Said Mtanda vs Dr. Hamis Kigwangalla

Leo Bunge la Jmahuri ya Muungano kwa sauti ya kishindo limempitisha mwanadiplomasia mbunge wa jimbo la Mchinga mhemishimiwa Said Mtanda kuwa mbunge wa Bunge la Afrika.

Mheshimiwa Mtanda baada ya kupata ushindi huo alikuwa na machache tu ya kusema "Nitawawakilisha vema kwenye bunge la Afrika"

Kinyume na maneno hayo machache ya mwanadiplomasia Mtanda, ambaye inaaminika kuwa busara zake na uzoefu wa taaluma ya diplomasia ndivyo vilivyomuwezesha kuwashawishi wabunge wenzake wamchague kwa kishindo, mgombea aliyeangushwa, mhe. Hamis Kigwangwallah, alikuwa na mengi ya kuongea.

"Siwezi jaribu tena! I will never try the impossible! This time I was checking out and have received the response! Sipendwi na wenzangu...I thought wamenisamehe kwa kosa la kusema ukweli na kuwa na misimamo mikali kwenye issues...
clear.cache.gif

kukata tamaa is not in my vocabulary...mapambano ndiyo kwanza yanaanza!

Wanapenda mtu wa ndiyo na mimi bahati mbaya sana siko hivyo, so siwezi kushinda uchaguzi ndani ya Bunge hata siku moja maana si-conform to the 'yes norm'

Ila nimepigwa kampeni chafu sana na watu wakubwa kabisa na nilijua wazi kuwa my chances were slim...na kampeni zenyewe zililenga kunichafua kuhusiana na msimamo wangu kuhusu haki na maslahi ya madaktari na sekta ya afya kwa ujumla. na pia kwenye sekta ya madini na harakati zangu za kudai haki za wananzega...nimesulubiwa kwa haya. namshukuru Mungu nimejifunza...japokuwa kwa machungu, na sasa sintotetereka tena, naijua nafasi yangu ndani ya CCM na miongoni mwa wabunge wenzangu

Nasikitika kwamba CCM imekosa watu makini wa kuelewa umuhimu na faida ya kuwa na vijana makini kama mimi na uwezo wetu wa kujenga hoja na kuweka misimamo yenye kuleta mafanikio kama ilivyojionesha, nadhani tunakoelekea si kuzuri sana ..."

Source: http://williammalecela.blogspot.cz/2012/08/mbunge-wa-nzega-apigwa-chini-bungeni-leo.html

My take: Hongera mh. Mtanda, hongera mh. Kigwangwallah, demokrasia imeshinda.

wabunge wengi wa ccm ni waumini wa waganga wa kienyeji ndio maana wamempenyeza professor maji marefu kuwa mbunge kwa sababu viongozi wengi wa ngazi za juu walikuwa wateja wake hivyo nchi hii haiongozwi kwa taaluma bali ni nguvu za giza,yakiwemo majini ,mashetani na mapepo mabaya mengi yanayowafanya watumishi wake kumfanyia hata mtetetzi wa madaktari dr ulimboka ndio maana mbunge 1 wa chadema anauwezo wa kuongoza safu za wabunge 50 wa ccm kwa sababu wao wengi wao wanaongozwa na mapepo na si taaluma.

Mkuu, Kiv. bado sijafanikiwa kuelewa connection kati ya unachoandika na topic ya thread. Would you enlighten me?!
 
"Wanapenda mtu wa ndiyo na mimi bahati mbaya sana siko hivyo" kigwa bana, Unakumbuka issue ya kung'oa PM na hoja ulizokujanazo humu JF? umesahau ulivyopitisha ile bajeti kwa mbwembwe? hlf leo unadai wewe sio mtu wa ndiyo mzeiya!!

"kuwa na misimamo mikali kwenye issues..." heheeee.. kigwa ! umeanza lini hiyo misimamo
 
Hongera sana Mhe Said Mtanda.
Natambua uwezo wako na hapana shaka kabisa utatuwakilisha vyema kwenye anga za kimataifa.
Na huyu kigwangala aache kulalamika kila siku,ubunge kura za maoni alikuwa wa tatu,ubunge wa afrika ndio aongoze? nyambafu
 
"Wanapenda mtu wa ndiyo na mimi bahati mbaya sana siko hivyo" kigwa bana, Unakumbuka issue ya kung'oa PM na hoja ulizokujanazo humu JF? umesahau ulivyopitisha ile bajeti kwa mbwembwe? hlf leo unadai wewe sio mtu wa ndiyo mzeiya!!

Kigs, siyo muungwana, alichotakiwa kufanya ni kumpongeza mh. Mtanda kwa kushinda, kwa sababu uchaguzi ulikuwa fair. Maneno anayoongea hapa yanadhihirisha kwanini hakushinda uchaguzi wa bodi ya Muhimbili, na chaguzi nyingine, anajiona yeye ana akili nyingi na uwezo mkubwa kuliko wengine. Siasa wakati mwingi huhitaji watu kukupenda na kukubali, ukiwaona wenzako ni wajinga na wewe ndio mwenye akili, hawawezi kukupenda.
 
Kazi kwelkweli Dr HK sasa hilo Jimbo la Nzega, anasemaje utaweza kuwabadili wote wapiga Kura? na (namuuliza anaposema Nasikitika kwamba CCM imekosa watu makini wa kuelewa umuhimu na faida ya kuwa na vijana makini kama mimi na uwezo wetu wa kujenga hoja hata ukihamia upinzani hayo mambo unayoyatetea wananchi wa Nzega wanayaafiki, Du kazi kwelikweli ya pili hiyo mfano ungekuwa Mbunge wa Rungwe (au Mbunge km sasa hivi) ungewashauri wanajeshi (JWTZ) wagome mpaka walipwe maslahi yao yote ndio wasonge mbele? unajua Jeshi la waMALAWI lingetuvamia na kuchukua mkoa mzima wa Mbeya na Ruvuma. basi ndio hivyo hivyo kuwaambia Madaktari gomeni mpaka mtakapolipwa, na mfano mzuri juzi Kenya wamewachukua Majreruhi wao na Maiti jiulize ni kwa nini.
Si wabunge wote wanaoafiki unayoyawaza hasa ulipojifunua katika kipindi cha Star tv kuwa ikifika Bajeti ya afya utaikwamisha,
Dr wangu lazima ufahamu kuwa km Baba uwezo wake ni wa kupanda Baiskeli ukimlazimisha kununua V8 na hana hela unamchanganya, hasa unapomwambia mbona anakunywa Pombe hela anapata wapi? asimpe mtoto mmoja kipaumbele (Dr) akumuacha kaka yake (Askari) asiye na manufaa
Hii thread najua haikuja kihivyo lakini Wabunge ndio wwanavyomuona Dr HK
 
Mhe. H K, hama tiGo njoo Voda fasta inayotikisa Chama Cha Mwabwepande kila kikicha and for sure utawakilisha na 2015 utachaguliwa. Nakuhakikishia kama utabaki huko kwa Magamba hata 2015 watakuengua. Tulia tu kwa sasa ila ikifika 2015 ukishapokea marupurupu yako ita press conferene na aga. Wakuu msiseme pengine nasujudu posho au mapato ya mbunge kwa sasa ila sitaki aishi maisha ya tabu, acha ale mihela yao kwa sasa maana hata akiiacha wenzake watabwia tu.
 
Kigs, siyo muungwana, alichotakiwa kufanya ni kumpongeza mh. Mtanda kwa kushinda, kwa sababu uchaguzi ulikuwa fair. Maneno anayoongea hapa yanadhihirisha kwanini hakushinda uchaguzi wa bodi ya Muhimbili, na chaguzi nyingine, anajiona yeye ana akili nyingi na uwezo mkubwa kuliko wengine. Siasa wakati mwingi huhitaji watu kukupenda na kukubali, ukiwaona wenzako ni wajinga na wewe ndio mwenye akili, hawawezi kukupenda.

tabia za kulialia kama NYC hazipendezi
 
Mhe. H K, hama tiGo njoo Voda fasta inayotikisa Chama Cha Mwabwepande kila kikicha and for sure utawakilisha na 2015 utachaguliwa. Nakuhakikishia kama utabaki huko kwa Magamba hata 2015 watakuengua. Tulia tu kwa sasa ila ikifika 2015 ukishapokea marupurupu yako ita press conferene na aga. Wakuu msiseme pengine nasujudu posho au mapato ya mbunge kwa sasa ila sitaki aishi maisha ya tabu, acha ale mihela yao kwa sasa maana hata akiiacha wenzake watabwia tu.

Maybe you are right...
 
Tatizo la HK ni kuchanganya uanaharakati na uanasiasa. Inabidi achague, yeye ni mwanaharakati au mwanasiasa? Mpaka sasa bado hajitambui wapi alipo.
 
Back
Top Bottom