Said Mtanda vs Dr. Hamis Kigwangalla

...CCM uwezo wa kufanya kazi ama sifa stahiki sio kigezo cha kushinda.... mtandao gani upo ndio kigezo!
 
Kigwangallah hayo maneno kayatoa wapi Chama kimemruhusu kuyasema? kwenye sahihi za zitto alisema hawezi kwenda kinyume na chama sasa kilichobakia watampeleka mabwepande
 
Kama ulikuwa unajua matokeo safi sana kuwapima upepo!!wanataka watu wa ndio ndio ndio na kusinzia wakiamka wanapiga makofi!
 
Kigwangallah unalipwa kwa unafiki wako, ulishasema kuwa ccm ndiyo ina watu wanaostahili kushika madaraka ya nchi hii. Je, utafanya kwa vitendo? Au utaishia kubwabwaja tu? Milango iko wazi kwenye nchi ya maziwa na asali na nafasi ipo, chukua hatua, uwe jasiri kijana! Wenzako kama wewe wanakusubiri, mpelekee salamu Mpina, Lugola na Filikunjombe!
 
Ccm kama hutoi rushwa hawawezi kukuchagua,mwenzake kakata mpunga wakampa,sasa hamisi nakushauri chukua hatua hicho chama hakifai
 
Analalamika nini wakati hata yeye anajua kuwa hata wananchi wa Nzega walimkataa akapitia mlango wa uani!
 
Huyoo aliyeisha demonstrate his fear factor sie huku upande wa pili hatufai hata kidogooo...upande wa mashujaa kosa kubwa ni kuwa na chembe za uwoga hasa wa kutetea na kutoa misimamo thabiti na ya haki kwa manufaa ya taifa, jamii, chama na mwisho kabisa nafsi yako mwenyewe.

Kila la kheri huko huko uliko ndugu hamisi kiiza kigwangala.
 
Muweka thread umeanzia katikakati...alikuwa anawanania nafasi gani? uenyekiti wa jumuia ya wanawake au?
 
uzi huu haueleweki ufutilie mbali kwanza hizo si kauli za Kigwangala zilipaswa ziwe quoted ili kuthibitisha usahihi wake , vile vile hujaeleza nafasi aliyokuwa anaigombea.
 
Pole sana mh.kigwangalah ila sasa baada ya kuona kuwa hupendwi nadhani kama kijana ,msomi ni wakati wa kwenda na wakati na kuzisoma alama za nyakati ambazo tayari zimekwisha somwa na wakubwa wengi 2 ila wanamalizia wakati 2 waondoke, kwa hiyo na wewe anza kuandaa mazingira ya kuondoka.
 
Said Mtanda aibuka kidedea kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika hivi punde bungeni kuwania nafasi ya ujumbe katika bunge la Africa.

Said Mtanda kapata votes 142 viz a viz Hamisi Kigwangalla with 76 votes.

Source: Toka Bungeni Live

Jamani hao wabunge wamempitisha Mtanda kwa vigezo gani? B'se ilionekana Kigwangala ana cv kubwa zaidi ya Mtanda! Au ndio kusema camps za coming general election ya 2015 ndio zilikuwa zinapimana ubavu!
 
Mara zote uwa nasema huyu Kingwangala hana uwezo wa kuwa kiongozi...nadhani angerudi kwenye fani yake ingekuwa bora sana. Maana hata kwenye kura za maoni 2010 alikuwa wa tatu na akapewa bure huo ubunge. Sasa kwa mtu kama huyu unategemea kuwa anaweza pambana na mtu aliyeshinda kwenye kura za maoni kwa kura nyingi na akapita kwenye ubunge kwa kura nyingi? Kingwangala ni mwepesi mno kwenye siasa. Na lile jimbo 2015 alipati tena.
 
Precise Pangolin embu tupe data zaidi za huyu Saidi Bangile maana twahitaji kujua...hadi ilipotokea kabadili jina. Nilisikia hata Mwigulu sio jina lake halisi???

Elimu yenyewe katumia majina ya watu badala ya jina lake la Said Bangile
 
Precise Pangolin embu tupe data zaidi za huyu Saidi Bangile maana twahitaji kujua...hadi ilipotokea kabadili jina. Nilisikia hata Mwigulu sio jina lake halisi???
Mkuu kuna thread kibao ambazo zilitoka siku za nyuma zimemuelezea sana huyu jamaa Hebu jaribu kusearch utamfahamu huyu jamaa vizuri sana mkuu wangu
 
Huyu Kigwangalla kwakweli hata huu ubunge ameupata kimagumashi magumashi tu!

Mheshimiwa Kigwangalla juzi tu aliibuka hapa akadai nao wana kundi lao ndani ya CCM la kumsimamisha mgombea wa urais 2015. Wakati huo huo chama chake kinahangaika huku na huko na propaganda za kudai kwamba kwenye CCM hamna makundi. Nikajiuliza huyu bwana ndio msemaji wa hiko kikundi ? wenzake wamemtuma aje huku JF kutangaza kwamba wana chama ndani ya chama? Au alijiamulia tu aje aseme ili hali walikubaliana kundi lao liwe siri?

I think 2015 wananchi wa Nzega watafanya maamuzi sahihi sio kuwa na huyu daktari kigeugeu ambaye mwanzo alikuwa upande wa mgomo wa madaktari baadae alipoona moto umewaka mwenyekiti wake amechachamaa aka lay low. Hilo jimbo bora atokee mtu makini huko Chadema alichukue kuliko kuwa na huyu daktari aliyekuja hapa kusema atasomea albadiri waliomtesa Ulimboka katika karne hii ya teknolojia maneno kama hayo kutoka kwa daktari! very dissapointing.
 
Mara zote uwa nasema huyu Kingwangala hana uwezo wa kuwa kiongozi...nadhani angerudi kwenye fani yake ingekuwa bora sana. Maana hata kwenye kura za maoni 2010 alikuwa wa tatu na akapewa bure huo ubunge. Sasa kwa mtu kama huyu unategemea kuwa anaweza pambana na mtu aliyeshinda kwenye kura za maoni kwa kura nyingi na akapita kwenye ubunge kwa kura nyingi? Kingwangala ni mwepesi mno kwenye siasa. Na lile jimbo 2015 alipati tena.

Nina wasi wasi kama hata huko kwenye fani ya udaktari kama ni mzuri!
 
Back
Top Bottom