Saidia kutatua ubishi huu tafadhali!

Mrimi

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
1,691
633
Kuna ubishi uanendelea hapa mtaani, inavyoelekea hakuna hitimisho litakalofikiwa.
So, wakuu naomba mnisaidie kujua japo kwa faida yangu.

Issue yenyewe ni hivi:

Iwapo bunge kwa kauli moja limepitisha mswada fulani (let's say kama ule wa juzi juzi), ukafika kwa rais ili ausaini kuwa sheria, lakini rais pengine kwa sababu anazoona zinafaa akakata kusaini ule mswada. Je, madhara yake ni yapi?

Sasa, kuna wanaosema rais atalivunja bunge kwa kuwa tayari kuna kupishana kwa hii mihimili miwili, yaani bunge na serikali.

Kuna wanaosema rais ataurudisha bungeni ukajadiliwe tena. Na kwamba ataambatanisha mapendekezo yake, na sababu za msingi zilizomfanya asiusaini. Swali, kama bunge litashikilia msimamo wake na kuupitisha tena bila kufanya marekebisho, itakuwaje?

Naamini kuna watalamu wa mambo haya wanapita humu, tafadhali naomba tafsiri ya hili jambo.
 
nyongeza,kuna ule msuada wa makampuni ya simu za mikononi kuwa registered DSE mpaka leo umekwama kwa rais sijui anamuogopa RA na vodacom yake au?
 
Kadiri ya ufahamu wangu, muswada ambao rais amekataa kutia saini utarudishwa bungeni kujadiliwa tena ukiwa na mapendekezo ya rais(rejea zengwe la ubinafsishaji wa NMB). Rais atavunja bunge, ikiwamo na yeye mwenyewe kujivunja endapo atashindwa kusaini muswada kwa mara ya tatu.
Bunge linaweza likaghairi kurudisha kwa rais mswada aliokataa kuusaini kama kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo!
Sawasawa?
 
sawa sawa
 
Back
Top Bottom