Saif Gaddaffi auwawa katika shambulizi la NATO

Me si kwamba nimeumizwa na yeye tu eti kwa kuwa ameuawa. Muda wote sipendi mauaji yoyote. I always say no to war!
 
Namkubali sana mzee wa GREEN BOOK.nimesikitishwa sana na hayo mauaji.
Natamani nikamate lizungu limoja nimlipizie kisasi.
 
Nyie wote mnaolalamika leteni ushahidi kwamba ni kweli ati Saif-al Arab na wajukuu watatu wa Gaddafi wameuwawa. Kwanza Saif hana watoto, na hawasemi hao wajukuu ni watoto wa mtoto gani wa Gaddafi.

Mpaka sasa hamna ushahidi wowote uliotolewa zaidi ya tamko la msemaji Moussa Ibrahim. Hiyo video ambayo Libya TV wameitoa maiti zenyewe zote zimefunikwa, sasa tutadhibitisha kivipi?

Mambo ya Balali hayo, na nyie munaingia mukichwa. Tena kiulaini! Tafakarini kabla ya kukurupuka.

Hebu angalieni huu "ushahidi"

Last edited by a moderator:
Me si kwamba nimeumizwa na yeye tu eti kwa kuwa ameuawa. Muda wote sipendi mauaji yoyote. I always say no to war!
Ni kweli mkuu, siku zote giza halifukuzi giza ila mwanga ndo huondoa giza, Hata kama Ghadafi kauwa suluhisho sio kuua wanae au kumuua yeye, wamarekani wataifanya Libya kuwa Afghanistan ya Africa, maana wakishamwondoa Ghadaf watataka wachimbe mafuta na baadhi ya walibya wataweka ngumu, hapo ndo watakapoanza kuchinjana na maisha yatakuwa magumu hadi watamkumbuka wanayemwita dikteta sahivi.
 
Hata kama Gaddafi ni mbaya na muuaji kiasi gani hukumu yake sio kuuwa watoto wake ambao hawana hatia.

Hata kama Gaddafi ni mbaya kiasi gani anapaswa kufikishwa mbele ya sheria , nani dunia hii ameua watu wengi kama George Bush? mbona hawakumvamia ?

Africa wanapaswa kuwa pamoja kwenye hili, kwani huu ni uonevu .

Hivi Gaddafi kapona? mbona hawajasema zaidi ya jana kusema kuwa alikuwa kwenye nyumba hiyo na mpaka sasa haijaelezwa kama yupo hai au naye alikufa na kama hakufa lazima atakuwa aliumia anatibiwa wapi?

Kwasababu ni mwafrika eti tukimbilie kumtetea Gaddafi! Siku zote huu ndiyo ujinga wetu mkubwa waafrika, mtu anafanya madudu alafu eti atetewe na waafrika kwa vile tu ni mwenzao!

Mbona hamkuita waafrika kumzuia Gaddafi wakati anaua watu wake bila huruma? Huyu mtoto wa Gaddafi roho yake ni muhimu kuliko roho za walibya wengine waliouwawa na Gaddafi?

Kama kumtetea Gaddafi inabidi iwe ni kwa sababu ya matendo yake na si kwasababu eti ni Mwafrika! Kama matendo yake ni sahihi atatetewa si na waafrika tu bali na wana-waulimwengu wote.

Kwa sababu hii, ndiyo maana AU inadharauliwa kwa kutetea maovu ya viongozi wa Afrika!

Mwisho:

Mungu apumzishe roho zote za Walibya waliouawa bila hatia mahala pema peponi. Amen
 
Mara baada ya taarika kusema kuwa mtoto wa Gadafi ameuwawa na Nato,wengi wetu wamefurahi
Binafsi nayalaani kama ambavyo nililaani uvamizi wa kihuni,kwa yeyote anayeitakia mema Africa hawezi kushabikia uvamizi na mauaji haya ya mtoto wa Ghadafi na raia wa Libya,kimsingi Nchi za magharibi hazina mapenzi ya kweli na Africa,wanachotaka ni mafuta ya Libya na rasilimali nyingine,kama Ghadafi angeondolewa na nguvu ya umma basi nisingekuwa na neno,hili la kuruhusu uvamizi,na kuuwawa kwa nchi huru kamwe sitalikubali.Historia itatuhukumu

Nalazimika kuamini kuwa ulilaani hata mauji ya raia wa Libya yaliyofanywa na vikosi vya Gadafi wakati wa maandamano ya amani!
 
Akili yako inaona upande mmoja wa shilingi. Kwa hiyo waliouliwa na Ghadafi hawana thamani. Maandamano yalizuiwa kwa risasi. Ina maana wewe una akili kuhusu Walibya?
 
...Kama kumtetea Gaddafi inabidi iwe ni kwa sababu ya matendo yake na si kwasababu eti ni Mwafrika! Kama matendo yake ni sahihi atatetewa si na waafrika tu bali na wana-waulimwengu wote.
Kwanza hata huyo mtoto wa Gaddafi anaitwa Saif al-Arab siyo Saif al-Africa.

Saif=sword, al=of, Arab (Sword of Arab), lakini bado tu watu oh waafrica, oh sijui nini, ati ilikuwaje...! Tuacheni kasumba ya kutetea kila kitu cha kiafrica, hata kama ni kibaya. Mkuki kwa nguruwe... au siyo?
 
Hongera sana NATO kwa kutetea haki za wanyonge wasio na wasaidizi, Kill 'em ALL.
 
Duh! yaaani wewe ndio unamjua Ghadafi vizuri sio,au chuki inayotokana na stori zenu za katika vijiwe vya kahawa ndio inayokusumbua?Na hakika hata wewe umjui ghadafi.

anaweza kuwa hamjui gaddafi,na we haumjui id amini dada aliyeua watz wa bukoba. Kagemro atakuwa anatokea kagera hasa mtukula ambapo jambaz id amini akifanya ukatili kwa nguvu za gadaf kuua wahaya wetu. Gadaf ni jitu la kuigwa na ma alqaida pekee na uzao wake umelaaniwa!
 
hivi hao waliouliwa na gadafi kwa maelfu si watu au hawana wazazi unaniogopesha Nanyaro hasa ukiwa ni kiongozi ambaye umri wako ni mdogo nilitaraji fikra zako zitakuwa za kidemokrasia zaidi lkn umenisikitisha kumbe kwako kufa kwa mtoto wa raia ni poa ila mtoto wa mtawala hapana . Tz imelaaniwa kijana kama wewe kuwa na mawazo mgando kiasi hiki huku ukiwa kiongozi ni hatari sana waliokuchagua wana hasara
 
Naona watanzania tumeamua kushabikia tu, Toka lini NATO wakawa watetezi wa wanyonge, acha tuonyeshane ujuzi wa kutype tu humu jamiiforums, lakini ukweli NATO wanajua walichokifuata Libya na itadhihirika baada ya kumwondoa Ghadafi ingawa wengi mnajifanya hamuelewi.

Chukua mfano wa Ivory coast watu wangapi wamekufa mbona NATO hawakwenda, Sudan wamekufa wangapi umesikia NATO wako kule, hata Somalia hadi leo haitawaliki watu wanakufa huwezi sikia NATO wameenda.

Watu wengi humu jamvini wanaolaani mauaji ya huyo dogo hawasemi kwamba Ghadafi anapoua ni sawa no, kuua ni kuua iwe Ghadaf kaua au mwanae ameuawa siyo sawa, siku zote haki haitafutwi kwa kuvunja haki nyingine, kama tunaona alichofanya Ghadaf sio sawa kwa nini kitu hicho hicho kikifanywa na NATO kiwe sawa?
 
jaman naye ni mwanadamu kila mtu ana haki ya kumsikitikia tenaa na watoto wake na mke qake jaman inauma kwa sababu yule dogo alikuwa hana makuu wangekuwa ni wale wawili wajinga sana waliotoa amri waandamaji wapige mabomu ningeona kawaida
 
Napongeza sana NATO!

mwl nyerere aliwakamata wavamizi majeshi ya gadafi mwaka 1979 huko kagera na kuwapakia wanajeshi wa libya kwenye dege lake na kuwashusha mpakani mwa Libya kisha kamwambia gadaf kuwa wale watiifu wako uliowaleta kwa nduli id amin ili watupige watanzania,nimewarejesha kwako salama! Na wakat huo majeshi ya tanzania yalivuka mpaka, wa tz,yakafika kwenye kijijini Arua, alikozaliwa amin ,yakamtoa nduli ikulu,nduli alitoroka kwa dege kwa msaada wa gadaf na alipoomba kurud uganda Obote alimwambia,ukija hai tutakunyonga,ukija maiti utakuwa na ruhusa ya kuzikwa tu! Binafsi,nkikumbuka alivokuwa ananyonga wazee na vilema na kuwatupa mto kagera kisha maji kugeuka rangi ya damu na maiti kuelea kama samaki mtoni kagera! Nduli amin aliishi na kufia libya kwa gharama za aliyemtuma kuishambulia Tz ,gadaf. Gadaf is a living cursed man whose spirit and offsprings are to be defended by the power of the Devils. Like the father like the sons of cursed gadaf!
 
Naona watanzania tumeamua kushabikia tu, Toka lini NATO wakawa watetezi wa wanyonge, acha tuonyeshane ujuzi wa kutype tu humu jamiiforums, lakini ukweli NATO wanajua walichokifuata Libya na itadhihirika baada ya kumwondoa Ghadafi ingawa wengi mnajifanya hamuelewi.

Chukua mfano wa Ivory coast watu wangapi wamekufa mbona NATO hawakwenda, Sudan wamekufa wangapi umesikia NATO wako kule, hata Somalia hadi leo haitawaliki watu wanakufa huwezi sikia NATO wameenda.

Watu wengi humu jamvini wanaolaani mauaji ya huyo dogo hawasemi kwamba Ghadafi anapoua ni sawa no, kuua ni kuua iwe Ghadaf kaua au mwanae ameuawa siyo sawa, siku zote haki haitafutwi kwa kuvunja haki nyingine, kama tunaona alichofanya Ghadaf sio sawa kwa nini kitu hicho hicho kikifanywa na NATO kiwe sawa?
Hivi mwezi uliopita wakati Gadaffi anauwa watoto wa wenzake ulikuwa hujajiunga JF je ulianzisha thread au topic yeyote kulaani mauaji hayo kwani wale watoto walikuwa hawana wazazi acheni unafiki wenu. Nafikiri haumjui Gadaffi tuulize tuliokwenda Mtukula miaka ya 70 kupigana na waarabu wa Libya wakitaka kuchukua ardhi yetu.
 
Mara baada ya taarika kusema kuwa mtoto wa Gadafi ameuwawa na Nato,wengi wetu wamefurahi
Binafsi nayalaani kama ambavyo nililaani uvamizi wa kihuni,kwa yeyote anayeitakia mema Africa hawezi kushabikia uvamizi na mauaji haya ya mtoto wa Ghadafi na raia wa Libya,kimsingi Nchi za magharibi hazina mapenzi ya kweli na Africa,wanachotaka ni mafuta ya Libya na rasilimali nyingine,kama Ghadafi angeondolewa na nguvu ya umma basi nisingekuwa na neno,hili la kuruhusu uvamizi,na kuuwawa kwa nchi huru kamwe sitalikubali.Historia itatuhukumu

Sawa tumekusikia.
 
Hivi mwezi uliopita wakati Gadaffi anauwa watoto wa wenzake ulikuwa hujajiunga JF je ulianzisha thread au topic yeyote kulaani mauaji hayo kwani wale watoto walikuwa hawana wazazi acheni unafiki wenu. Nafikiri haumjui Gadaffi tuulize tuliokwenda Mtukula miaka ya 70 kupigana na waarabu wa Libya wakitaka kuchukua ardhi yetu.

Nami namshangaa tena sana.
 
Back
Top Bottom