Safari yataka kuvunja ndoa msaada

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,766
894
Wadau JF.

Tunaitaji msaada kuokoa ndoa ya jamaa yangu.

Zimepita wiki tatu toka kisa hiki kitokee, jamaa yangu alipanga safari yake ya kibiashara kwenda Japan..

Wakati yupo nyumbani akijiandaa na safari huku wakiongea na mke wake.

Muda ulivyofika kuanza safari ya airport alikuwa anaondoka na Air Qatar mchana, akamuomba mke wake simu ili ampigie dereva wa tax aje kumchukuwa.

Simu yake ilikuwa imeishiwa pesa, wakati kachukuwa ile simu ya mke wake ili apige sms ikaingia, akaona ngoja haisome kwanza..

Maneno aliosoma yameandikwa hivi "Dear vp huyo bwegge kaishaondoka? Nimekumiss sana leo takuja kulala"..

Jamaa yangu alivyomaliza kusoma akampa ile simu mke wake akamwambia soma sms yako..

Jamaa akabeba begi lake na kuondoka kuelekea airport aliporudi kutoka safari hakumkuta mke wake nyumbani..

Alipompigia simu akamwambia yupo nyumbani kwa dada yake mume wake ndipo alipokimbilia baada ya kisa kile..

Ushauri wakuu jamaa yangu anaomba!
 
Good_wanaume ndio sisi,wengine ni mafisi tu....nilifikiri ataahirisha safari kwa kuleta maugonvi,.....mpe big up sana jamaa yako...real men should act like that.
 
Sasa mkuu, unashauri nini kifanyike?
 
Sasa anataka ushauri wa nini hapo? kama mkemwenyewe kaenda kwao hakumfukuza sasaakili kichwani mwake, kama bado anampenda aendelea nae wala asitake ushauri yeye ndio mwenye mali akiitoa sadaka yake akiifanyia biashara yake mwenyewe.
 
Mkuu,
Mke kaenda kwa dada yake Mume wake yaani kwa wifi yake..
 
ndoa hizi,
amuite mkewe ajieleze kwa nini amecheat, mkewe akiri kutorudia tena(kama yupo tayari) kucheat, kuvunja uhusiano na huyo mwanaume wa pembeni na akiridhika na maelezo ya mkewe na kama ataomba msamaha amsamehe (kumbuka makosa mangapi wanaume mnayotena wake zenu wanasamehe?) amrudie mkewe.
 
Hakuna cha kushauri kwenye huu mtanange
Mke ameshachukua uamuzi
OTIS
 
ndoa hizi,
amuite mkewe ajieleze kwa nini amecheat, mkewe akiri kutorudia tena(kama yupo tayari) kucheat, kuvunja uhusiano na huyo mwanaume wa pembeni na akiridhika na maelezo ya mkewe na kama ataomba msamaha amsamehe (kumbuka makosa mangapi wanaume mnayotena wake zenu wanasamehe?) amrudie mkewe.

Mkuu.
Ngoja nichukue huu ushauri nimpelekee jamaa yangu!
 
Hivi unadhani atajieleza nini huyo mwanamke???Jamaa afanye uchunguzi kwanza kama ni kweli. Then kama ni kweli hakuna mke hapo.. au jamaa amezidi kusafiri sana??????
 
ndoa hizi,
amuite mkewe ajieleze kwa nini amecheat, mkewe akiri kutorudia tena(kama yupo tayari) kucheat, kuvunja uhusiano na huyo mwanaume wa pembeni na akiridhika na maelezo ya mkewe na kama ataomba msamaha amsamehe (kumbuka makosa mangapi wanaume mnayotena wake zenu wanasamehe?) amrudie mkewe.
mmmmmmmh.......kweli nimeamini watu(wanaume) wengine wana mioyo na roho nzuri kuliko hata malaika.
 
sijaelewa anataka ashuriwe nini, mke kaenda kuongeza maujuzi yeye analalamika. Amwache huko huko akifuzu atarudi tu
 
Sasa ushauri gani anataka???
Ni either aende akamsombe mkewe huko kwa dadake amrudishe nyumbani au amfungashie virago vyake ampelekee.
Na hayo maamuzi hamna anaetakiwa kuyafanya zaidi yake yeye mwenyewe maana kama ni kuishi kama ***** ataishi yeye na kama ni kumkosa mkewe atamkosa yeye....aangalie kama uwezekano wa kumsamehe na kuendelea nae upo akaongee nae na kama anaona hawezi kuendelea nae amjulishe!!
 
Mie kilichoniuma ni jamaa kuitwa *****, yaani inaonekana huyo mama sio mara ya kwanza anatumiwa meseji za namna kwa mume kuitwa ***** na anaridhika, hamthamini kabisa mume wake, kweli ningemuambia dada yangu amtimue na kwangu asikanyage, kucheat nimegundua, ningesamehe, lakini kucheat na anaye acheat kuniita ***** haivumiliki.
 
Hebu fikiria unavyomkunja mkeo kwenye sita kwa sita, mapaja anavyoyatanua, miguno anayoitoa then aje afanywe hivyo na mwanaume mwingine tena huwezi jua wengine huruka hadi ukuta tena daaah me sikubaliiiii bora nimwache.
 
Kwa maelezo hayo machache inaonekana huyo jamaa anasafiri sana na hana muda na mke wake yuko kibiashara zaidi na ndo maana rijamaa rinasema hiro ***** halijaondoka? cha msingi ni kumrudisha mama nyumbani na kuanza maisha upya kwanza ajiuile kwanini mwanamke anafanya hvyo inawezekana nae pia ni tatizo inawezekana mama anapata kutu anaumua kwenda kuosha nje.
 
Sasa ushauri gani anataka???
Ni either aende akamsombe mkewe huko kwa dadake amrudishe nyumbani au amfungashie virago vyake ampelekee.
Na hayo maamuzi hamna anaetakiwa kuyafanya zaidi yake yeye mwenyewe maana kama ni kuishi kama ***** ataishi yeye na kama ni kumkosa mkewe atamkosa yeye....aangalie kama uwezekano wa kumsamehe na kuendelea nae upo akaongee nae na kama anaona hawezi kuendelea nae amjulishe!!

Lizzy.
Mbona umetoa ushauri mzuri tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom