Safari yangu Nyumbani hivi Karibuni

View attachment 35729h
Ndugu zangu mwezi uliopita nilifika Nyumbani Tanzania na kwa Neema ya Mungu nikajipatia Mke mwema

Ndugu Makondo,
Wewe sema tu umepata mke, maana kwa sasa huwezi kujua kama kumpata huko ni dalili za neema za Mungu kweli au ni balaa na kwa hakika hujui kama ni mwema au mwovu. Subiri siku ziende halafu tuandikie tena. Huenda ukawa na maoni tofauti kuhusu yeye! Kwa sasa nakushauri tu uombe, tena sana, ili kweli awe mwema. Good luck and all the best.
 
Hongera sana!
Ushauri wangu kwenu.. Muwe wabunifu ktk mambo yenu yote hasa yale mambo yetu. Mkikosa ubunifu mtajikuta mnakinai mlo mapemaaaa! Leo nazi kidogo, kesho chukuchuku na chachandu pembeni.
Mume; Ukigombana na mkeo usibadili muda wa kurudi nyumbani kwa kuchelewa, badala yake rudi mapema kuliko.
Mke; Ukigombana na mumeo usilale na dengirizi (jeans) badala yake piga kanga moja ikibidi hata bilabila.
Msisahau kuwaleta wajukuu huku nyumbani waje watuone nasi tuwaone. Muwafundishe maadili ya kinyumbani bila kusahau kuwaimbia nyimbo zetu tamu... Si mnazikumbuka!!
MUNGU AWABARIKI SANA!!
 
<font size="3"><font color="#ff0000">Mkuu huyo ni mimi kabisaaaa na ahsanteni sana ndugu zangu, &quot;Apataye mke apata kitu chema kutoka kwa Mungu&quot;</font></font>
<br />
Kama kweli ni wewe hongera sana na ndoa ydumu iwena umri sawa na maisha yenu. Kama si wewe baraka hizi ziwe kinyume chake<br />
 
Mkuu hivi kwanini hukuchukua huko huko ulikototoka? Huyu ulitafutiwa na wazazi au ulimwacha kabla hujaondoka kwenda kokote ulikokuwa?
Mkuu huyu nilimwacha huko nyumbani kabla sijaja hapa nilipo kwa sasa so majira yalipofika nikarudi nyumbani kwenda kukamilisha shuhuli yenyewe. Kama ningetafuta mwingine hapa nilipo hii inamaanisha kwamba mtu angeachwa solemba huko nyumbani jambo ambalo nadhani si la kiungwana
 
Hakika hii ni habari njema sana....
Ninamaono katika familia yenye furaha na upendo mwingi
 
Mke mwema utajua baada ya silver jubilee.....................kwa sasa keep on wishing...........................it is good for the heart too.......
 
View attachment 35729hNdugu zangu mwezi uliopita nilifika Nyumbani Tanzania na kwa Neema ya Mungu nikajipatia Mke mwema
Makondo.......nianze kwa kukupa hongera kwa kupata mke.pili nimpongeze mkeo kwa kukupata weye makondo.Tatu niwatakieni maisha yenye kheri,amani na upendo kama familia,Nne nikushauri kuwa kwa kuwa una familia anza kudunduliza vijisenti kwa ajili ya familia,tumuombe mungu awajalie watoto na muweze kuwalea, Hata hivyo fahamu kuwa kuna njia nyingi za kujikwamua kiuchumi,ikiwa ni pamoja na kuanzisha biashara ndogondogo na kujiwekea akiba kwa ajili ya baadaye, ikiwa ni pamoja na kujiunga JE SACCOS ambayo hivi karibuni washirika walikutana na kamati ya muda ambapo afisa ushirika alitoa mada kuhusu ushirika,udhubutu wa uwekezaji,faida za ushirika na mengi mengineyo.Tembelea jukwaa la biashara kwa taarifa zaidi,Na mwisho,usisahau kukaribisha mkeo jamvini,hongera sana na msalimie mkeo.....kwa taarifa tuu,ni kwamba kiingilio pamoja na hisa ni kiasi cha tzs 120,000 nakushauri uwahi mara moja
 
Mhhhh,

Uchokozi mwingine sasa umezidi kipimo. Ngoja nikaongee na wanasheria wangu..Tumehangaika sana kumtafuta huyu dada...She was/is my......!!!

Nitakuja baadaye na thread ya kuoma michango ya hali na mali ili nikaoneshe dunia kwamba na mimi nikidume, kinachoweza kupambana ili kukomboa mali zake.

Ahsanate sana Makondo kwa msaada wako!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom