wengi kuamini kwamba ni Lazima gesi itokea kwanza Mtwara kwenda sehemu nyingine ya nchi, halafu wananchi wa mtwara waje kupata faida za gesi hii baadae; Hata simple economics zinazozingatia factors nilizojadili hapo juu zinathibitisha kwamba approach ya is not the best alternative kiuchumi; pengine; it’s the best alternative kisiasa, hasa in the context of rent seeking behavior and short terms gains kwa wahusika;

Ebu tuujadili mkoa wa Mtwara Kidogo

Duniani kote, GDP Per Capita ni kiashiria (indicator) cha hali ya wananchi kiuchumi i.e. kipato/income. Zifuatazo ni takwimu za pato la kila Mtanzania kwa mwaka 2010 - Nimechukua kumi bora na kuziweka in ‘order of ranking’:

Jedwali la Kwanza: Vipato Vya Watanzania Kulingana na Mikoa Wanayotoka (GDP Per Capita)
MKOA
PATO LA KILA MWANANCHI KWA MWAKA (T.Shillings) (2010)
1. Dar-es-salaam
1,740,947 (million)
2. Iringa
979,882 (laki)
3. Arusha
945,437
4. Mbeya
892,877
5. Kilimanjaro
879,432
6. Ruvuma
866,191
7. Mwanza
829,647
8. Tanga
763,203
9. Morogoro
744,234
10. Rukwa
726,658
Source: Bajeti Za Serikali.

Tukitizama jedwali namba moja, Mikoa ya Kusini (kama Mtwara) haipo katika orodha hii; Je, hii ni kwa sababu gani? Pengine tutazidi elewa ndani ya mjadala wetu baadae, lakini kwa sasa tutazame takwimu nyingine:


  • Je, ni Mikoa ipi inachangia Zaidi Kwenye Pato la Taifa/Inayozalisha Bidhaa na Huduma Nyingi Zaidi Tanzania (GDP)?

Jedwali la Pili: Kumi Bora Kwa Uzalishaji Wa Bidhaa na Huduma (GDP).
MKOA
UZALISHAJI WA BIDHAA NA HUDUMA (GDP) T.shillings (2010)
1. Dar-es-salaam
T.sh 5.4 trillioni
2. Mwanza
T.sh 3.0 trillioni
3. Mbeya
T.sh 2.3 trillioni
4. Shinyanga
T.sh 1.9 trillioni
5. Iringa
T.sh 1.7 trillioni
6. Morogoro
T.sh 1.6 trillioni
7. Arusha
T.sh 1.5 trillioni
8. Kilimanjaro
T.sh 1.3 trillioni
9. Kagera
T.sh 1.3 trillioni
10. Ruvuma
T.sh 1.2 trillioni
11. Tabora
T.sh 1.2 trillioni
12. Rukwa
T.sh 1.1 trillioni
Source: Bajeti Za Serikali.

Vile vile, tukitazama jedwali la pili hapo juu, mikoa ya kusini (e.g. Mtwara) pia haipo katika kumi bora katika mchango wa uzalishaji na pato la Taifa; Swali linalofuata ambalo ni la kimantiki zaidi hasa kiuchumi kuliko siasa ni je:

  • Kwanini sasa tusitumie fursa hii ya gesi asilia mikoa ya kusini kuigeuza mikoa hii na yenyewe iwe na mchango kwa pato la taifa?

Binafsim nadhani ugunduzi wa gesi ya Asilia ndio fursa pakee iliyopo ya kuifanya mikoa ya kusini nayo iwe na mchango mkubwa kwa pato la taifa kupitia uwekezaji utakaotokana na mapato ya gesi; Nasema kwamba ni fursa pekee kwa sababu kwa miaka zaidi ya hamsini, wananchi wa kusini kama nilivyokwisha jadili, wamekuwa wakipuuzwa kimaendeleo; Inaonekana kwamba sera ya serikali ni kuwekeza katika maeneo yenye michango mikubwa kwa pato la taifa (GDP contribution) na ushahidi katika hili upo kwenye takwimu juu ya vipaumbele vya bajeti kwa mikoa mbalimbali kila mwaka; Ushahidi wa hili upo katika jedwali lifuatalo:

Jedwali la tatu: Mikoa Yenye Michango Midogo Katika Uzalishaji/Pato la Taifa (bottom 5).

MKOA
UZALISHAJI WA BIDHAA NA HUDUMA (GDP) T.shillings (2010)
1. Singida
T.sh Billioni 661
2. Pwani
T.sh Billioni 608
3. Lindi
T.sh Billioni 621
4. Kigoma
T.sh Billioni 906
5. Mtwara
T.sh Billioni 927
Source: Bajeti Za Serikali.

Tukitazama jedwali la tatu, tunaona Mtwara, Lindi na mikoa mingine kwamba ni ya mwisho kabisa katika kuchangia pato la taifa (GDP contribution in terms of production of Goods and Services); Note pia Kigoma ni sehemu ya orodhahii na hatupo mbali na mgogoro mwingine mkubwa katika mkoa huu; Vinginevyo si ajabu ndio maana mikoa hii imekuwa ikitengewa fedha ndogo katika bajeti za kila mwaka kama tunavyoona kwenye jedwali namba nne hapo chini:

Jedwali la nne: Mikoa inayotengewa fedha ndogo za Bajeti (bottom five)

MKOA
BAJETI YA MWAKA (T.sh) (2010)
1. Mtwara
T.sh Billioni 57
2. Kigoma
T.sh Billioni 56
3. Singida
T.sh Billioni 50
4. Manyara
T.sh Billioni 54
5. Rukwa
T.sh Billioni 49
Source: Bajeti Za Serikali

Je ni mikoa gani ambayo inapewa kipaumbele katika kila bajeti? Jibu ni – Mikoa ile ile ambayo ndio inachangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa (GDP) kama ambavyo tuliona katika jedwali namba mbili hapo juu; Mikoa hiyo pamoja na kiasi cha fedha wanazotengewa katika bajeti ni kama ifuatavyo:

Jedwali la tano: Orodha ya kumi bora – vipaumbele katika Bajeti Ya Serikali.

MKOA
BAJETI YA MWAKA (T.sh)
1. Dar-es-salaam
T.sh Billioni 154
2. Mwanza
T.sh Billioni 135
3. Mbeya
T.sh Billioni 109
4. Shinyanga
T.sh Billioni 104
5. Kilimanjaro
T.sh Billioni 100
6. Tanga
T.sh Billioni 92
7. Kagera
T.sh Billioni 88
8. Morogoro
T.sh Billioni 86
9. Iringa
T.sh Billioni 85
10. Arusha
T.sh Billioni 81
Source: Bajeti Za Serikali


Hitimisho

Njia pekee ya ya serikali kutegua bomu lililopo ambalo linaweza pelekea nchi yetu kuingia katika machafuko yasiyokuwa ya lazima ni kwa kuzingatia hoja nilizojenga huko juu; Nimeelezea kwa hoja na takwimu juu ya jinsi gani mikoa mingi ikiwepo ya kusini mwa Tanzania imekuwa ikipuuzwa kimaendeleo kwa miaka zaidi ya hamsini kutokana na sababu moja tu kubwa - Kutokuwa na mchango wa maana kwa pato la taifa; Kama nilivyobainisha kwa hoja na takwimu, mikoa inayopewa kipaumbele katika bajeti zetu ni ile inayochangia zaidi katika pato la taifa (GDP); Kwa mantiki hii, ni muhimu kwa Serikali kusikiliza vilio vya wananchi wa kusini ili na wao wawe sehemu ya mikoa iliyopo katika jedwali namba tano hapo juu; Vinginevyo, kama nilivyokwisha sema awali, the government is shooting on its own foot, na mbaya zaidi, its prescribing tiba ambayo sio sahihi, huku kidonda kikizidi kuchimbika; Sidhani kama serikali ina nia ya kuendelea kuzembea katika hili na kupelekea mguu kukatwa na madaktari kama njia pekee itakayobakia kutibu tatizo;

Cc: invisible, revolutionarytz, nguruvi3, EMT, et al…
 
Japokuwa umetumia njia ndefu sana kuelezea lakini kwa kutumia busara ya kawaida ni kuwa serikali (soma majambazi) inapigania matumbo yao. Hivyo vyote ulivyoelezea sio kama hawavijui bali haviwalipi! Haya majambazi hayataeleweshwa kwa takwimu bali kwa action!
 
Mchambuzi Yoote hayo umeandika yanafahamika na hakuna jinsi ambavyo Tanzania inaweza kuepuka hiyo unayoiita resource curse, na sababu ni moja tu UTAMADUNI, hatuna Utamaduni ambao unaweza kujenga jamii yenye mpangilio wa Maisha, Jamii ambayo inaweza ikajenga Nchi yenye kustaarabika, sisi woote tumelelewa na kukuzwa na huu Utamaduni na hakuna Miujiza, mtaongea mnavyotaka, mtawanukuu wasomi wa Kizungu mnvyotaka lkn mwisho wa siku nakuhakikishia hakuna jipya Tanzania wala Afrika, kwa maana Utamaduni wetu ndio adui yetu Mkubwa!

Na Wazungu wanalijua hilo na ndio maana kuna msemo unasema Africans are not ready to rule themselves sasa aliyetunga huo msemo hakuutoa hewani, alijua alichokuwa anakisema, kwa nini hakusema Wahindi au Wachina?

Hivyo nenda mbele rudi nyuma hizo Rasilimali hazitaondoa umaskini Tanzania hata kwa miaka 200 ijayo hata aje Kiongozi gani maadamu amezaliwa na kulelelwa Tanzania hakuna miujiza!
 
Last edited by a moderator:
mkuu Mchambuzi heshima kwako!
kwanza nikushukuru kwa uchambuzi yakinifu, umeelezea kwa undani na kwa kina kwa mtu yeyote makini atakuwa amekuelewa, binafsi nnaunga mkono hoja,
Gesi inaweza kutumiwa na serikali ya ccm kuamsha kama si kukuza mapato yanayokusanywa kutoka kusini, Gesi ni tunu ambayo wanamtwara kamwe hawapaswi kukubali kuipoteza.
 
Last edited by a moderator:
Ni muhimu kwa viongozi wa Serikali sasa kuja na maamuzi magumu na makini ambayo yatalenga kurudisha imani ya wananchi wa mtwara kwa serikali yao; Huu sio wakati wa siasa za ubabe na arrogance, na pia vyama vyote vya siasa ni vyema vikaliondoa suala hili majukwaani na badala yake kutafuta mazingira ya kukaa meza ya pamoja na kulifanya suala hili kuwa ‘bipartisan' kama kweli nia ni kurudisha hali ya amani na utulivu katika taifa letu;

…

Maamuzi haya magumu ni pamoja na kuweka mikataba wazi, sio kila kitu kijibiwe kisiasa.

Pia topic nzito kama hii nashauri wadau msiwajibu akina Chris Lukosi na ndugu zake wakija hapa kuvuruga mijadala mizito kama hii.
 
Last edited by a moderator:
MchambuziKwa muda sijaona uchambuzu wako hspa. Ninakubaliana kabisa kuwa tunaelekea kwenye 'resource curse'. Kwa vile wanaotupeleka nuko ni wanasiasa (siamini kama ni serkali), ninakubaliana na ushauri wako kuwa vyama vya siasa vinapaswa kuweka pembeni tofauti zao na mapenzi yao kwa vyama vyao katika suala la raslimali. Kwa hiyo ni jukumu la Serkali kuwaunganisha hawa wanasiasa ili kuweka sera ya pamoja ya utawala na mfumo wa kusimamia raslimali zetu. Ninaamini kuwa raslimali hizi ikiwemo gesi, mafuta, madini n.k ni mali ya taifa zima na lazima zitumiwe kwa manufaa ya taifa zima. Lakini pia ninaamini kuwa pale raslimali hizi zinapotoka lazima wapate manufaa yake zaidi na kwanza. Kwanza hawa wakifaidika nazo watakuwa walinzi wake wakuu.Hata tatizo kubwa hapa ni mikataba tuliyokwishajifunga kwa usiri mkubwa. Inaonyesha nguvu hizi zinazotumika inawaaminisha watu kuwa kuna kitu ambacho wanasiasa wetu wa chama tawala wanajaribu kukilinda. Tunajua kabisa katika suala hili nguvu haxitatui bali zinakoleza tu. Mifano ni mingi na najua waheshimiwa wabunge na mawaziri wanaijua katika nchi ambazo mpaka leo hazijatulia kwa sababu ya raslimali. Wekeni tofauti zenu na kujaribu kulaumu kila upande hadharani kwa political gain kutuokoa kutoka kwenye janga.
 
Njia pekee ya ya serikali kutegua bomu lililopo ambalo linaweza pelekea nchi yetu kuingia katika machafuko yasiyokuwa ya lazima ni kwa kuzingatia hoja nilizojenga huko juu; Nimeelezea kwa hoja na takwimu juu ya jinsi gani mikoa mingi ikiwepo ya kusini mwa Tanzania imekuwa ikipuuzwa kimaendeleo kwa miaka zaidi ya hamsini


Mkuu
Mchambuzi
Mikoa ya Kusini inapuuzwa na itaendelea kuupuzwa kama wanamtwara wenyewe wasipoamka.Nafikiri gharama za kuipeleka gesi Dar kwa bomba ni kubwa kuliko gharama za kujenga hicho kiwanda cha kuzalisha umeme huko Dar. Mpaka sasa nashindwa kuelewa kwa nini wanag'ang'ania kuipeleka gesi Dar es salaam?

Kwangu Mimi binafsi Nawaunga mkono watanzania wenzangu wa Kusini wasiukubali huu mradi wa kuipeleka Gesi Dar. hata kama ikibidi kumwaga damu ni bora wafanye hivyo kuliko kudharauliwa na Watu wachache wanaojiita viongozi kumbe ni Mafisadi wanaoiba rasilimali zetu kwa kuwatumia wawekezaji.
 
Mchambuzi binafsi sijawahi kufatilia wala kusoma popote takwimu za mikoa inayotengewa bajeti ndogo.
Umenifungua sana ndugu yangu.Thanks JF maana bila uwepo wake tungeendelea kusoma heading za magazeti yetu uchwara.
 
Last edited by a moderator:
Mchambuzi Hongera sana, bila kujali itikadi yako hii imekaa kisomi sana na italeta tija kwa taifa. Huyu Jamaa anaitwa Lukosi ni heri asingechangia kabisa mana ukiwa mpumbavu na hutaki watu wafahamu upumbavu wako ni heri ukae kimya.
 
Mchambuzi umefafanua vema sana,huyu lukosi apotezewa tu kwani tushaijua rangi yake na hila zake. Back to point,ni kwamba simple analysis..kwann Makinda kazuia mijadala ya wizara ya nishati bungeni kuhofia kwamba watakuwa wanamwaga mafuta juu ya moto? Ni kwamba kuna vitu ving havipo wazi na usiri mkubwakatika suala hili la gesi asilia. Na naamini baadh ya wabunge walikuwa tayari kueleza umma usiri huo ndani ya bunge. Ni ukweli usiopingika kwamba sisi wananch wa Mtwara kuna kitu tunafichwa kuhusu hii gesi. Haiwezekani tayari kuna matatizo halafu Rais anasema eti "gesi ni ya watanzania wote"...atakata mapembe wote walio nyuma ya mgomo. Kwani ges ikibakia mtwara haiwi na manufaa kwa watz wote!mpaka iende kinyerezi au bagamoyo? Kwahyo hadi ifike dar ndo iwe ya watz wote?thz is real crazy...kwann LNG ndio isijengewe bomba liende kinyerezi,mpaka watake raw ges!halafu mtwara tuendelee kubaki maskin sio. JK ana maslah yake binafsi,thtz all..na sisi tutakaza tu, HAITOKI NG'OOO,!
 
CCM hakuna think tank ya kufanya analysis kama hii, wenyewe kila kitu CHADEMA kama vile watanzania hawezi kufikiri, kuhoji na kupambana bila CHADEMA.

Mchambuzi this is a billion dollar public lecture given free of charge.
 
Chris Lukosi,

Ni dhahiri umekosa ujasiri sio wa kujibu tu hoja yangu kwa hoja, lakini pia kuisoma yote na kuielewa; Umeishia kwenye kichwa ambapo hata hivyo kwa kauli ya 'tuache' ni dhahiri kwamba hata mimi naweza kuwa na hulka ya kinafiki na woga, lakini katika hili nimeamua kuuvua unafiki na woga;

Naomba nikurudishe kwenye mwongozo wa chama japo kwa muda mfupi - Mwongozo wa CCM una kanuni moja muhimu sana isemayo kwamba: Kukosoa na Kukosolewa Ndio Silaha ya Mapinduzi; kanuni hii inahimiza viongozi na wanachama kuwa tayari kukosolewa bila ya kuhamaki kwani hiyo ndio njia pekee ya kujenga chama chetu cha mapinduzi; Lakini kwa vile wewe ni 'pumba' katika chama, hauna ufahamu wa kanuni kama hizi, badala yake wewe ni mwana ccm mchumia tumbo na ulikiri mwenyewe kwa uwazi kabisa jinsi gani ulijipendekeza kwa Dr. Slaa na jinsi gani sasa umeamua kujipendekeza wa wakubwa huko CCM kwa maslahi binafsi; ndio maana baina yangu na wewe, linapokuja suala la kujipendekeza, ni dhahiri kwamba wewe ndie nguli, kwani upo CCM kwa kutarajia miradi yako fulani fulani itafanikiwa; Pole sana kaka Lukosi kwani huo ni Mkosi wa kisiasa in the making;

Naomba niende mbali zaidi katika maandiko yetu ya chama (CCM) na kumnukuu Mwalimu Nyerere ambae miaka zaidi ya hamsini iliyopita, aliwajadili wanachama wa ovyo kama wewe bila ya uwoga wala unafiki; Mwalimi alisema hivi katika kitabu chake cha Tujisahihishe:

["Ukiondoa matatizo wayapatayo binadamu kwa sababu ka
m
a mafuriko, nzige, kiangazi, n.k, matatizo yao mengi hutokana na unafsi. Unafsi ni wa aina nyingi. Swali ambalo twalisikia mara kwa mara, "Hali yetu ya baadae itakuwaje?", ni swali ambalo sina shaka kuna wanaouliza kwa nia safi kabisa. Lakini mara nyingi linatokana na unafsi. Mtu anayeuliza anafikiri TANU iliundwa kwa faida yake binafsi. Ni kama kwamba TANU ilipoundwa ilimwahidi kwamba ikiwa atakubali kuwa mwanachama, au kiongozi, basi TANU itamfanyia yeye jambo fulani kama tunzo! Anasahau kabisa kuwa TANU inajishughulisha na haja za Jumuiya kwa ujumla. Lakini kwa mtu wa aina hiyo, hata kama TANU inatimiza madhumuni yake kwa jumuiya, ataona kuwa ni umoja ambao hauna maana kwa sababu haumtimizii haja zote za nafsi yake. Huu ni unafsi. Kama wanachama wa TANU, na hasa viongozi, hawatakihukumu chama chetu kwa mahitaji na nafsi zao wenyewe, chana hakitadumu. Wanachama wa aina hiyo ni ugonjwa katika chama.

Dalili nyingine ya unafsi, na ambayo ni ugonjwa mbaya sana ni fitina. Kanuni moja ya TANU inasema hivi: "Nitasema Ukweli Daima. Fitina Kwangu ni Mwiko." Lakini bado tunao wanachama ambao ni wafitini wakubwa bila kujitambua. Ni wa aina mbali mbali. Wengine humwona mwenzao anafanya kosa. Badala ya kumwambia pale pale kijamaa kwamba atendalo ni kosa, watanyamaza kimya. Lakini hawanyamazi kabisa. Watakwenda kumteta katika vikundi vya siri. Mateto haya si ya kumsaidia mwenzao, ni ya kumdhuru. Hii ni aina moja ya fitina. Wengine hugawa watu katika mafungu. "Fulani" japo kafanya kosa kubwa sana hasemwi. Lakini "Fulani" wa pili akifanya kosa japo dogo, kosa lile hukuzwa likawa kama mlima Kilimanjaro. Hawa hutafuta sababu ya kumtetea "Fulani" wa kwanza, au za kumaulumu "Fulani" wa pili, ambazo hazifanani kabisa na ukweli. Kwa watu wa aina hii, ukweli ni jambo ambalo hutegemea mtu, si kitu kinachojitegemea chenyewe bila kujali mtu. "Fulani" wa kwanza akisema katika majadiliano kuwa mbili na mbili ni tano, wao watakubali. Lakini "Fulani" wa pili akisema sivyo, mbili na mbili ni nne, watamwona ni mtu mbaya kabisa ambaye hastahili hata kusikilizwa. Hawa hawajali ukweli, hujali nafsi tu. Kwao, ukweli ni maoni yao na matakwa yao. Hatuna budi, hasa katika majadiliano na mazungumzo yanayohusu jumuiya, tujifunze kusikiliza hoja zenyewe zinazotolewa na wenzetu, na kuzijibu zile hoja kwa kuzikubali au kuzikataa, bila kujali kama anaezitoa ni rafiki au si rafiki. Pia wanaopingwa hawana budi wakubali kuwa kinachopingwa ni zile hoja zao, sio wao wenyewe. Bila mazoea haya, mazungumzo hayana maana; yanakuwa ni kupoteza wakati, maana huwa tumekwisha kuzihukumu hoja za mtu hata kabla hajazitamka; kadhalika, hoja zetu zikijibiwa kwa kupingwa halafu tunawakasirikia waliozipinga tunafanya mazungumzo yasiwe na maana, kwa sababu tunapenda hoja zetu zikubaliwe tu hata kama si hoja safi.

Ukweli una tabia moja nzuri sana. Haujali mkubwa wala mdogo; haujali adui wala rafiki. Kwake, watu wote ni sawa. Pia ukweli unayo tabia ya kujilipiza kisasi kama ukipuuzwa. Ukiniona nataka kulipiga teke jiwe kwa kuwa unafikiri kuwa ni dongo au mpira, natumaini utanionya. Lakini nikilipuuza onyo lako kwa sababu eti wewe ni mdogo au kwa sababu sikupendi, nikalipiga teke, basi litanivunja dole japo ningekuwa nani.Ukweli haupendi kupuuzwa.


Wakati mwingine, mtu tunayempinga huwa ana makosa kweli lakini hoja tunazozitoa ni za kinafsi na hazihusiani kabisa na hoja zake. Nikisema mbili na tatu ni sita, nakosa. Lakini ni bora kunionyesha kwamba pengine nafikiri tunazidisha kumbe tunajumlisha. Ni kweli mbili mara tatu ni sita; lakini mbili na tatu ni tano, siyo sita Lakini ukijaribu kuwashawishi wenzetu wakatae mawazo yangu na kukubali yako kwa kusema kuwa meno yangu ni machafu, au natoa kamasi daima, utakuwa unatumia hoja ambazo hazina maana. Huu ni mfano wa upuuzi; lakini mara nyingi hoja tunazotumia kuwashawishi watu wakatae mawazo ya wale tusiowapenda, au kukubali mawazo yetu, huwa hazihusiani kabisa na mambo tunayoyajadili.

Makosa yetu mengine hutokana na woga; woga unaotuzuia kumlaumu mkubwa japo tunajua kuwa kakosa, au unaotuzuia kumtetea mdogo anayelaumiwa na wakubwa japo tunajua hana makosa. Na msingi wa woga ni unafsi. Pengine huwa tunaogopa sisi wenyewe kulaumiwa au kupata hasara fulani. Pengine twaweza kuwa hatuna cheo chochote ambacho tunaogopa kupoteza; pengine huwa hatuna tamaa yoyote ya kupata cheo fulani. Lakini woga unaweza kutokana na tamaa ya kila binadamu kupendwa na binadamu wenzake. Sisi sote tunayo tama hii, au sivyo tusingekuwa binadamu. Woga huu huweza kumfanya mtu kuvumilia maovu, hasa kama maovu yale yanatendwa na walio wengi kwa walio wachache, au yanatendwa na wakubwa kwa wadogo. Kwa kuogopa kuwaudhi wengi tunawaacha watende makosa bila kuwasahihisha, wasije wakatuchukia. Huu ni unafsi mbaya sana Ni kweli kwamba demokrasi haiwezi kudumu ikiwa wachache watakubali matakwa ya wengi. Lakini matakwa ya wengi hujulikana katika majadiliano au mazungumzo wa wazi.

Kadhalika, matakwa ya wachache hujulikana katika majadiliano na mazungumzo. Bila wachache kusema wazi wazi matakwa yao, majadiliano hayana maana. Wakati mwingine, hata baada ya majadiliano, wachache – japo wamekubali kutii uamuzi wa wengi wanaweza kuendelea kuamini kwamba mawazo yao ni sawa, na ya walio wengi yamepotoka. Demokrasi inawapa haki, na ukweli unawapa wajibu wa kuendeleza mawazo yao mpaka wengi waone kuwa ni ya kweli. Bila hivyo Maendeleo katika mawazo hayawezekani, kwani mara nyingi wazo zuri hutokana na mtu mmoja tu. Mwanzo laweza likapingwa, pengine kwa nguvu kabisa, na walio wengi, lakini hatimaye wengi hulikubali. Huu ndio msingi wa Maendeleo katika mawazo ya binadamu.

Makosa ni makosa na dhuluma ni dhuluma, japo watendao makosa hayo au dhuluma ile ni wakubwa au ni wengi. Chama kinachopenda ukweli na haki hakina budi kiwape wanachama wake uhuru na nafasi ya kusahihisha makosa na kuondoa dhuluma. Wanachama hawana budi waone kuwa ni wajibu wao kuutumia uhuru huo, na nafasi hiyo. Wanachama wasiotumia uhuru huo na nafasi hiyo, kwa sababu ya kuogopa kuchukiwa au kupoteza nafasi zao, wanafanya kosa kubwa la unafsi, ambalo ni adui wa haki na ukweli."]

Lukosi, kwa kweli inasikitisha sana kuona jinsi gani unazidi kujidhalilisha mbele ya umma, lakini pengine ni kwa sababu wanachama 'pumba' kama wewe ndio wanaonekana ni wa maana Lumumba; Pengine viongozi wengi wa CCM (sio wote hakika) wanatamani sio tu wanachama bali wananchi wote wangekuwa na sifa kama zako kwani hiyo ingesaidia sana chama kuzidi kupaa badala ya kuzidi kupwaya katika medani za siasa kutokana na madhaifu yake mengi ambayo, hao viongozi unaowasujudia wanayajua na mwalimu anawazungumzia (rejea tujisahihishe), lakini kwa vile wewe umekubali kuwa ignorant na hali halisi ya chama leo, umeamua kuvua kabisa dignity yako na kuacha hata wadogo zako wa mbali kabisa wakibakia kupigwa na butwaa jinsi gani umekuwa ni mtumwa wa wakubwa; Wakubwa hawa watasfaafu na kwenda zao katika pindi ambacho wewe utakuwa ndio kwanza in your middle age, katika kipindi muafaka kabisa cha kujenga career yako kisiasa; Hao hao viongozi unaowaabudu sasa na madhaifu yao, ukija kuwafuata baadae kwa misaada utaambuliwa maneno tu kwamba "mimi sasahivi mstaafu bwana..."; Hivi utajificha wapi pale tabia zako za leo zitakapokuja kukusuta? Ndio maana watu kama wewe the only way out ni kuhakikisha CCM inabaki madarakani come what may; Hamna jeuri ya kukubali kwamba sasa CCM is no longer the only political expression of the state, bali that right ipo kwa vyama vyote vya siasa Tanzania; Its because of your ignorance, unachanganya political expression of the state and political expression of the government, hivyo kutuona sisi ambao ni sehemu ya the state kama ni maadui wakati kimsingi tunachofanya ni kutumia haki yetu kikatiba; Nakuonea huruma sana, hasa kutokana na ukweli kwamba umejitokeza in terms of identity kwani unajulikana wazi ni nani, na mbaya zaidi, rekodi zako zitadumu humu daima;

Turudi katika hoja iliyo mbele yetu;
 
Mkuu Mchambuzi, heshima kwako...

In principal nakubaliana na hoja zako karibu zote. Ila suala la kutenga bajeti kubwa kwenye mikoa yenye kuchangia zaidi katika GDP naona kama ni coincidence. Hii ni kutokana na ukweli kuwa mikoa hii inayochangia zaidi kwenye GDP ina idadi kubwa ya watu na miundombinu hafifu zaidi ambayo serikali inalazimika kuwekeza kidogo ilichonacho ambacho hakitoshelezi huko. Nina uhakika ukichukua hizo allocated budgets ukagawanya na idadi ya watu unaweza kukuta Mtwara na Lindi hazitofautiani sana na sehem nyingine (Unaweza kusaidia kugawanya ili tusio na takwimu tujiridhishe)

Mi naona tatizo kubwa kabisa ni serikali ya CCM kushindwa kujitathmini mara kwa mara na kufanya mabadiliko ya sera pale ambapo mambo hayaendi. Kwa mfani sera ya madini imeshindwa, tulitegemea approach ya kwenye gas ingeangalia tumejikwaa wapi kwenye madini hivyo huku kwenye gesi turekebishe. Ujinga ni wakati wa kwenda na kurudi tunajua pabaya na pazuri, but kwa NYIE maCCM ujinga ni kwenda na kurudi. Tuna approach gas in the same way as madini mengine halafu tunajidanganya kupata MIJI YA VIWANDA. Swali, mbona Geita sio mji wa viwanda licha ya deposit kubwa ya dhahabu iliyokuwepo? Mbona Buhemba sio mji wa viwanda? Mbona hospitali za Nyamongo hazina dawa licha ya kulalia madini ya kufa mtu?? CCM ijitathmini itaendelea hadi lini kuuza rasilimali zetu kwa wageni?
 
wanajua ila ni wanafiki sana hawa viongozi walioko madarakani na wanaishi kimazoea kuwa wananchi hawaelewi lolote kwa viongozi wa serikali "UZALENDO NI KUKUBALI KILA WANALOLIHITAJI VIONGOZI WALIOKO MADARAKANI NA KUKAA KIMYA WANAVYOFANYA MAMBO YAO KWA SABABU WAO NDIO MIUNGU WA WATANZANIA NA KAMWE HAWAKOSEI KATIKA MAAMUZI YAO" KWA MTAZAMO HUU INATUPATIA MACHUNGU MAKUBWA MNO SISI WATU WA KUSINI NA WATANZANIA WENYE MAPENZI MEMA NA HIVI WANADILIKI HATA KUWAAMINISHA WATANZANIA WENGINE KUWA NI WABINAFSI,,,SASA WABINAFSI KATIKA LIPI??WANAKUSINI SIO WABINAFSI HATA KIDOGO NA KWANINI UBINAFSI USIWE ULE UCHIMBAJI AU UPANUZI WA BANDARI YA BAGAMOYO NA HUKU ZIKISUSIWA ZILE ZA TANGA NA MWARA???NINI MAANA YA UBINAFSI BY THE WAY!!!!!WANAKERA SANA HAWA JAMAA...
 
Unaelewa unachokisema mkuu, tatizo langu ni moja tu, unataka serikali isikilize vipi kilio cha wanamtwara? Kinachohitajika Dar na sehemu zingine za nchi ni gesi na mitambo y kusafisha itajengwa mtwara. Umeme mtwara upo wa gesi kwa hiyo kama wawekezaji wanataka umeme wataenda. Tatizo, wawekezaji hawafuati umeme, wanataka kuwa karibu na soko. Wangekuwa wanafuata umeme tu, mikoa yote Ingekuwa na uwiano sawa wa viwanda. Serikali haijengi viwanda tena, mtwara wanataka nini?
 
Sioni sababu yoyote ya maana kwa Mchambuzi kuweka figures hapo juu. Kama kipato ni kidogo hiyo ni sababu tosha serikali ichukuie hatua za makusudi kuinua mikoa hiyo ili iende sambamba na mikoa mingine. IKUMBUKWE KWAMBA WAKATI MAREHEMU SOKOINE ALIPOTEMBELEA MIKOA HIYO SERIKALI ILITOA uamuzi wa kupunguza bei za nguo kwa mikoa hiyo ili waweze kununua nguo kwa bei nafuu.

Hatuwezi kuwaacha watanzania wengine waishi maisha ya kimasikini na wengine waishi kama wafalme. Huu ni wakati wa kuinua maisha ya wananchi wa mikoa ya kusini wakati wana utajiri waliorithi kutoka kwa mababu zao. Serikali ichukue hatua za makusudi kuweka mitambo ya kufua gas kule Mtwara na kuachana na hii nadharia ya Kikwete kuwekeza kila kitu kule Bagamoyo. Huu ni ujinga uliokithiri wa kufikiria kwamba Bagamoyo ndio itakuwa centre ya maendeleo. Uwanja wa ndege Bagamoyo atakuwa anapanda ndege Jakaya peke yake oops na wana Bwagamoyo, Bandari Bagamoyo itakuwa inasafirisha mali za Jakaya peke yake au? Ahamishe makao makuu basi yaende Bagamoyo, Je Bagamoyo imechangia nini zaidi ya kutupatia JK ambaye akimaliza muda wake lazima ashitakiwe kwa sheria ya Uhujumu wa uchumi?

Sababu za yeye kushitakiwa zipo, nia ya kumshitaki ipo, uwezo wa kumshitaki upo .... ..... .... safi sana time will tell. Tuliwaona watawala wa Romania, Libya, Misri nk nk nk nk
 
Back
Top Bottom