Buyaka
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 1,643
- 1,786
Bakhressa akimpa Rais ''zawadi"
Bakhressa akimsomesha Rais
Rais Shein akifungua biashara ya Bakhressa
Wadau, wakati nchi bado ina kumbukumbu za karibu za vifo vya Watanzania kwa kupinduka kwa meli ambapo serikali ilibeba lawama ya kutokusimamia kanuni, taratibu na sheria za uendeshaji wa vyomo vya majini, serikali kupitia Rais wa Zanzibar, imekimbilia kwenda kukata utepe kufungua biashara ya mtu . Nchi za wenzetu ni vigumu sana kumpata Rais kwenda kufungua biashara ya mtu.
Serikali isilale kitanda kimoja na wafanyabiashara, iwakunjie uso wamiliki ili iweze kuwaratibu, sio kupewa "zawadi" na kuwachekea chekea.
Je ni alama ya kuja kuchafuka kwa the last don of Tanzania business elite, Said Salim Bakhressa?