Sahau Kambi afariki dunia

Kibunango

Platinum Member
Aug 29, 2006
8,420
2,271
Kipa wa zamani wa klabu ya Yanga, Sahau Kambi amefariki dunia jana jioni baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Kambi ambaye aliidakia Yanga kwenye miaka ya mwishoni ya 80 alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa tumbo ambalo lilisababisha alazwe KCMC na baadaye kuhamishiwa Jijini Dar es Salaam ambako alifariki dunia huko Tandika nyumbani kwa baba yake.

Kipa huyo aliichezea Yanga kwa umahiri mkubwa hadi akafanikiwa kutwaa nafasi katika kikosi cha timu ya Taifa - Taifa Stars. Hata hivyo umahiri wa Kambi uliingia dosari mwaka 1988 katika mechi ya mwisho ya ligi kati ya Simba na Yanga ambapo wapenzi wa Yanga walimtuhumu kuiachia Simba kupata bao la ushindi lililofungwa na John Makelele. Simba ilishinda 2-1, ushindi ambao uliiokoa Simba kutoshuka daraja.

Marehemu atazikwa kesho saa 7 huko Tandika Jijini Dar es Salaam.

Source: Yanga
 
Namkumbuka huyu nguli alitupa shida sana watani akiwa langoni
ninawaombea ndugu wa marehemu subira na faraja ktk kipindi hiki kigumu
 
RIP golikipa wetu Sahau Said Kambi. Yanga na wanayanga tutakukumbuka daima! Yanga Imara Daima
 
i miss you Sahau kambi........... as if i see you standing between the two posts....... and far away opposite is MOSES MKANDAWILE/IDD PAZI/MACKENZIE RAMADHANI......... without forgerting MAVUMBI OMARI.......! THE LREAL LEGEND HAS GONE ..........POLENI WATANI.....TUPOE WATANZANIA.....TUPOE WANAMICHEZO....POLENI WANAFAMILIA.......it is now the great opportunity kwa sisi tuliobaki kuzidisha na kuendelea na SALA.....!
 
Pole kwa wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki.... Sahau "Tz one" Kambi pumzika kwa amani......... Pigo kwa wanaYanga, wapenda michezo kwa ujumla!!!
 
Sahau kambi sitam sahau
Kipa aliyekuwa na kipaji
Mungu mlaze pema peponi Amen
 
Back
Top Bottom