Safari za Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005

nahisi kabla ya kumaliza hii ngwe ilyobaki huenda anataka kufika mpaka visiwa vya Tonga,Vanuatu,New papua Guinea,Somoa,Sumatra,Guyana,Fiji n.k.
Rais wetu inabidi ajifakirie mara mbili sasa kuhusu safari zake.Thats too much!

Alishawahisema kama asiposafiri mngekufa na njaa
 
"JAMAN MNYONGE MNYONGEN HAKI YAKE MPENI, BILA SAFARI ZANGU ZA NJE MNGEKUFA NJAA" presdaa.. KAMA VP TUNGEMRUHUSU AKAE HUKOHUKO NJE ATAFUTE MISAADA NA WAWEKEZAJI INCHI AMUACHIE MAKAMU WAKE
 
.......
Je tunapata tija gani kama nchi kwa safari hizi ambazo kama kweli ni 313 means amekuwa nje almost the whole year! Ukiacha 28days za likizo...sasa wasting a year in 5yr reign is no small joke, his pace can only be beaten by Mugabe........

Kwa hesabu ya haraka haraka kama ni kweli amesfiri mara 313 na amekaa safarini kwa siku tatu...UWIIIIIIII inamaanisha ameishi nje ya nchi min siku 939......INATISHA.

Mhe Mnyika amedai safari ya Mkulu na nakuu "
Msafara mmoja wa Rais kwenda nje unagharimu kidogo sana ni shilingi milioni 50 na wakati mwingine msafara unakwenda mpaka shilingi milioni 200 na safari ni nyingi kweli kweli. "

mwenye calculator atusaidie hizo hesabu maana yangu ina digits kidogo.
 
Anaomba kila wakati patokee msiba nje ya nchi aende kama sio ndugu wa Michael Jackson kusema wanahitaji mazishi ya faragha angeweza kwenda ... Hivi ile harusi ya Prince William alishindwaje kwenda au alikuwa nchi nyingine...???
 
nahisi kabla ya kumaliza hii ngwe ilyobaki huenda anataka kufika mpaka visiwa vya Tonga,Vanuatu,New papua Guinea,Somoa,Sumatra,Guyana,Fiji n.k.Rais wetu inabidi ajifakirie mara mbili sasa kuhusu safari zake.Thats too much!
Itabidi nimlipue...
 
Anaomba kila wakati patokee msiba nje ya nchi aende kama sio ndugu wa Michael Jackson kusema wanahitaji mazishi ya faragha angeweza kwenda ... Hivi ile harusi ya Prince William alishindwaje kwenda au alikuwa nchi nyingine...???
Hana kheshima za kutosha kualikwa kwenye Royal Wedding .. Hataakaa aalikwe...
 
Hospitali/zahanati hakuna, chakula haba, wanavyuo hakuna mikopo ya uhakika, maji safi ni ndoto, umeme ndio usiseme. Hivi kama nusu tu ya pesa ya safari kama ingeelekezwa katika mahitaji ya hawa watanzania nadhani kungeweza kuwa na ahueni ya maisha. Nadhani JMK ana mpango wa kuiuza nchi. JMK tuonee huuruma watz.
 
Du sasa kama hiyo ni safari ya 313, ina maana ukichukua average ya siku mbili kila safari si ni 2 years yuko nje ya nchi. Wakuu kama hii ni kweli basi ni disaster!!!!!!!!
 
swla sio mkuu wa kaya kwenda nje kama hii ishu ya juba alipaswa aende na wafanyabiashara wa bongo huko ili wafanye hela yeye anaenda kuuza sura yaani bongo kazi kwelikweli..
 
swali zuri sema its too general,safari ya wapi manake it differs africa, ulaya,asia ,america etc......vile vile na ukubwa wa msafara pia.....ila kwa huyu jamaa anavyosafiri na kundi lake kokote pale ndungu zangu mi nimebahatika kujua maswala ya mambo ya nje huu utawala unatumaliza na inshort umeshatumaliza ukifatilia kujua garama watu mutaingia mtaani hata kesho......
 
Kwa kweli ni vigumu kufahamu ukizingatia kwamba matumizi ya raisi hayapaswi kuhojiwa mahali popote pale na matumizi yake hayakaguliwi na cag.
Kwa kifupi zile safari zinaghalimu taifa mabilioni ya shilingi, wewe i megine msafara wa watu 50 na kuendelea.
Nikwamba safari moja kwa ulaya na marekani inaghalimu c chini ya 5 bilioni.
1.posho za viongozi wa msafara na posho zao zinakuwa ni katika international rate, c rate ya hapa bong
2. Mafuta ya ndege na ile ndege inakunywa mafuta c mchezo waarabu wenyewe pamoja na kuwa na mafuta wanaziogopa sana ndegeza type hiyo ya raisi
3. Matengenezo ya ndege
4. Hotel five star
5. Matibabu/bima ya afya kwa msafara
6. Ukodishwaji wa magari ya kupigia misere wakiwa huko ziarani.
7. Ghalama za kuandaa tafirija mbalimbali wakiwa huko,

kwa kifupi ni bilion of money
 
Naona kuna haja ya kuwa na kasehemu kwenye katika kanachotaka raisi akienda nje akirudi lazima aje fanya retirement na kabla ya kwenda aseme dhumuni na cost to be incurred na je anachofuata is it worth gharama aliyoingia?
 
nakumbuka safari ya sumaye marekani wakati fulani ili cost dola 500,000 kwahiyo unaweza ku make conclusion kutokea hapo lakini swali lako
is too general be more specific.
 
[h=1]Safari za Kikwete zakausha hazina[/h]
picture-22.jpg

Imechapwa 12 May 2010

jk_99.jpg



SAFARI za Rais Jakaya Kikwete nje ya nchi, tangu alipoingia madarakani, zimeligharimu taifa mabilioni ya shilingi, MwanaHALISI limebaini.
Uchunguzi umeonyesha kuwa katika kipindi cha miaka minne tangu awe rais, Kikwete amekaa nje ya nchi kwa takribani siku 120, sawa na miezi minne.
Hadi mwishoni mwa mwaka jana, kiasi cha Sh. 2.4 bilioni zilikuwa zimetumika kwa ajili ya posho na gharama za malazi kwa rais na ujumbe wake nchi za nje.
Mara nyingi, ujumbe wa rais huhusisha mkewe, walinzi, waziri kutoka wizara inayohusika na safari, waziri wa mambo ya nje, pamoja na wasaidizi binafsi wa rais na wale wa mke wake.
Kwa mujibu wa uzoefu wa safari, ujumbe wa rais anaposafiri nje ya nchi huwa na kati ya wajumbe 15 na 22.
Kwa viwango vya serikali, watu wanaosafiri kwenye msafara wa rais hulipwa kiasi cha kati ya dola 350 na 500 (Sh. 600,000 kwa siku).
Hata hivyo, MwanaHALISI limeambiwa kuwa rais hutakiwa kulala katika hoteli yenye hadhi ya aina yake – ambayo gharama yake huwa kati ya dola 800 na 1,200.
Kwa kuimarisha ulinzi na kukabiliana na upweke, hoteli anakolala rais hulaza pia walau watu wanne, gazeti limeelezwa.
Hawa wanaweza kuwa walinzi wa rais, daktari na wasaidizi wake wa karibu ambao anaweza kuwahitaji wakati wowote.
Kwa hiyo, kwa msafara wa watu 20 ambayo ni idadi ya kawaida kwa msafara wa rais, hasa anapokwenda nje ya nchi, wastani wa matumizi kwa siku inaweza kufikia kiasi cha dola 15,000 (Sh. milioni 20).
Kwa safari kama ya Mei 12 hadi Mei 26 mwaka 2006, wakati Rais Kikwete alipokuwa nje ya nchi kwa karibu wiki mbili, kiasi cha Sh. 273 milioni kilitumika kwa ajili ya safari hiyo pekee.
Katika safari yake hiyo, Rais Kikwete alitembelea Uganda, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Ufaransa na Marekani.
Katika mahojiano mbalimbali ambayo MwanaHALISI limefanya na wafanyakazi wa ikulu pamoja na wizara ya mambo ya nje, gazeti limeambiwa kwamba kiasi hicho (Sh milioni 273) "si kikubwa sana" kwa viwango vya matumizi wakati wa ziara za wakubwa nje ya nchi.
Kwa safari hiyo pekee, Kikwete alitumia fedha nyingi kuliko kiasi cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya safari zake zote za nje ya nchi kwa mwaka huu wa fedha (2009/2010).
Kwa mujibu wa bajeti ya mwaka huu, rais ametengewa Sh. 115 milioni kwa safari za nje; takwimu ambazo zimeleta utata ikilinganishwa na matumizi kwa safari za ughaibuni.
Kwa mfano, bajeti ya safari za nje, kwa mujibu wa bajeti ya 2009/2010, imekuwa ndogo kiasi kwamba kwa uzoefu, fedha zote zinaweza kutumika kwa safari moja tu.
Aidha, bajeti ya ikulu ya safari za ndani ya nchi nayo imeongezeka kutoka Sh. 608,419,000 kwa bajeti ya mwaka 2008/2009 hadi Sh. 723,360,000 kwa mwaka 2009/2010, ikiwa ni ongezeko la Sh. milioni 114.9.
Kwa takwimu hizi, matumizi ya safari za ndani za ikulu (rais) yanaonekana kuwa makubwa kuliko yale ya nje, jambo ambalo wazoefu wa safari za ikulu wameeleza kuwa siyo sahihi.
Miongoni mwa mambo ambayo Rais Kikwete amekuwa akilalamikiwa na wanasiasa, wanaharakati na wananchi kwa jumla, ni wingi wa safari zake za nje ambazo zinaelezwa kuwa zinachota fedha nyingi kwa manufaa haba.
Rais alifanya safari nyingi mwaka 2006 hadi kulalamikiwa na wananchi. Miongoni mwa safari za mwaka huo pekee ni kama ifuatavyo:
  • Tarehe 19-25 Januari alikuwa Khartoum, Sudan kuhudhuria mkutano wa nchi za Afrika (AU)
  • 23 Machi alifanya ziara ya siku moja ya kiserikali kujitambulisha Kigali, Rwanda.
  • Tarehe 22 Machi rais alikwenda Kampala, Uganda kwa ziara ya siku moja ya kujitambulisha
  • 24 Machi alikwenda Nairobi, Kenya
  • 19-20 Aprili alikuwa Lesotho na Swaziland.
  • Tarehe 21-22 Aprili rais alikuwa ziarani Maputo, Msumbiji;
  • 28 Aprili alikuwa Harare na Bulawayo, nchini Zimbabwe
  • 6 Aprili alikuwa Gaborone, Botswana.
  • Rais alikuwa ziarani Namibia 10-12 Aprili;
  • Tarehe 7-9 Mei alikuwa Pretoria, Afrika Kusini.
  • Tarehe 12 Mei rais alianza ziara ya wiki mbili katika nchi za Uganda (13 Mei), Arabuni (15 Mei), Ufaransa (16-19 Mei) na Marekani (21-26 Mei).
  • Tarehe 31 Mei hadi 3 Juni rais alihudhuria Jukwaa la Kiuchumi la Dunia mjini Cape Town, Afrika Kusini
  • Tarehe 4 Julai alihudhuria mkutano wa AU, Banjul nchini Gambia.
  • Julai 10-12 rais alikuwa Cape Town, Afrika Kusini kuhudhuria mkutano wa viongozi wa serikali ulioandaliwa na kampuni ya Microsoft ya Marekani
  • 20 Julai alihudhuria mkutano wa Leon Sullivan, Abuja nchini Nigeria.
  • Rais alikuwa Berlin 21 na 22 Julai kwa ajili ya kuchunguza afya yake;
  • Alihudhuria mkutano wa SADC, Maseru nchini Lesotho kati ya 19 na 20 Agosti
  • Tarehe 21-22 mwezi huo alikuwa ziarani Angola.
  • Rais Jakaya Kikwete alikuwa Cuba tarehe 12 Septemba kwa maandalizi ya kikao cha Nchi zisizofungamana na upande wowote (NAM);
  • 15 Septemba alikwenda Madrid, Hispania kwenye Uwanja wa Mpira wa uwanja wa Santiago Bernabeau unaotumiwa na klabu mashuhuri ya Real Madrid.
  • Septemba 15 hadi18, rais alikuwa Havana, Cuba kwa mkutano wa NAM
  • Kati ya 19 na 25 Septemba, rais alikuwa kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York.
MwanaHALISI lina taarifa kuwa tayari matumizi ya serikali kwa jumla mwaka huu wa fedha yamezidi kiwango kilichoombwa wakati wa kikao cha Bunge la bajeti mwaka jana.
Enzi za utawala wa Rais Benjamin Mkapa, kuna wakati ilidaiwa kwamba Waziri Mkuu, Frederick Sumaye, alitumia kiasi cha Sh. 500 milioni kwa safari moja tu nchini Marekani.
Pia mwaka 1990, msafara wa Tanzania ulioongozwa na Rais Ali Hassan Mwinyi kwenye mkutano wa Dunia wa Mazingira uliofanyika Rio de Janeiro nchini Brazil, ulinusurika kuzuiwa kuondoka baada ya kumaliza fedha zote zilizotolewa.
Miongoni mwa maofisa wa ngazi za juu wa wizara ya mambo ya nje waliozungumza na gazeti hili wiki iliyopita, wakati wa safari yoyote ya rais nje ya nchi, sharti msafara uwe na angalau dola 50,000 hadi 100,000 (kati ya Sh. 70 na 140 milioni).
"Unajua haya mambo wakati mwingine yanategemea na kiongozi wa nchi uliye naye. Kama unasafiri na Nyerere siyo sawa na kama unasafiri na Mobutu. Kama kiongozi ni mfujaji mtatumia fedha nyingi na kama kiongozi si mfujaji basi mtatumia fedha kidogo.
"Cha msingi ni kwa mkuu wa msafara kutoa taarifa serikalini kuhusu matumizi. Si kwamba kama utapewa dola 50,000 basi ni lazima uzitumie zote hadi ziishe. Lakini kama kiongozi anajua kutumia, hela zitaisha tu. Si mradi zitolewe maelezo tu," alisema.
Uchunguzi umebaini kuwa tangu awe rais, Kikwete ameonekana kupendelea sana kwenda nchini Marekani na Uingereza.
Hadi mwanzoni mwa mwaka huu, Kikwete ametembelea Marekani mara nane na Uingereza zaidi ya mara nne; mara nyingine akipitia tu kutoka katika nchi nyingine.
Tathmini ya MwanaHALISI imeonyesha kwamba kwa wastani, ziara za Kikwete katika nchi za Afrika huchukua wastani wa siku mbili wakati Ulaya huchukua wastani wa siku tatu hadi nne.
Pia, Kikwete alifanya safari nyingi zaidi ughaibuni mwaka 2006 kwa lengo la kujitambulisha kwa nchi mbalimbali na mwaka 2008 alipokuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).
MwanaHALISI limefanikiwa kukusanya orodha ya safari zote ambazo Kikwete amefanya tangu alipoingia madarakani hadi mwanzoni mwa mwaka huu.
Gazeti toleo na. 188


0








Average: Select ratingPoorOkayGoodGreatAwesome
 
Back
Top Bottom