Safari yangu Selous - Picha na Misamiati niliyojifunza.

Mie nitawasilisha picha za huku ngorongoro crater baada ya vacation, ni pazuri mno! bongo raha jamani....

mkuu ninatamani kufika hapo maana nina mpango wa kufungua Gallery na ninasikia huko kuna maajabu na vivutio mbalimbali ukiaachana na wanyama...
Ukienda Jukwaa la Biashara kuna thread kule nimeanzisha... (Wakuu nahitaji mawazo yenu)
 
Nimeku-zoom Gustavo mpaka nimekuona yuleeee. Utalii wa nchini ni mzuri sana, ni kujipanga tu kunatakiwa!!

Thanks for sharing mapicha!
 
Ukiacha wanyama, askari pori akisema mkuki maana yake bunduki
 
Mie nitawasilisha picha za huku ngorongoro crater baada ya vacation, ni pazuri mno! bongo raha jamani....

Kwa kweli Ngorongoro crater ni pazuri sana na ukikuta siku hiyo hamna ukungu ndani utapenda kuangalia. Tuliwakuta Wamasai pale na ukitaka kupiga nao picha jiandae kuwalipa maana baada tu ya kupiga picha wanakuomba pesa, ole wako usiwape, patachimbika. Tanzania is so beautiful. Glory to GOD.
 
Baba mbona zile picha nilizoonekana hujaziweka humu?
Yani kukubali kwangu kuwapiga picha ndio nilizohusika hujaziweka!
Siku nyingine hata unigombeze sishiki camera ili na mie niuze sura jf lol!
 
Baba mbona zile picha nilizoonekana hujaziweka humu?
Yani kukubali kwangu kuwapiga picha ndio nilizohusika hujaziweka!
Siku nyingine hata unigombeze sishiki camera ili na mie niuze sura jf lol!
Acha baba yako auze sura kwanza humu JF, nyie watoto msubiri ukifika wakati wenu..................
Unataka watu waanze kukugombea au? Subiri mwakani tukienda Ngorongoro itakuwa zamu yako kuuza sura.......sasa umefurahi eh!
View attachment 48147
Nimeweka hii, umeonekana kwa mbali
 
Acha baba yako auze sura kwanza humu JF, nyie watoto msubiri ukifika wakati wenu..................
Unataka watu waanze kukugombea au? Subiri mwakani tukienda Ngorongoro itakuwa zamu yako kuuza sura.......sasa umefurahi eh!
View attachment 48147
Nimeweka hii, umeonekana kwa mbali
Asa mbona unanibani baba,hutaki wakwe?afadhali nikizoom naonekana lol!nimefurahi kidogo!!
 
Hivi karibuni nilitembelea Selous na miongoni mwa mambo niliyojifunza ni lugha inayotumiwa na Tour Guide katika kuwasiliana pale wanapoulizana mahali walipo wanyama Fulani. Kule wanyama hawaitwi kwa majina yao halisi, bali wamewapa majina yao wenyewe ambayo wao kwa wao wanaelewana, nitataja machache na kama kuna mtu anajua zaidi atatujuza:
1. Sharubu-Simba
2. Pembe- Kifaru
3. Sikio- Tembo
4. Shingo-Twiga
5. Doa la Juu-Chui
6. Doa la Chini- Duma
7. Jino- Ngiri
8. Mjusi maji-Mamba
9. Askari-Nyati –Jina hili limetokana na wimbo wa Buffalo Soldier wa Bob Marley<o:p></o:p>
10. Watu Pori-Nyani<o:p></o:p>
11. Endelezeni................<o:p></o:p>
<o:p> View attachment 48032
Nilifikia hapa
View attachment 48037
Mto Rufij ukiuangalia kwa juu
View attachment 48038
Tumetua Stiglers Air Strip
View attachment 48039
Mivumo ukiangalia kwa juu
View attachment 48040

View attachment 48041
Tent
View attachment 48042

View attachment 48043

View attachment 48044

View attachment 48046

View attachment 48047

View attachment 48048
View attachment 48049

View attachment 48050

View attachment 48051


View attachment 48052
Niliambiwa kwamba mbuga ya Selous ilikuwa inaitwa Shamba la Bibi, lakini ikabadilishw ana kupewa jimna la huyu Bwana ambaye alifia katika mbuga hiyo miaka ya 50, inasemekana alikuwa mhifadhi wa mbuga hiyo na ndio akapewa heshima hiyo.
View attachment 48053
Hapa tunapata picnic lunch
View attachment 48054



View attachment 48047

View attachment 48055
</o:p>

<o:p></o:p><o:p></o:p>

Sababu zipi zinafanya wasiwaite majina yao halisi?
 
Gharama zake zikoje mkuu,Mungu akipenda niwapeleke wanangu wakaone Simba live


Angalia usije ukauwa ukoo mzima huko, kwenda kuangalia wanyama wakali unabeba familia yote, nenda kimachale mkuu.
Umekwisha onywa!!!
 
Back
Top Bottom