Saga ya Familia ya Gupta kuiweka serikali ya Zuma mfukoni

Freelancer

JF-Expert Member
Sep 22, 2008
2,965
2,141
Kwa ambao mnafuatilia siasa za kimataifa, huko nchini Afrika ya kusini kulikuwa na kashfa kuhusu serikali ya Zuma kuwekwa mfukoni na familia maarufu ya wafanyabiashara wenye asili ya kiasia wajulikanao kam Gupta. Kuna taasisi ambayo kazi yake ni kuchunguza "misconduct" zozote zinazofanywa na maofisa wa umma. Ipo kama tume ya maadili hapa kwetu ila hii ina meno zaidi. Hii taasisi imekuwa mwiba mkali sana kwa Rais Zuma kuanzia kwenye ile kashfa ya Zuma kutumia fedha za umma kufanya marekebisho katika makazi yake binafsi huko kijijini kwao. Hii taasisi ilikuwa inaongonzwa na mwanamama anaitwa Advocate Thuli Mandosela. Ijumaa iliyopita (nafikiri tarehe 14/10/2016) ndo ilikuwa tarehe yake ya mwisho kuwepo ofisini kwa hiyo akawa anataka kurelease taarifa za uchunguzi wao kuhusu sakata la familia ya Gupta kuiweka mfukoni serikali. Ina onekana ripoti haijakaa vizuri itamharibia Zuma pamoja na ANC kisiasa kwa hiyo serikali ya Zuma ikakimbilia mahakamani ili mahakama itoe zuio la ripoti kusomwa kwa umma. Kwa wachambuzi wa mambo wanasema hii ilikuwa ni delaying tactic kwa kujua fika kwamba mrithi wa Mandosela hataweza kuirelease ripoti. Inasemekana serikali ya Zuma walikuwa wanataka Advocate Mandonsela aondoke ofisini bila kuisoma. Kuna mwanamama mwingine ndo ameteuliwa na bunge kushika hiyo nafasi anaitwa Advocate Busisiwe Mkhwebane. Huyu mama anatokea State Security Agency (SSA) ambayo ndo kama TISS ya afrika kusini. Kupata hiyo nafasi huyo mama alikuwa na back up ya watu wa ANC (wabunge wengi ni wa ANC) kwa maana ni watu wa Zuma. Kwa mujibu wa dokezo mbali mbali kuna watu ambao walikuwa more qualified na wana experience kubwa kuliko huyo mwanamama lakini hawakupendekezwa sababu kura zilikuwa zinapigwa na wabunge na wabunge na watu wa ANC ndo walikuwa wengi. Chama cha upinzani cha DA(Democratic Alliance) kilijaribu kuweka pingamizi kwa kusema kwamba wanazo habari kutoka vyanzo vya uhakika kwamba huyo mama amekuwa spy wa muda mrefu kwa hiyo upo uwezekano wa kwamba akawa loyal kwa ANC kama walivyo maafisa wengi wa SSA. Hizi tuhuma zimepingwa na huyo mwanamama na anadai kwamba yeye amejiunga na SSA mwaka huu julai. Kabla ya hapo alikuwa uhamiaji. DA wanasema kwamba tayari alishakuwa undercover spy toka alipokuwa uhamiaji na amefanya kazi nchi mbali mbali kama vile ubalozi wa SA nchini China kwenye branch ya uhamiaji. Kwa hiyo inaonekana ni mkakati wa Zuma kuweka spy ili aweze ku "contain" hiyo situation. Mazingira yake ya kutoka Immigration mpaka SSA yanatatanisha kwa sababu alikuwa mkurugenzi huko uhamiaji akaenda SSA ambako amekuwa analyst. Kwa hiyo DA wanasema alikuwa undercover spy miaka yote na amerudi tu SSA officially. Hili sakata la Gupta ni zito sana. Inasemekana limefanya aliyekuwa mkurugenzi wa SSA kutoka mwaka 2013 ajiuzulu hivi majuzi (August 2016). Huyu pia alikuwa mwanamama anayeitwa Sonto Kudjoe. Inasemekana alikuwa ana poke kwenye ishu ya Gupta kwa hiyo ikabidi tu wafikie mutual agreement ajiuzulu bila shari.. Hayo ndo yanaendelea huko Afrika ya kusini. Kuna uwezekano mkubwa kabisa huyu Advocate asirelease hiyo report kwa kisingizio cha usalama wa taifa. Kwa hiyo watai categorize report kama ni top secret.
 
Ila hawa ndugu zetu Wa kiasia wanatuburuza sana..siku zote ukishakubali kufanya nao biashara kaa ukijua itakula kwako zaidi..Na wanajisifu kabisa jinsi wanavyoingia mikataba mikubwa na nchi tofauti ambayo mingi ina utata.. Na kujitajirisha kwa kuwaziba midomo hawa tunaowaita "Waheshimiwa"
 
Summary nzuri, tupia sosi ili tuendelee kufuatilia
zipo multiple sources. Google hayo majina niliyoweka kama Gupta, Mandosela, State Capture South Africa, etc..

Mkhwebane will not fight Zuma's State Capture report interdict

Des van Rooyen withdraws 'state capture' interdict application

Fight over release of 'state capture' report

South Africa is at an inflection point: will it resist, or succumb to state capture?

kwa hiyo "State Capture South Africa" ndo keyword muhimu kwa kufuatilia
 
Back
Top Bottom