Safari..

Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,328
23,879
Niliianza safari, japo likuwa mdogo,
niliionja futari, au asali ya gogo,
sikuiona hatari, wala sikuona dogo,
niliianza safari, safari yangu pendoni.

Ilikuwa na utamu, ukweli siwezi ficha,
iliniongeza hamu, safari singeiacha,
nilijifanya hakimu, nikaapa sitoacha,
niliianza safari, safari yangu pendoni.

Siku nenda siku rudi, alinipenda jamani,
kueleza sina budi, penzi tulilithamini,
tulipendana shahidi, kuachana sikudhani,
niliianza safari, safari yangu pendoni.

...to be continued!
 
Niliianza safari, japo likuwa mdogo,
niliionja futari, au asali ya gogo,
sikuiona hatari, wala sikuona dogo,
niliianza safari, safari yangu pendoni.

Ilikuwa na utamu, ukweli siwezi ficha,
iliniongeza hamu, safari singeiacha,
nilijifanya hakimu, nikaapa sitoacha,
niliianza safari, safari yangu pendoni.

Siku nenda siku rudi, alinipenda jamani,
kueleza sina budi, penzi tulilithamini,
tulipendana shahidi, kuachana sikudhani,
niliianza safari, safari yangu pendoni.

...to be continued!


Mi si mtaalamu wa lugha, Lakini Kama bdo Unaendelea na huyo uloanza nae safari..ni jambo jema sana.Well and good.
 
Niliianza safari, japo likuwa mdogo,
niliionja futari, au asali ya gogo,
sikuiona hatari, wala sikuona dogo,
niliianza safari, safari yangu pendoni.
so u mean ulianza mapenzi ukiwa bado kinda shule ya msingi Kwimba. Au?
 
1.
Ubeti huu wa kwanza, hoja yako kuchangia,
Safari uliyoianza, siku bado kutimia,
Pasi mwalimu kufunza, kitanda ukarukia,
Safari bado kuanza, japo ndiyo yaishia

2.
Safari yako ya hima, tena isiyo na shari,
Wadhani huwezi kwama, hata wakati wa hari,
Hilo laweza simama, bila kutoa hadhari,
Safari bado kuanza, japo ndiyo yaishia

3.
Nimekurushia fataki, ili uanze fikara,
Wala siyo kuhamaki, bali ukune kipara,
Kama mpara samaki, Yule asiye na dira,
Safari bado kuanza, japo ndiyo yaishia

4.
Anza sasa tafakuri, juu ya yako kauli,
Ati unayo safari, kabla ya hiyo nauli,
Utavukaje bahari, nawe wapanda bakuli,
Safari bado kuanza, japo ndiyo yaishia

5.
Mapenzi uloanza , hakika siyo asali,
Japo watoka uvinza, shurti kwanza usali,
Tena bila kuviza, wale wasafiri kweli,
Safari bado kuanza, japo ndiyo yaishia

6.
Uzoefu waonesha, mwisho wa pendo udhia,
Busu zikali nyesha, mengine yaja tibua,
Japo waweza kesha, bila pendo kuokoa,
Safari bado kuanza, japo ndiyo yaishia

7.
Utamu uliolamba, ndiyo wenyewe utamu,
ukikinai mtamba, koo hakidhi hamu,
Utakimbilia kamba, hima kujihukumu,
Safari bado kuanza, japo ndiyo yaishia

8.
Shukuru ulicholamba, zaidi yake hakuna,
Uache huko kutamba, demu lisije kununa,
Utatamtmani komba, demu huyo akiguna,
Safari bado kuanza, japo ndiyo yaishia

9.
Mwisho nakupongeza, kwa penzi kuweka wazi,
Japo si wa kwanza, kupiga mwenzi kwa jozi,
Sasa ule machenza, pasi toa machozi,
Safari bado kuanza, japo ndiyo yaishia.
 
Mgombea wadakia, ila asante kujibu
kitanda sijarukia, wala hakuna sababu
sihitaji kufundishwa, ama kupewa jawabu
Safari niliianza, na bado yaendelea!

Safari lianza vema, na bado liendelea
sikujuta fanya hima, kwani bado natembea
utamu ndo warindima, ngoma sijaiachia
safari niliianza, na bado yaendelea!

asante kwa lako fataki, ndo kwanza meniamsha
niligubikwa na chuki, sikupata mshawasha
kama nimenyweshwa siki, kwa aliyonionyesha
safari niliianza, na bado yaendelea

binti niliyempenda, mikasa kaniletea
mwanaume sikupinda, kamba nikashikilia
moyo akaniponda, halafu kanikimbia
safari niliianza, na bado yaendelea!

asali likuwa tamu, nikawasahau nyuki
nilipaonja patamu, katolewa kwa mikiki
penzi kaweka hatamu, hivi sasa kenda wiki,
safari niliianza, na bado yaendelea!

Naamini bila yeye, singeyajua machungu
ingawa sikudhani yeye, angekuwa nungunungu
moyo nilimpa yeye, akanitoa manundu
safari niliianza, na bado yaendelea!

to be continued...
 
Hongereni sana wataalamu wa lugha, kumbe jukwa la Shaan Sudi Andanenga bado lingalipo, big up JF.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom