ATCL wawakilisha sababu za kuharibikiwa
Mwandishi Wetu
Daily News; Friday,December 19, 2008 @21:15
Habari nyingine
ATCL wawakilisha sababu za kuharibikiwa
Mpigapicha wa Channel Ten aagwa
TSN watoa msaada wa kompyuta
Zimbabwe isaidiwe kukabili kipindupindu
Mgonja kula sikukuu uraiani
Basi laua polisi watatu
Bilioni 40 /- za mafisadi zanufaisha wakulima
Bodi ya ATCL matatani
Ujenzi wa barabara mpya Dar waiva
Dhamana ya Mgonja yakamilika
Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), imewasilisha kwa Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu ripoti ya maelezo ya kwa nini kampuni imefika hatua mbaya baada ya kupewa siku saba za kujieleza.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Balozi Mustafa Nyanganyi aliliambia gazeti hili jana kuwa siku saba walizopewa na Waziri Dk. Shukuru Kawambwa zilianza Jumatatu na zinamalizika kesho, lakini walikamilisha kabla na tayari wameiwasilisha kwake.
Dk. Kawambwa juzi katika mkutano na waandishi wa habari, alisema ameipa bodi siku saba ieleze ni kwa nini ATCL imefikia kufungiwa na kuahidi kuwa baada ya maelezo hayo wale wote watakaobainika kuhusika atawawajibisha ipasavyo.
Katika mahojiano na gazeti hili jana kuhusu hali ya kampuni hiyo na matakwa ya wafanyakazi wa ATCL ya kumtaka ajiuzulu pamoja na Menejimenti inayoongozwa na Mkurugenzi, David Mattaka, Balozi Nyanganyi alisema kujiuzulu kwake si tatizo, anaweza kufanya hivyo, lakini tatizo ni mtaji mdogo wa kuendesha kampuni hiyo.
Unadhani tatizo ni kujiuzulu? Watu hawajui tulikuwa tukijiendesha vipi kwa kipindi chote cha miaka miwili, tuliomba mtaji kwa serikali wa US dollar milioni sabini na sita (takribani Sh bilioni 91.2) kuendesha kampuni, lakini kutokana na kuwa serikali nayo haina fedha, tumekwama mpaka leo, alisema Nyanganyi.
Alisema hata hivyo waliandika maombi ya kupatiwa fedha kwa ajili ya kutafuta na kuchagua wataalamu wa kusaidia uendeshaji wa kampuni wenye ujuzi wa kiwango cha juu, lakini ukosefu wa fedha ulisababisha baadhi ya kampuni ikiwa ni pamoja na yaliokuwa yakiandika nyaraka ya ndege mpya ya Air Bus na DASH8-Q300 kushindwa kuendelea kwani zilihitaji Euro 360,000.
Alisema hata hivyo wanaendelea na juhudi za kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanapata mshahara wa Desemba kwa wakati hata kama kampuni hiyo haizalishi na kwamba viwango vya kukidhi kumaliza dosari zilizoainishwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) vinatarajia kukamilika.
Kuhusu hatua za serikali kuinusuru ATCL kwa kuiongezea mtaji, alisema ni bora na italeta manufaa makubwa endapo ikitekelezeka kwa haraka. Aidha, taarifa zilizopatikana jana kutoka wizarani zilieleza kuwa Waziri Kawambwa alikutana na viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Mawasiliano na Uchukuzi, COTWU jana kwa ajili ya kuzungumzia hatua za serikali kwa madai yao na kuhakikishiwa mishahara kwa wakati.