Said Mwema - Kuwa shemeji ya Rais ni leseni?

Utendaji wa serikali hii ukifuatilia sana alafu ukarudi nyumbani ukakuta na familia nayo magumashi kama serikali yao, unaweza kufa kabisa kwa mawazo
 
Sijui mpaka lini na kwanini...
Sijui kwanini CDM hadi leo hii hawajaanzisha maandamano ya kumshinikiza Mwema aondoke au aondolewe; hata Bungeni hakunyoshewa kidole yeye mwenyewe na kutaka aondoke.. sijui mpaka nani wa CDM auawe ndio watajua kuwa Mwema na Chagonja ni hatari kwa demokrasia!!! Kutokana na rekodi zao wenyewe inaonekana wamejifanya kuwa ni maadui wa kudumu wa haki za kiraia na haki za binadamu. Wazo kuwa wananchi wana haki ya kuandamana kuipinga serikali yao au uongozi wa walio madarakani halijawaingia kabisa kichwani! Wako kama maafisa wa kizungu wa wakati wa mkoloni ambao walijaribu kuzima maandamano yaliyoongozwa na Mwalimu Nyerere au wale waliowafunga kina Makange! Hawana tofauti!
Kilio cha mtanzania akiingii kabisa masikioni mwa polisi wetu. Wanatoka kuwaua, kuwatesa, na kuwanyanyasa raia bila sababu. Sijui siku raia watakapowageukia kama DHAIFU atakuwepo kuwatetea?
Huyu Mwema anachunga tumbo yake na basi. Kama angekuwa kiongozi jeshi zima lisingalinuka kiasi hiki. Angechukua hatua za haraka yaani hata zile za msingi tu. Wewe ni kiongozi unamtuma Kova akatangaze upuuzi, uwongo, na ujinga kwenye vyombo vya habari? Wewe ni kiongozi unatuma polisi wakawalipue watanzania wanaoenda kwenye mkutano kutetea haki zao? Wewe ni kiongozi unatangaza kuwa mko tayari kumlinda raia alliyeponea chupuchupu mikononi mwa polisi? Hayupo anachokifanya huyu Mwema na jeshi lake. Wanajenga chuki, hasira, na woga kwa wananchi. Wanasahau kuwa: "Asiyefunzwa na mamaye hufunza na ulimwengu." Siku ya mwema na polisi kwa ujumla inakuja. Hizo hongo zinamchanganya akili hadi hawajui polisi ana wajibu gani katika kulinda raia na mali zao. Damu hii inayotumwagikia kila siku kupitia mikono ya polisi inalichafua taifa letu.
 
Nikikumbuka msemo maarufu wa mchungaji Martin Niemöller (1892–1984) usemao “First they came…” naona watanzania tumelala!... Mchungaji martin alisema: ...............First they came for the communists, ............and I didn't speak out because I wasn't a communist. .............Then they came for the Jews, ..........and I didn't speak out because I wasn't a Jews. ...........Then they came for the trade unionists, ................and I didn't speak out because I wasn't a trade unionist. .............Then they came for me, ...........and there was no one left to speak for me. ....................................... Sasa maneno haya yanatimia kwetu!!!!
 
Sijui mpaka lini na kwanini...
Sijui kwanini CDM hadi leo hii hawajaanzisha maandamano ya kumshinikiza Mwema aondoke au aondolewe; hata Bungeni hakunyoshewa kidole yeye mwenyewe na kutaka aondoke.. sijui mpaka nani wa CDM auawe ndio watajua kuwa Mwema na Chagonja ni hatari kwa demokrasia!!! Kutokana na rekodi zao wenyewe inaonekana wamejifanya kuwa ni maadui wa kudumu wa haki za kiraia na haki za binadamu. Wazo kuwa wananchi wana haki ya kuandamana kuipinga serikali yao au uongozi wa walio madarakani halijawaingia kabisa kichwani! Wako kama maafisa wa kizungu wa wakati wa mkoloni ambao walijaribu kuzima maandamano yaliyoongozwa na Mwalimu Nyerere au wale waliowafunga kina Makange! Hawana tofauti!

nchi hii ya tz kwa miaka hii inatawaliwa kwa mtaji wa chini....na ndio maana maswala ya nepotism hatayataisha tz.....ukifatilia sana kwa karibu utagundua watawala wa nchi hii wameiweka rehani nchi hii kwa mtaji wa pumbu(chini)....ndio maana mambo yanafanyika ya hovyo hovyo na hamna wa kumwadhibu mwenzake....maana utamwadhibu vipi mtu anaekupa utamu???????.....long way to go tz......very bad indeed.....
 
Kuwa familia moja sio kosa na wala sidhani kama watu wana-object hilo, tatizo linakuja kwenye uwajibikaji na kama undugu/ukaribu unaonekana kuwa kinga dhidi ya maovu. Ni hivi majuzi rais wa Liberia amemsimamisha mwanae kazi. Can we do that here?

we can't !
 
Huyu Paul Chagonja anaonekana Mungu mtu vile. Check wanavyomcheka mama wa watu......

Mama kawapa heshima na wao wanamcheka. Kuna siku na wao watapiga magoti.....

DSC_0202.JPG


Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Said Mwema, amewatoa machozi wananchi kufuatia ujumbe wake mfupi wa maneno kwa njia ya simu (SMS) iliyokuwa ikilalamikia kitendo cha baadhi ya wanakijiji wa Mwakashahala kumuua polisi Joseph Milinga aliyewakamata wakiwa na bangi.

IGP Mwema alikuwa akiwalalamikia watu hao kwa vile kitendo alichokuwa akikifanya marehemu kilikuwa cha kuzuia mihadarati hiyo isisambae na kuharibu watoto au kizazi kijacho.

Aidha, katika meseji hiyo iliyonaswa na Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita, pia Mwema alionesha kukerwa na tabia iliyoota mizizi ya watu kujichukulia sheria mikononi. Akahoji, wako wapi watu wema?

Maelezo kamili ya meseji hiyo yanasomeka kama ifuatavyo:
Salam, nakutakia heri ya Pasaka. Pia naomba tafakari mob justice (kujichukulia sheria mikononi) ni adui wa human rights rule of law,(sheria za haki za binadamu).
Good governance (Utawala bora) iwe kwa raia au askari aliyeuawa Tbr (Tabora) ambaye niko njiani kwenda Rukwa kumzika.

Na iwe sababu yoyote, hata Mungu hampendi anayetoa kikatili roho ya mtu mwingine na hasa anapotaka kukamata bangi ili isidhuru watoto wetu na watu wengine.

Where are the good people? (Wako wapi watu wema?) Lets join hands and have ant mob justice campaign in this country for common good.
(Tushikamane kupinga wanaojichukulia sheria mikononi katika nchi kwa ajili ya ustawi).
Baadhi ya watu waliokutwa wakiisoma meseji hii walionesha kusikitishwa sana na tabia ya watu kujitwalia sheria mikononi wakati vyombo vya sheria vipo na wengine walishindwa kujizuia kutokwa machozi.

Afande Milinga, aliuawa na wananchi waliojiita wenye hasira kali wakati akitimiza wajibu wake wa kazi akiwa katika zoezi la kusaka watu wanaolima na kuuza Bangi.
Tukio hilo lilitokea Aprili 20, mwaka huu katika kijiji cha Mwakashahala, kata ya Puge, wilayani Nzega, Mkoa wa Tabora.

Wananchi hao walimshambulia marehemu kwa silaha mbalimbali za jadi mpaka kifo chake.
Mbali na marehemu, afande mwingine aliyekuwa naye alijeruhiwa vibaya na kulazwa hospitali ya Mkoa wa Tabora.

Mbali na tukio hilo, vitendo vya raia kuua askari katika kijiji hicho hii ni mara ya pili.
Marehemu Milinga alizikwa katika kijiji cha Kisiwa cha Manda Karenge, kata ya Kirambo, wilayani Nkasi, Mkoa wa Rukwa, ameacha mke na watoto wanne.

Wakati huo huo, IGP Mwema amewataka wananchi wa Kijiji cha Mwakashahala waliokimbia makazi yao wakihofia kukamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za mauaji, warudi na kuungana na familia zao kwani watuhumiwa wameshakamatwa na wanahojiwa na jeshi lake.

Akiongea katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo Jumamosi iliyopita, Kamanda Mwema alisema hakuna haja ya mtu kukimbia kama hakuua, kwa sababu jeshi lake halimkamati kila mtu.

Katika kipindi hiki cha uongozi wake, IGP Mwema amefanikiwa kuifanya jamii iliamini jeshi la polisi tofauti na miaka ya nyuma.

Aidha, hali ya utulivu imeongezeka, sanjari na kupungua kwa ujambazi ambao zamani ulikuwa ukitikisa nchi.
 
Hapo umechemka unawezaje kumfananisha Wema na Adolf Hitler? Hitler alikuwa genius! Huyu Wema si takataka tu, watu wakiamua kesho anatoka mara moja!

Kijakazi unamaanisha wema sepetu au ulikuwa unamaanisha said Mwema?punguza Jazba
 
Ajabu ni kuwa haohao Polisi kila siku wanasisitiza ushirikiano na raia kwa kauli yao ya Polisi jamii ili wananchi wawape ushirikiano ili kufanikisha kazi zao. Kisha wanawaua na hakuna anayewajibika au kuwajibishwa. Nchi inatumbukia shimoni nasi tunaangalia tukiwa kimya.
 
Kuwa familia moja sio kosa na wala sidhani kama watu wana-object hilo, tatizo linakuja kwenye uwajibikaji na kama undugu/ukaribu unaonekana kuwa kinga dhidi ya maovu. Ni hivi majuzi rais wa Liberia amemsimamisha mwanae kazi. Can we do that here?
Unamaanisha shemeji yake amfukuze shemeji yake..!? Kama unashindwa kumfukuza rafiki pamoja na maufisadi yote yale ataweza kumtimua kazi shemeji?
 
Nikikumbuka msemo maarufu wa mchungaji Martin Niemöller (1892–1984) usemao "First they came…" naona watanzania tumelala!... Mchungaji martin alisema: ...............First they came for the communists, ............and I didn't speak out because I wasn't a communist. .............Then they came for the Jews, ..........and I didn't speak out because I wasn't a Jews. ...........Then they came for the trade unionists, ................and I didn't speak out because I wasn't a trade unionist. .............Then they came for me, ...........and there was no one left to speak for me. ....................................... Sasa maneno haya yanatimia kwetu!!!!

The only thing necessary for the triumph of evil is for good men to do nothing - Edmund Burke
 
Ocampo wa iv anawasubiri tu,pls kna marcus,Bi Simba na mama nkya ni wakati sasa wa kuyapeleka haya Amnest International kwenda kuwaadabisha!
 
Sijui mpaka lini na kwanini...
Sijui kwanini CDM hadi leo hii hawajaanzisha maandamano ya kumshinikiza Mwema aondoke au aondolewe; hata Bungeni hakunyoshewa kidole yeye mwenyewe na kutaka aondoke.. sijui mpaka nani wa CDM auawe ndio watajua kuwa Mwema na Chagonja ni hatari kwa demokrasia!!! Kutokana na rekodi zao wenyewe inaonekana wamejifanya kuwa ni maadui wa kudumu wa haki za kiraia na haki za binadamu. Wazo kuwa wananchi wana haki ya kuandamana kuipinga serikali yao au uongozi wa walio madarakani halijawaingia kabisa kichwani! Wako kama maafisa wa kizungu wa wakati wa mkoloni ambao walijaribu kuzima maandamano yaliyoongozwa na Mwalimu Nyerere au wale waliowafunga kina Makange! Hawana tofauti!

Nasikia una usongo wa kila mwenye cheo Serikalini kwani ulikuwa na hamu ya kurithi kazi ya baba'ko na umpite kwa cheo kwani yeye aliishia u rpc tu lakini kimo ndio kikawa tatizo kwako na ukashindwa kukubalika jeshini na uraiani ukaamuwa kuzamia USA na kuishi mafichoni. Pole sana na ahsante aliyegunduwa intaneti, angalau unaweza kujificha nyuma ya pazia na ukasambaza ***** bila ya kujulikana ni nani.

Sitaki kuamini kuwa ni kile kisa cha Tanga!
 
Mwema aliingia na focus kubwa kwelikweli ya kufanya/tenda kazi kwa haki sambamba na kuboresha jeshi lenyewe lkn madudu ya wanasiasa waliomteua yamembadili kabisa
Hapo naomba nipingane na wewe, toka mwema ameingia jeshi la polisi limekuwa la hovyo haijapata kutokea. Rushwa inachukuliwa njenje, mtu ukiibIwa huwezi kufikiria kwenda polisi kwani ni kupoteza hela bure. Utendaji wa polisi umekuwa kama wa waganga wa kienyeji baada ya Mwema kuingia na sasa anataka akumbukwe kwa mauaji ya raia
 
kila zama na kitabu chake. kitabu cha zama hizi kimejaa upendeleo, urafiki, undugu na kufahamiana.
 
Back
Top Bottom