Saini ya Pinda yaghushiwa bungeni; kunawaathiri zaidi wabunge wa upinzani, hasa wa Chadema

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Wednesday, 27 July 2011 21:32


Neville Meena na Habel Chidawali

VITUKO vya wabunge ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vimezidi kuongezekana; sasa baadhi ya wabunge wanadaiwa kugushi sahihi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa malengo ambayo bado hayajafahamika.

Kitendo cha kugushi sahihi ya Waziri Mkuu ndani ya ukumbi huo kunawaathiri zaidi wabunge wa upinzani, hasa wa Chadema ambao wamekuwa wakipelekewa ‘meseji’ za kuwadanganywa kuwa wanaitwa na Waziri Mkuu.

Juzi jioni kabla ya kikao cha Bunge kuahirishwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alialazimika kuomba mwongozo wa Mwenyekiti kukemea kitendo hicho alichokiita kuwa ni cha kihuni.

Lukuvi asimama mara tu baada ya Bunge kumaliza kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ambayo yalikuwa yalijadiliwa kwa siku mbili mfululizo.

“Naomba mwongozo wako kwamba, humu ndani imejitokeza tabia ambayo naona imezoeleka kidogo. “Kuna watu wanawaandikia wenzao meseji za kuwasumbua kwamba wanaitwa na mtu fulani halafu wanaweka sahihi na wakati mwingine haitokei,” alisema Lukuvi na kuongeza:

“ Nimeisikia hayo wiki iliyopita, lakini leo Mheshimiwa Joseph Selasini (Chadema) ameitwa kwa meseji inayodaiwa kuwa imesainiwa na Waziri Mkuu na hii nyingine ameitwa Mheshimiwa Leticia Nyerere (Chadema) kwamba anaitwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu wakazungumze maneno ya maana, lakini Waziri Mkuu hana habari na wamegushi sahihi yake,’’ alisema Lukuvi.

Waziri huyo wa Sera, Uratibu na Bunge alitaka mwongozo wa Mwenyekiti kama jambo hilo linaweza kufanywa na Wabunge, ndani ya Bunge kwa wabunge kugushi taarifa ambazo alisema nyingine na zinatisha.

Mwenyekiti wa Bunge George Simbachawene alikiri kuwepo kwa tabia hiyo ndani ya ukumbi wa bunge ambayo imekuwa ikifanywa na baadhi yao na kamba inaonekana kuota mizizi.

“Nakushukuru sana Mheshimiwa Waziri, ni kweli kuna mtu amefanya hivyo na karatasi aliyoiandika ipo hapa, Kwa kweli siyo nzuri haionyeshi kama tupo serious (makini) na kazi,” alisema Simbachawene na kuisoma:

“Amemwandikia hivi, Mheshimiwa Joseph Selasini Mbunge, samahani nakuomba mara moja tuje tujadili suala moja muhimu ambalo ningependa kujua kutoka kwako. Ahsante. Mizengo Peter Pinda na sahihi”.

Simbachawene alisema Selasini alipokwenda kwa Waziri Mkuu alishindwa kusaidiwa kwa kuwa wakati huo Waziri Mkuu alikuwa makini kusikiliza hotuba ya Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika katika majumuisho yake.

Hata hivyo, mwenyekiti huyo alisema uongozi wa Bunge utafanya kila liwezekanalo kubaini ni nani mwenye tabia hiyo na kwamba ili kukomesha vitendo hivyo
 
Du! Kweli mwaka huu tutasikia na kuona mengi! Hawa ndio watunga sheria wetu kwetu jamani? Sio ajabu nchi kulaaniwa, kumbe wawakilishi wetu wanafanya mzaha katika wakati ambao tunawategemea sana.
 
Watafutwe wataalam wa maandishi ili kubaini muhusika na akipatikana ashitakiwe kwa jinai
 
Ndio maan Jairo aliwaita 'comedians' hao mnaodai waheshimiwa,yaani nchi hii hovyo kabisa,bunge lilipokua la wana CCM wazee watupu tulishuhudia wakichapa usingizi leo bunge limejaa vijana tunashuhudia utoto na dharau kwa wananchi,Lord,whats wrong with thsi country???

Wednesday, 27 July 2011 21:32


Neville Meena na Habel Chidawali

VITUKO vya wabunge ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vimezidi kuongezekana; sasa baadhi ya wabunge wanadaiwa kugushi sahihi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa malengo ambayo bado hayajafahamika.

Kitendo cha kugushi sahihi ya Waziri Mkuu ndani ya ukumbi huo kunawaathiri zaidi wabunge wa upinzani, hasa wa Chadema ambao wamekuwa wakipelekewa ‘meseji' za kuwadanganywa kuwa wanaitwa na Waziri Mkuu.

Juzi jioni kabla ya kikao cha Bunge kuahirishwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alialazimika kuomba mwongozo wa Mwenyekiti kukemea kitendo hicho alichokiita kuwa ni cha kihuni.

Lukuvi asimama mara tu baada ya Bunge kumaliza kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ambayo yalikuwa yalijadiliwa kwa siku mbili mfululizo.

"Naomba mwongozo wako kwamba, humu ndani imejitokeza tabia ambayo naona imezoeleka kidogo. "Kuna watu wanawaandikia wenzao meseji za kuwasumbua kwamba wanaitwa na mtu fulani halafu wanaweka sahihi na wakati mwingine haitokei," alisema Lukuvi na kuongeza:

" Nimeisikia hayo wiki iliyopita, lakini leo Mheshimiwa Joseph Selasini (Chadema) ameitwa kwa meseji inayodaiwa kuwa imesainiwa na Waziri Mkuu na hii nyingine ameitwa Mheshimiwa Leticia Nyerere (Chadema) kwamba anaitwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu wakazungumze maneno ya maana, lakini Waziri Mkuu hana habari na wamegushi sahihi yake,'' alisema Lukuvi.

Waziri huyo wa Sera, Uratibu na Bunge alitaka mwongozo wa Mwenyekiti kama jambo hilo linaweza kufanywa na Wabunge, ndani ya Bunge kwa wabunge kugushi taarifa ambazo alisema nyingine na zinatisha.

Mwenyekiti wa Bunge George Simbachawene alikiri kuwepo kwa tabia hiyo ndani ya ukumbi wa bunge ambayo imekuwa ikifanywa na baadhi yao na kamba inaonekana kuota mizizi.

"Nakushukuru sana Mheshimiwa Waziri, ni kweli kuna mtu amefanya hivyo na karatasi aliyoiandika ipo hapa, Kwa kweli siyo nzuri haionyeshi kama tupo serious (makini) na kazi," alisema Simbachawene na kuisoma:

"Amemwandikia hivi, Mheshimiwa Joseph Selasini Mbunge, samahani nakuomba mara moja tuje tujadili suala moja muhimu ambalo ningependa kujua kutoka kwako. Ahsante. Mizengo Peter Pinda na sahihi".

Simbachawene alisema Selasini alipokwenda kwa Waziri Mkuu alishindwa kusaidiwa kwa kuwa wakati huo Waziri Mkuu alikuwa makini kusikiliza hotuba ya Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika katika majumuisho yake.

Hata hivyo, mwenyekiti huyo alisema uongozi wa Bunge utafanya kila liwezekanalo kubaini ni nani mwenye tabia hiyo na kwamba ili kukomesha vitendo hivyo

 
Hii inachangiwa na idadi kubwa ya wabunge ndani ya bunge, dawa ni kupunguza wabunge na sanasana wa viti maalumu ambao mimi naona wengi wao ni wanafki tuu. Viti maalumu sanasana wa magamba nadhani kazi yao kubwa ni kuitiki ndiyooo na kupigia makofi pumba za magamba yao yanapoongea.
 
Senema nyingine ya Magamba! Kwa maoni yangu wabunge wa CCM wanahusika, na kila wanachofanya mle ndani ni kwa maagizo ya Chama chao. Hapo si bure kwa jambo kama hilo, haiwezekani Mbunge mmoja mmoja aamue kufanya jambo kama hilo, binafsi siamini. Na kuamini haya nisemayo tungoje sarakasi ya uchunguzi na kituko cha matokeo ya uchunguzi. Hakuna majibu ya kueleweka ng'o!
 
Ni kitendo cha aibu kwa mfumo [System] kukubali Watunga Sheria kuwa ni watu wa kudanganya [Magumashi] na kwa mwenendo huo hatima ya Watanzania kwa matendo hayo ya kiovu ni hatari kwa Usalama wa Taifa.

Umajua inauma sana kuona kuwa wahusika wa matendo hayo ya kiuni,ambayo yanatendwa na sana na vijana na wajanja wa mijini wanapenda kujiita watoto wa mijini leo hiii yako ndani ya Bunge ni AIBU KUBWA SANA KWA TAIFA.

Athari za kughushi saini ya Kiongozi Mkuu kama Pinda ni Kulitia Taifa katika KITANZI CHA MATATIZO.Tendo hilo tena lianatendwa ndani ya BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO ambako ndio sehemu kuu ya UTUNGAJI WA SHERIA ZA HAKI KWA UMMA.Leo hii kwa tendo hilo KWELI NCHI HII IKO TAYARI REHANI na dalali wake anabagain na wateja tofautitofauti.

Inauma sana pale viongozi watu wazima [miaka 55-kuendela] wanapochezea maisha ya Watanzania,wanapoyafanya Maisha yetu kama tamthiria za kituo cha Television cha ITV.Wakiona mijadala Wananchi makini wanayofanya na watu ambao wako serious wao useme UZUSHI, UCHOKONOZI,UCHONGANISHI DHIDI YA WANANCHI.Polepole Taifa linaingia kwenye mongonyoko la Maadili na tayari Mioyo ya Watanzania inaanza kuwa sugu.Usugu huo kimatendo na Mawazo inaaamia BUNGENI na kisha mioyo hiyo inaludi kwa UMMA,ambako kwa kujifunza Watanzania wanaona na kubebe dhana ya kuwa kumbe udanganyifu ni sehemu ya maisha yetu HATA BUNGE WATU WANADANGANYA KWA VIMEMO.

Mchezo huo ni BOMU hatari kwa vizazi vijavyo haswa Watoto walioko Mashuleni, Shule za Msingi,Sekondari na Kaka na Dada zao vyuoni,wote hao watayaona na kuhalalisha matendo hayo kama ni kitu sahihi.Kwa kuwa waliona BABU zao Bungeni wakifanya na kuwa huo ni mfumo halali kama ilivyo mifumo mingine kama ROBBING ya kusaidia budget ya WIZARA ipite.

Kama kuna sehemu USALAMA WA TAIFA WANAPASWA KUFANYA KAZI USIKU NA MCHANA KUWAPATA WAUNDA VIMEMO VYENYE SAINI YA KUGHUSHI HAPO BUNGENI.Kwa kuwa kughushi huko kwenye eneo hili muhimu kwa maisha ya Watanzania ni kuliweka rehani TAIFA na Watu wake.

Kuna wakati uwa naumia sana nikiona wasanii [Watoto wa Mijini maalufu kwa kughushi na kuwaumiza/kuwatapeli Wafanyabishara na Wanasiasa na ofisi za Serikali] maalufu kwa kughushi wanavyosifiwa kwenye majiji na miji yetu kupitia vyombo vya habari na nyimbo za muziki kama kuwa ni watu bora sana kwenye jamii huku jamiii na wanaohusika kujua matendo hayo wakikaa kimywa. Huwa napata shida sana hivi kwa kuwaendekeza na kuwalea Watu hawa mbona madhala ni makubwa kuliko faida ya watu hawa kuwepo kwao kwa umma.Isharrah Mungu kasikia magumashi hayo YAMEINGIA BUNGENI NAYO YAMEKUWA NI SEHEMU YA BUNGE.

Tutashindwaje kuaminisha kuwa RAIS NA WAZIRI MKUU saini zao zimegushiwa na kutumika KUUZA MALI ASILI ZETU AU MADINI YETU,au zimetumika kumshawishi WAZIRI AU MBUNGE kutenda jambo lenye MASLAHI YA TAIFA kwa favour ya KUTII AMRI AU OMBI LA WAZIRI MKUU AMA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO.

Kuna wakati niliambiwa msanii mmoja alipiga magumashi saini ya kigogo wa kampuni maalufu, Bosi mzee alipopewa saini ile akaulizwa ili kuitambua kama ni saini yake siunajua mtu chake.Mzee akakubali bila kusita kuwa absolute yaaaah this is Mine.Wakamwambia Mzee hii sio saini yako ujasaini wewe imesaini na mtu mwingine Mzee kichwa kikauma akakili this is BONGO.

WANAUSALAMA HAYO SASA YAMETINGA HUKO NDANI WANANCHI WATEGEMEE NINI?KWA KUWA HUKU MITAANI MAMBO HAYO WATANZANIA WALISHAZOEA.WAO HUKU WANAITA MAGUMASHI,AU KWA LUGHA NYINGINE MWANAMUZIKI WA KIZAZI KIPYA PROFESSOR J ALIPATA KUSEMA AKILI MU KICHWA.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Hao si wengine ni wabunge wa chama cha magamba tu.Wao wako kwa ajili ya kutafuta mshiko kwa akina Jairo na maslahi ya chama chao cha kifisadi.Si unaona ile kamati ya Mrema inakaribia kufa baada ya kuumbuliwa wanaomba na kupokea mlungula ili kuficha maovu ya Halmashauri zetu.Haya magambaaaaaaaaaaaaaaa hayafai kabisa.Sasa yameanza kufoji hata sahihi ya Mtoto wa mkulima na kuwakejeli wapinzani ambao wanaonekana kuleta changamoto ndani ya bunge.Bila kukimwaga chama hiki cha magamba nchi hii basi tena.
 
hao wabunge wa ccm wamekosa kazi sasa wameanza kufoji saini ya boss wao
kila kitu wao ni makofi tuu wanapiga na kushinda kunywa pombe ikipigwa kengele
yakwenda kupiga kura mbio yaani awajui nini wanachokipigia kura baada ya ndiyooooooo

hawo wanarudii kunywa hayo nimeyashudiia bungeni na kushangaaa sana

kikupacho raha na uchungu kitakupa
 
Magamba yaliweza kuchakachua masanduku ya kura yashindwe kuchakachua saini ya magamba mwenzao...

Pinda lia tena kama ulivyowalilia albino...

Jamaa huwa hawana cha kufanya mule ndani ndio maana wanatumia dk 10 kusifiana tu, wanaingia bungeni kwa ajili ya kusaini mahudhurio wachukue 70,000 wasepe. Ndio maana watakuua ukiongelea kuhusu posho. Haya watetezi wa posho mliopo humu jamvini mtaiweka wapi hii aibu ya magamba wenzenu
 
kuna vitu vingi muhimu vya kujadili lakini wamekuwa kama watoto wa chekechea...kwa kweli bunge livunjwe hakuna lolote linalofanyika huko zaidi ya vituko na matukio
 
Tatizo ni kuwa Wabunge Wetu Wengi ni Mzaha wanasubiri his 10% za mikataba na bajeti; Unadhani kupewa asante zimeanza wakati wa hiyo Bajeti ya Wizara ya Nishati?

Tangu lini Mmeona Kampuni kama VODACOM kwenda Dodoma kuwafanyia party Wabunge wakiwa kwenye Vikao Vyao; Bajeti ya Wizara ambayo VODACOM inaripoti bado haijatoa Bajeti yake... Nani amepata 10%? hakuna kitu kama hicho kwenye Mabunge Mengine Duniani.

Angalia kuna BENKI MOJA pia imeenda kucheza michezo na wabunge; rather than wabunge wao kwa wao... Shame on this GVT
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Majibu ya Mwenyekiti wa Kikao Mh Simbachawane ni fedheha. Kugushi sign kosa (criminal offense), lakini kwa watu waliopewa dhamana ya kutunga sheria kuvunja sheria ni janga la kitaifa na nilitegemea uchunguzi ufanyike haraka. Nani anaweza kusema kuwa wagushi sign bungeni hawafanyi hivyo huku uraiani?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom